MUHIMU KWA KESI ZA EPA, must read!

UFASHE MLIBHONA

Senior Member
Nov 28, 2012
177
0
Usione ajabu mzee, hapo ndipo tulipo. Kwa sasa hatuna serikali wala uongozi nchi inajiendea tu. Amefariki mkuu wa majeshi mstaafu. Amiri jeshi mkuu hakwenda kumzika. mtu ambaye ndiye anamuweka madarakani, anamlinda. Haya maajabu nafikiri hayajawahi kutokea yanazidi ya musa hata yale ya filauni
 
Takalani Sesame

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
588
170
Mkuu Ubungoubungo,
Hujui nature ya wanasiasa kupenda ujiko mbele ya jamii? Sasa kati ya Boniface na kina Kanumba nani alikuwa maarufu mbele ya jamii? Sio kwa wanasiasa tu mkuu. Je uliona coverage ya media kuhusiana na kifo cha Boniface ukilinganisha na vifo vya hao wasanii?

Inasikitisha lakini ndio hivyo tena tumeshafika huku ambapo ze comedy ni maarufu na wanagusa maisha ya watu kuliko hata jopo la madaktari bingwa wanaokesha kuokoa maisha ya mgonjwa au wanasayansi ambao wanapigana kila siku na kuumiza vichwa kugundua majibu ya matatizo yanayotukabili katika nyanja fulani.
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Pretty sad indeed.

Lakini tusiwahukumu wanasiasa bila sababu za msingi, kwani sijui ni wangapi waliokuwa wanamfaham marehemu Boniface.
Kila ofisi au tasnia ina mashujaa wake, mfano mimi leo ndio nimesikia habari za huyo Mzalendo Boniface.

Je mazingira ya kifo chake ni yapi? Ni nini kinaendelea kwenye majalada aliyokuwa akifanyia kazi?
 
englibertm

JF-Expert Member
May 1, 2009
9,256
2,000
Ina wezekana pamoja na kuwa jembe alikuwa anajulikana hapo ofisni kwake tu,pili hata taarifa za kifo chake hazikusambaa kwahiyo tusiwahukumu kama hayo mawili juu ni sahihi.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,130
2,000
Dah ! ndugu pole sana na asante sana kwa taarifa nzuri , japo umechelewa kidogo kujua uharamia wa viongozi wa nchi hii , always watakutumia then wanakutelekeza , ndiyo maana tunahangaika kutwa kucha kuwang'oa , nadhani sasa hata wewe unatuelewa !
 
Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,211
2,000
Hili ni swali najiuliza kila siku na si mara moja nimeliuliza hapa JF.....

Hivi watanzania unafiki nani alitufundisha?

I am very serious kwenye hili, maana ni nadra sana kuwakuta watanzania halisi kwa blood na aliyekulia nchini kuwa sincere and honest tofauti sana na watu wengi niliokutana nao huku duniani...Hata wa Nija (Nigerians) japo wengi wanaaminika ni matapeli lakini wana kuwa very sincere at times na wanaamua kuku deal wazi wazi ukiwavurugia mambo yao. Mtanzania (wengi wetu) atakwambia hakuna tatizo ukijua kweli kumbe moyoni kakuhifadhi....Na ukiona mtanzania anasifia mtu ni yule ambaye majority wana mtambua...Yeye kama yeye hawezi simama na ku-appreciate mtu kwa kitu chochote peke yake bila kuhitaji wengine kumuunga mkono....This is a very good research topic kwa watu wa pyschology na human behaviour (It is very important maana bila kujua chanzo hili taifa litakumbwa na matatizo ya kiuuongozi)....

Ajabu ni kuwa hata wewe ukiishi honest and sincere life watanzania wa arround you watakutahadharisha...be careful! I wonder where is this habit/attitude from...Je ni makuzi, elimu ama muundo wa uongozi wa serikali iliyokuwa na itikadi ya kutishia watu?

Kutokana na maelezo yako hii ni typical of Tanzanians kuanzia viongozi mpaka raia...Ni kwasababu hii nitatengeneza mradi kushirikiana na wenzagu wa University of Dar es salaam University (Sociology na psychology specialists) kuelewa kiini cha haya matatizo ni nini....Kwa sasa my main hypothesis ni siasa ya Ujamaa na kujitegemea hasa wakati wa Mwl Nyerere kwasababu mwl was very smart kila mtu akamwogopa badala ya ku-forwad arguments zao.....So kwakua alikuwa Rais (Role model) kwa wengi basi kila alilosema hata kama binadamu wa kawaida alikosea hakukuwa na wakumkosoa na viongozi wengine wote pamoja na wazazi waka-iga hiyo style kwamba mkubwa hakosei ndiyo maana kukawa na maneno kama zidumu fikra za kiongozi so and so.....as a result kila mtu anatafuta umaarufu, ukubwa, heshima pasipo kuwa na substance in it na wale ambao wanaokuwa visible ndiyo wanaotafutwa na wengi kusifiwa siyo wale wenye quite spirit na utendaji mzuri....
 
Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,211
2,000
Pretty sad indeed.

Lakini tusiwahukumu wanasiasa bila sababu za msingi, kwani sijui ni wangapi waliokuwa wanamfaham marehemu Boniface.
Kila ofisi au tasnia ina mashujaa wake, mfano mimi leo ndio nimesikia habari za huyo Mzalendo Boniface.

Je mazingira ya kifo chake ni yapi? Ni nini kinaendelea kwenye majalada aliyokuwa akifanyia kazi?

Ukimsoma vizuri mleta mada....Haikutakiwa Boniface asijulikane..Tatizo ni je hizo (character zake ) ni interesting kwenye ears za watanzania? Kila jamii inamambo ambayo inashabikia then it means Boniface being a Tanzanian na kwa culture ya watanzania hiyo siyo habari maana watu wachapakazi na wasiopenda usanii na sifa za kijinga siyo watu wanaopendwa kusikika katika kile ambacho watanzania watakiita habari..'News'....Wa kumleta Boniface kwenye ears za watanzania ni wanahabari nao hawawezi leta habari ambayo siyo 'news' maana siyo preference ya consumers wao...Then we come back to the conclusion wengi wa watanzania wanapenda watu wanafiki na wasanii...

Ukipenda kujua ukweli wa hili angalia thread zinazoshabikiwa na wana JF ambao ni representative wa informed group ya watanzania.....Leta habari ya fisadi fulani kasikika yupo so and so.....Kiongozi fulani kafumaniwa.....Kikombe cha babu kimetibu na kuua wangapi....utakuta ni uzinzi, wizi, ushirikina ndiyo news za wengi wetu....So hizi habari za wakili mahiri utazisoma sangapi wakati thread za jinsi hizi hazisomwi na wengi? Je waleta habari wataleta thread za jinsi hiyo?

Kuna rafiki yangu mmoja alinipa ushauri..mzuri tu kwakweli..kwamba nikipenda wengi wanisome basi niache kuandika habari kuhusu imani yangu na niandike za profession yangu...Swali likanijia hivi mimi objective yangu ya kuhabarisha wengine ni ipi? Kama preacher basi ni kuhusu imani yangu kwanza na taaluma yangu inafuata baada ya imani yangu..Sasa nikiacha hivi nitakuwa naishi ndani ya dhamira yangu au nitakuwa na ishi kwa kuiga wengine? its either na endelea kuandika hizo habari kwa as few as watakaopenda kusoma ama naacha kabisa maana ni kupoteza muda kufanya jambo ambalo si objective yangu...

Watanzania wengi wanatatizo la kujitambua na kujiamini...sababu bado sijaijua lakini naitafuta na soon will be informed of why watanzania wanashindwa kujitambua na kujiamini badala yake wanapenda kuiga mno na kufuata mkumbo.
 
Ngagarupalu

Senior Member
Oct 13, 2012
156
0
Pole sana ubungoubungo, ukweli inatia huzuni kuona watu muhimu hawatajwi, na hata hawazikwi!!
Hapa najifunza mengi, mojawapo, tunapoteza uzalendo, hatuna vipaumbele na zaidi hatuna waandishi wa habari wenye weredi wa kutosha kwenye tasnia mbalimbali, hivyo habari nyingi hazipatikani accordingly!!
Ina wezekana pamoja na kuwa jembe alikuwa anajulikana hapo ofisni kwake tu,pili hata taarifa za kifo chake hazikusambaa kwahiyo tusiwahukumu kama hayo mawili juu ni sahihi.
Ndugu unataka mtu ajitangaze nje ya ofisi yake? au atangazwe kwa kazi zake? watu leo tunasoma udaku tu, wangapi wanajua kesi za EPA, DOWANS, etc ( kwa kifupi habari za mahakama, afya, Elimu, etc) zaidi siasa na udaku!!
watu walijaa kwenye kesi ya Mh Lema, mbona kwa kezi za DOWANS, EPA, hawajai????????
Waandishi mpo wapi kutupatia habari?
wakatabau
 
tetere

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
963
225
Ithink ni tatizo la priority sio tu katika eneo la kazi, bali pia katika mahusiano yetu na watu. Ni kweli kuwa kuwa katika jamii zetu wale wenye pesa huwa wanapata wahudhuriaji wengi kuliko wale wasiokuwa na pesa (katika mazishi). Na hili ni tatizo sugu. And this is another form of violation of principles of life. Maana kumzika mtu - hufanyi hivi kwa ajili aliyekufa, bali unafanya hivyo kwa ajili ya yako mwenyewe na wale wanaoishi. Huwezi kumbagua mtu wa kumheshimu. Kama unaheshimu UTU hii ni principle hata kama humpendi unaeelekeza heshima kwake, lakini unasimamia principle - unaonyesha heshima.
Kuhudhuria mazishi sio kulipa deni - kwa hiyo usijeuliza mbona anahudhuria ya wenzie na yeye ya kwake hawakuhudhuria. Unahudhuria mazishi kwa sababu unaamini katika kutoa mapenzi kwa waliofiwa na wanaoyahitaji mapenzi (Its a principle). Ukisimamia principle hii huwezi kubagua au kuonekana unabagua watu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,119
2,000
KUNA MAKALA MOJA NILISOMA JUU YA KESI ZA EPA na uendeshaji pale kisutu. kwa bahati nzuri, mimi kama mwanasheria wa kujitegemea kwa muda mrefu, kuna jambo limekuwa likiniuma sana, na ni muhimu watu wajue.

wakati KANUMBA alipokufa, viongozi hata wa serikali wengi walihudhuria, wabunge walihudhuria, na watu wa vyama mbalimbali. WAKATI SHAROBARO alipokufa, NAPE alienda kule na wengine wakuu wa wilaya sijui. kanumba na sharo walikuwa watz waliotoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia sanaa zao, hilo halipingiki na walistahili misiba yao kufanyiwa vile ilivyofanyiwa. ajabu yake, kuna mtu mmoja alikufa pale kwa DPP, ni kijana ambaye nimefanya naye kwazi kwa muda mrefu yeye kama wakili wa serikali, anaitwa marehemu BONIFAS. huyu ni mashine ambayo imekuwa ikiendesha kesi nyingi sana na tegemeo kubwa kwa kesi za epa, na zile kuukuu, conviction nyingi zinatokea pale kisutu , appeal zote, kesi ya MURO ambayo rushwa ilitembezwa sana ushaidi upo wazi lakini hakimu akaamua atakavyo pamoja na rushwa za mahakimu, yeye ndiye amekuwa kiongozi. ni mara nyingi ametishiwa hadi maisha kwasababu ya kesi za epa. lakini alipokufa, hakuna kiongozi hata mmoja alienda kumzika. hakuna wa chadema, wa ccm, mbunge, waziri, mkuu wa wilaya wala mkoa wala nani. pamoja na kwamba kazi aliyokuwa anafanya ni moja ya kazi hatari mno, ni kazi iliyofunga watu na kurudisha hela zilizoibiwa nyingi. IKUMBUKWE KUWA, PAMOJA NA KWAMBA WATU WENGI WANAFIKIRI WALE WEZI WA EPA HAWAFUNGWI, WENGI TU WAPO WAMEPEWA CONVICTION.

JAMBO KUU ninalopenda kuliongea hapa ni seriousness ya serikali yetu katika kuchangua maeneo ya vipaumbele. kwa bahati, kabla sijaenda private, nilishafanya kazi kama wakili wa serikali kwa muda mrefu, na bado kwenye damu yangu kazi hiyo ipo pamoja na kwamba kwa nje simo tena, niliondoka kwasababu ya maslahi.

ukitembelea pale kisutu, au mahakama yeyote ila ya wilaya, mkazi, mahakama kuu au rufaa, utawakuta mawakili wa serikali na visuti vyao vyeusi, wanashitaki watu badala ya serikali. hawa ni watu wanaobeba maslahi ya umma sana, wanaitetea serikali na kushitaki watu badala ya serikali ili uhalifu upungue. lakini mchango huu hautambuliwi sawia na serikali kiasi kwamba ilishindwa HATA KWENDA KUMZIKA BONIFAS, ambaye kwa kifo chake ni furaha kubwa kwa akina MRAMBA na akina KATITI etc ambao kesi zao bado zinaendelea pale kisutu. hakika yake, bonifas akiwa anatoa submissions zake, hadi mahakimu wengine walikuwa wanaacha mahakama zao wanaenda kumsikiliza ili wajifunze, kwasababu alikuwa na uzoefu wa muda mrefu mno na mahakimu wa kisutu wenyewe walikuwa wanajifunza toka kwake. wakili gani wa kujitegemea alikuwa na ujasiri wa kutosha mbele yake? amehatarisha maisha yake kwa kitambo kwa kazi hizi za kujitoa mhanga, lakini HATA SERIKALI NGAZI ZA JUU WALE WALIOENDA KUMZIKA KANUMBA HAWAKUJA KWAKE. sijui niseme ni aibu kwa serikali au ni nini, au tuseme hujali ili waonwe tu ila haitoki moyoni.

pamoja na polisi kujitahidi kuharibu ushahidi wa kesi mara nyingi (wao ndio wapelelezi, prosecutors wanaletewa tu vitu ili wa present mahakamani kisheria), mawakili wa serikali bado wameendelea kufanya kazi katika mazingira magumu, fungu na hawatambuliwi sana. hivi wakila rushwa tutawalaumu? wakiharibu kesi tutawalaumu? ulinzi wao uko wapi? mbona ulinzi wao tofauti na ule tunaouona pccb? unajua ni wangapi wanaikimbia hiyo ofisi karibia kila mwezi? watu wanaajiriwa wanaona uzushi wanaacha wanakuja kwenye private, kwasababu ya mambo kama haya. unaitumikia serikali kwa kujitoa mhanga kwenye mazingira magumu ya kutishiwa na washitakiwa ambao haujui watakuvamia saa ngapi, halafu mtu kama bonifas akifa mawaziri hata rais hawaji; kama kazi ya yule jamaa ingekuwa imeandikwa kwenye magazeti na kesi zake zote zile, hakika rais angekuja kwasababu ule mchakato wa mafisadi wa epa na wengine bonifas ndiye aliyekuwa mashine pale kisutu na mahakama kuu etc kuhakikisha kesi zinaenda vizuri. NI JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKINIUMA KWA MUDA MREFU, NASHUKURU NIMELITUA KWA JAMII ILI MZIGO MOYONI MWANGU UTULIWE. kama tunataka wahalifu, mafisadi etc wafungwe na kurudisha mali zetu, ni lazima wale wanawashugulikia tuwapromote na kuonyesha tunawajali. mishahara yao midogo, hata kwenda kuwazika jamani mmeshindwa? kama kuna mtu alihudhuria ule msima atajua ninachoongea hapa.....yule jamaa likuwa na hadhi ya jaji, hata majaji wenyewe akiwa high court akiongea walikuwa wanamsikiliza kwa makini ili wapate vitu toka kwake, ilikuwa mashine kubwa sana, na taifa hili limepoteza mtu muhimu sana ambaye mchango wake kwa jamii haujatambulika hadi sasa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Hapo kwenye red Mkuu nadhani umeteleza kidogo!Japo msiba wake haukupewa uzito uliokuwa unastahili,lakini nakumbuka siku ya mazishi Waziri wa sheria wakati huo bwana Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali bwana Werema,walikuwa ni miongoni mwa waombolezaji wa msiba huo.
 
Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,434
1,500
Boniphace atamsaidia nini mwanasiasa? wao wanatafuta umaarufu na sio umuhimu, idadi ya kamera na audience ingewavutiaje kina Nape na aina ya siasa zao za leo? pole ila ndo tulipofika.
 
Mlangaja

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
565
250
Mwenyezi Mungu awape nguvu watu kama hawa. Naamini ngozi ya unyayo ingetaka leo iwe usoni, hakuna angeweza kukanyaga. Mungu ameviumba vyote ili vifanya kazi kwa ushirikiano. Dharau zinatoka kwa shetani na ccm inaongozwa na shetani. Kwa hakiki vyote yaani shetani na sisiem vitakwisha lakini wema wataendelea kuwepo. Jina lake Boniface liandikwe kwenye mwamba kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi. Na yote ya ccm yaandikwe kwenye mchanga kwa mti na upepo utakapopita vyote vifutike. Mungu na atutolee chaka hili na mafisadi, wala rushwa, waongo, wauaji na wenye kiburi. Mungu mwenye nguvu awainue masikini na waliodharauliwa na kuwapa kiti chake. Amina.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Mpeni sifa Yesu

JF-Expert Member
May 23, 2010
649
0
Hapo kwenye red Mkuu nadhani umeteleza kidogo!Japo msiba wake haukupewa uzito uliokuwa unastahili,lakini nakumbuka siku ya mazishi Waziri wa sheria wakati huo bwana Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali bwana Werema,walikuwa ni miongoni mwa waombolezaji wa msiba huo.
ni kweli, nilihudhuria msiba ule, waziri huyo wa sheria na mwanasheria mkuu walikuja. lakini napenda kumuunga mkono huyo mtoa mada, waziri huyo na mwanasheria mkuu ni maboss wake toka kwenye ofisi yake. viongozi wa chadema, cuf na ccm, wabunge na wanasiasa weingine kwa ujuma, legal and human rights centre and others, waandishi wa habari za magazeti tv radio etc, wote hawa wamekuwa wakiongea sana kuhusu ufisadi katika nchi hii, wizi wa epa ulifunika nchi nzima, kila chombo cha habari kilikuwa kinaliongelea, lakini wezi wale wachache walipokamatwa, waongeaji wale wamenyamaza kimyaaa kumbe mzigo na hatari ziko mikononi mwa vijana pale kwa DPP. najua hiyo ni kazi yao wanatakiwa kuifanya lakini wale waongeaji na washabiki sana wa kesi za epa walienda wapi? kina zitto walienda wapi? kina slaa, nape na wanasiasa wote walikuwa hawajui nani anaendesha kesi hizi za epa? ninakubali kuwa wanasiasa na hata vyombo vya habari vingi ni wanafiki (pamoja na kwamba si vyote tuseme hivyo), namjua bon, nilishawahi kufanya naye kazi. pale kwa dpp wamempoteza mtu mwenye akili sana, pamoja na kwamba najua bado wapo vijana ambao wapo pale aliowafundisha kazi najua kuondoka kwake ni pengo kubwa sana. rai yangu ni kwa serikali kufuatilia mambo na kuwatia moyo wananchi wanaojitolea. mkiwatupa wapiganaji namna hiyo kama inavyoongelewa hakika yake watu wataichukia nchi na hawatakuwa wazarendo kwenye nchi yao, na hao vijana watakula rushwa hapo na kesi zote watawaharibieni kwa taarifa yenu....watieni moyo waone kuna mtu anayeappreciate kazi yao. ni kazi ya hatari sana hiyo, wengine sisi tulishaikimbia.
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,948
2,000
R.I.P. BON.
Umeondoka lakini kazi yako itabaki.
Haki haipotei ila inaweza kucheleweshwa.Wahusika waliobaki hakikisheni mnamuenzi Bon kwa yale mazuri aliyo yaacha.
Mtusaidie mafisadi wafungwe na warejeshe mali walizoiiba.Mtumie mitandao kufichua uozo unaoendelea maana Media inaonekana kushika kasi kama muhimili mpya unaoweza kuleta mabadiliko katika jamii baada ya ile mitatu kutufikisha tulipo.
 
Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
745
250
Ame!!!
Wa-TZ wanamatatizo ya kujiamini. Asilimia 88% hadi tisini ya wa-TZ hawaamini wanachokisema wala kukifanya!!
Siku ukikutana na mfanyakazi au raia anayeamini anachokisema utasikia ama anapewa jina la Mchawi au usalama wa Taifa au ana link na Wamarekani. hayo yote ni matekeo ya kutojiamini!! ambalo ni zao la uvivu!!
Kuhusu wanasiasa kutohudhulia huo msiba .... sidhani kama kuna politician anayeenda msibani kwa kuguswa na huyo aliyekufa zaidi ya kutafuta idadi ya wananchi watakaovutiwa naye. they never mean what they do at the funeral!! ndio maana kama mtu si maarufu hata kama alikuwa national patriot hakuna atakayepoteza muda wake!!

Hili ni swali najiuliza kila siku na si mara moja nimeliuliza hapa JF.....

Hivi watanzania unafiki nani alitufundisha?

I am very serious kwenye hili, maana ni nadra sana kuwakuta watanzania halisi kwa blood na aliyekulia nchini kuwa sincere and honest tofauti sana na watu wengi niliokutana nao huku duniani...Hata wa Nija (Nigerians) japo wengi wanaaminika ni matapeli lakini wana kuwa very sincere at times na wanaamua kuku deal wazi wazi ukiwavurugia mambo yao. Mtanzania (wengi wetu) atakwambia hakuna tatizo ukijua kweli kumbe moyoni kakuhifadhi....Na ukiona mtanzania anasifia mtu ni yule ambaye majority wana mtambua...Yeye kama yeye hawezi simama na ku-appreciate mtu kwa kitu chochote peke yake bila kuhitaji wengine kumuunga mkono....This is a very good research topic kwa watu wa pyschology na human behaviour (It is very important maana bila kujua chanzo hili taifa litakumbwa na matatizo ya kiuuongozi)....

Ajabu ni kuwa hata wewe ukiishi honest and sincere life watanzania wa arround you watakutahadharisha...be careful! I wonder where is this habit/attitude from...Je ni makuzi, elimu ama muundo wa uongozi wa serikali iliyokuwa na itikadi ya kutishia watu?

Kutokana na maelezo yako hii ni typical of Tanzanians kuanzia viongozi mpaka raia...Ni kwasababu hii nitatengeneza mradi kushirikiana na wenzagu wa University of Dar es salaam University (Sociology na psychology specialists) kuelewa kiini cha haya matatizo ni nini....Kwa sasa my main hypothesis ni siasa ya Ujamaa na kujitegemea hasa wakati wa Mwl Nyerere kwasababu mwl was very smart kila mtu akamwogopa badala ya ku-forwad arguments zao.....So kwakua alikuwa Rais (Role model) kwa wengi basi kila alilosema hata kama binadamu wa kawaida alikosea hakukuwa na wakumkosoa na viongozi wengine wote pamoja na wazazi waka-iga hiyo style kwamba mkubwa hakosei ndiyo maana kukawa na maneno kama zidumu fikra za kiongozi so and so.....as a result kila mtu anatafuta umaarufu, ukubwa, heshima pasipo kuwa na substance in it na wale ambao wanaokuwa visible ndiyo wanaotafutwa na wengi kusifiwa siyo wale wenye quite spirit na utendaji mzuri....
 
kibodi

Member
Jul 2, 2012
88
0
Thread yako imenitoa machozi mkuu. Huyu Bonifasi namfahamu na mara kadhaa nilishuhudia umahili wake mahakamani. Ulichoandika juu yake hapa ni ukweli mtupu. Nakupongeza.
 
Ng'azagala

JF-Expert Member
Jun 7, 2008
1,287
1,250
KUNA MAKALA MOJA NILISOMA JUU YA KESI ZA EPA na uendeshaji pale kisutu. kwa bahati nzuri, mimi kama mwanasheria wa kujitegemea kwa muda mrefu, kuna jambo limekuwa likiniuma sana, na ni muhimu watu wajue.

wakati KANUMBA alipokufa, viongozi hata wa serikali wengi walihudhuria, wabunge walihudhuria, na watu wa vyama mbalimbali. WAKATI SHAROBARO alipokufa, NAPE alienda kule na wengine wakuu wa wilaya sijui. kanumba na sharo walikuwa watz waliotoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia sanaa zao, hilo halipingiki na walistahili misiba yao kufanyiwa vile ilivyofanyiwa. ajabu yake, kuna mtu mmoja alikufa pale kwa DPP, ni kijana ambaye nimefanya naye kwazi kwa muda mrefu yeye kama wakili wa serikali, anaitwa marehemu BONIFAS. huyu ni mashine ambayo imekuwa ikiendesha kesi nyingi sana na tegemeo kubwa kwa kesi za epa, na zile kuukuu, conviction nyingi zinatokea pale kisutu , appeal zote, kesi ya MURO ambayo rushwa ilitembezwa sana ushaidi upo wazi lakini hakimu akaamua atakavyo pamoja na rushwa za mahakimu, yeye ndiye amekuwa kiongozi. ni mara nyingi ametishiwa hadi maisha kwasababu ya kesi za epa. lakini alipokufa, hakuna kiongozi hata mmoja alienda kumzika. hakuna wa chadema, wa ccm, mbunge, waziri, mkuu wa wilaya wala mkoa wala nani. pamoja na kwamba kazi aliyokuwa anafanya ni moja ya kazi hatari mno, ni kazi iliyofunga watu na kurudisha hela zilizoibiwa nyingi. IKUMBUKWE KUWA, PAMOJA NA KWAMBA WATU WENGI WANAFIKIRI WALE WEZI WA EPA HAWAFUNGWI, WENGI TU WAPO WAMEPEWA CONVICTION.

JAMBO KUU ninalopenda kuliongea hapa ni seriousness ya serikali yetu katika kuchangua maeneo ya vipaumbele. kwa bahati, kabla sijaenda private, nilishafanya kazi kama wakili wa serikali kwa muda mrefu, na bado kwenye damu yangu kazi hiyo ipo pamoja na kwamba kwa nje simo tena, niliondoka kwasababu ya maslahi.

ukitembelea pale kisutu, au mahakama yeyote ila ya wilaya, mkazi, mahakama kuu au rufaa, utawakuta mawakili wa serikali na visuti vyao vyeusi, wanashitaki watu badala ya serikali. hawa ni watu wanaobeba maslahi ya umma sana, wanaitetea serikali na kushitaki watu badala ya serikali ili uhalifu upungue. lakini mchango huu hautambuliwi sawia na serikali kiasi kwamba ilishindwa HATA KWENDA KUMZIKA BONIFAS, ambaye kwa kifo chake ni furaha kubwa kwa akina MRAMBA na akina KATITI etc ambao kesi zao bado zinaendelea pale kisutu. hakika yake, bonifas akiwa anatoa submissions zake, hadi mahakimu wengine walikuwa wanaacha mahakama zao wanaenda kumsikiliza ili wajifunze, kwasababu alikuwa na uzoefu wa muda mrefu mno na mahakimu wa kisutu wenyewe walikuwa wanajifunza toka kwake. wakili gani wa kujitegemea alikuwa na ujasiri wa kutosha mbele yake? amehatarisha maisha yake kwa kitambo kwa kazi hizi za kujitoa mhanga, lakini HATA SERIKALI NGAZI ZA JUU WALE WALIOENDA KUMZIKA KANUMBA HAWAKUJA KWAKE. sijui niseme ni aibu kwa serikali au ni nini, au tuseme hujali ili waonwe tu ila haitoki moyoni.

pamoja na polisi kujitahidi kuharibu ushahidi wa kesi mara nyingi (wao ndio wapelelezi, prosecutors wanaletewa tu vitu ili wa present mahakamani kisheria), mawakili wa serikali bado wameendelea kufanya kazi katika mazingira magumu, fungu na hawatambuliwi sana. hivi wakila rushwa tutawalaumu? wakiharibu kesi tutawalaumu? ulinzi wao uko wapi? mbona ulinzi wao tofauti na ule tunaouona pccb? unajua ni wangapi wanaikimbia hiyo ofisi karibia kila mwezi? watu wanaajiriwa wanaona uzushi wanaacha wanakuja kwenye private, kwasababu ya mambo kama haya. unaitumikia serikali kwa kujitoa mhanga kwenye mazingira magumu ya kutishiwa na washitakiwa ambao haujui watakuvamia saa ngapi, halafu mtu kama bonifas akifa mawaziri hata rais hawaji; kama kazi ya yule jamaa ingekuwa imeandikwa kwenye magazeti na kesi zake zote zile, hakika rais angekuja kwasababu ule mchakato wa mafisadi wa epa na wengine bonifas ndiye aliyekuwa mashine pale kisutu na mahakama kuu etc kuhakikisha kesi zinaenda vizuri. NI JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKINIUMA KWA MUDA MREFU, NASHUKURU NIMELITUA KWA JAMII ILI MZIGO MOYONI MWANGU UTULIWE. kama tunataka wahalifu, mafisadi etc wafungwe na kurudisha mali zetu, ni lazima wale wanawashugulikia tuwapromote na kuonyesha tunawajali. mishahara yao midogo, hata kwenda kuwazika jamani mmeshindwa? kama kuna mtu alihudhuria ule msima atajua ninachoongea hapa.....yule jamaa likuwa na hadhi ya jaji, hata majaji wenyewe akiwa high court akiongea walikuwa wanamsikiliza kwa makini ili wapate vitu toka kwake, ilikuwa mashine kubwa sana, na taifa hili limepoteza mtu muhimu sana ambaye mchango wake kwa jamii haujatambulika hadi sasa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Hapo kwenye red Mkuu nadhani umeteleza kidogo!Japo msiba wake haukupewa uzito uliokuwa unastahili,lakini nakumbuka siku ya mazishi Waziri wa sheria wakati huo bwana Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali bwana Werema,walikuwa ni miongoni mwa waombolezaji wa msiba huo.

hata mimi nilishiriki kwenye msiba, si kweli kwamba viongozi hawakushiriki kwani DPP, Mwanasheria mkuu walikuwa wanashinda kwenye msiba, pia niliwaona mawaziri kadhaa na hata wakati wa mazishi kinondoni alikuwepo Waziri wa Sheria na naibu wake yaani Chikawe na yule Mama, pia walikuwepo wabunge kadhaa na viongozi wa kisiasa, watu wa Ikulu, DPP, mwanasheria mkuu nk. labda ungesema hakuwepo JK au Nape lakini waliwakilishwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom