Habari za jumapili wakuu. Ngoja tujikumbushe kidogo usafi kwa kinadada. Yawezekana uzi kama wa aina hii ushaletwa ila sio mbaya, lengo ni kujenga mahusiano.
Moja kwa moja kwenye mada. Jamani kinadada hebu tukumbuke kufanyia usafi vitu vyetu tunavyotumia usiku. Utakuta mdada kila siku kasuka nywele za bandia aidha weaving au les wig ambazo zinatakiwa kuwa covered na kitambaa au kofia nyepesi. Lakini cha kushangaza hata siku moja kwa wiki hawezi kufua hako ka kofia kake.
Sasa shida ni kwamba joto jumlisha hizo weaving ambazo mtu anataka kukaaa nazo mwezi au zaidi zinavyotoa harufu ya uvundo. Na hataki kuziosha hata mara moja kwa wiki kisa zitalegea. Hapo kishapakwa mafuta ya sulphar kuzuia kuwashwa. Basi tena hana haja ya kuziosha. Basi ni uvundo mwanzo mwisho.
Matokeo yake anamkwaza mwenzi wake kuwa naye karibu hasa wakati wa majambozi usiku. Jamani sio jambo jema hawa kinababa tunaweza kusema wana michepuko kumbe ni sisi wenyewe tunaharibu kutokana na kutokuwa wasafi.
Muhimu. fua kofia ya kichwani ,au kitambaa chako cha kulalia mara nyingi uwezavyo.
Jitahidi kuosha nywele angalau mara moja kwa wiki hata kama umesuka weaving au nywele zingine za bei juu. Biashara ya kusema hadi zirudishe chenji tuache.
Mafuta yanayowakera wenzi wetu tusipake, maana yataweza kumnyima furaha ya kuwa na wewe usiku katika ile habari ya kutafuta kuitwa mama fulani.
Ni hayo tu.