Shida iko wapi wajameni, nafikiri mleta mada labda alichokosea kutumia hilo neno ''10%'' ambalo ktk mazingira yetu linahusishwa na rushwa, lakini ujumbe wake ni wa kawaida kabisa: Anatafuta agent atakayemuunganisha na clients/customers na malipo ya huyo agent ni 10% ya fee atakayolipwa na huyo client/customer.
Tatizo liko wapi? tuko kwenye ulimwengu ambao Taarifa ndio msingi wa uchumi wa kisasa (Information based economy) na taarifa ina thamani kubwa sana, kwa kutambua hilo mleta mada anaona yeyote atakayempa 'taarifa' kuhusu wapi anaweza kuuza ujuzi wake wa kutengeneza website basi yeye hana budi kumlipa na anaona ''10%'' ya kile atakachopata ni sawia.