MUHIMU KWA KESI ZA EPA, must read!

Anachosema Ubungoubungo ni kuwa kazi aliyokuwa anaifanya Learned Boniface ilikuwa ni ya kutukuka kwa Serikali. Viongozi serikali walilijua hili. Wanasheria wenzake, Majaji na wanasheria wa kujitegemea waliuenzi na kuheshimu utumishi wake. Sisi wengine wa magazeti ya udaku hatujui. Lakini sio anaotudai tungehudhuria, anawadai wanaojua. Ukiachilia mbali viongozi wa kisiasa je; kuna wanataaluma wenzake wangapi walioguswa na kifo cha Boniface?
Watanzania wengi moyo wa upendo wa dhati hawana. Watanzania wa sasa kwa kila jambo wanajiuliza watafaidika nalo vipi leo au kesho. Jambo la jana halina thamani teni mioyoni mwa watanzania. Sio kweli kwamba viongozi wa kisiasa walimpenda sana marehemu Kanumba, hapana! Kwa kuwa sanaa inavuta watu wengine wanasiasa wanataka waonekane wako pamoja na kundi la wasanii na wapenda sanaa. Kundi la wapenda sanaa ni vijana, wasio na kazi hata wamachinga ni wengi kuliko kundi lolote. Wanasiasa hawaendi kwa kuwapenda la hasha, wanaenda kwa maslah ya kesho ya kisiasa zaidi.
Njaa ya kesho ndiyo inayotawala. Mkuu wa majeshi hana kundi na wala hata rudi tena kumlinda Rais. Boniface halikadhalika. Wanasiasa wa Tanzania wanaishi kwa kujipendekeza. Mfano wakuu wa mikoa, wa Wilaya na viongozi wengine wlienda kwenye msiba wa Kanumba kwa kuwa Raisi alikuwepo hivyo hoja ya kuwepo ni ili waonekane na mkubwa.
Ukimsoma vizuri mleta mada....Haikutakiwa Boniface asijulikane..Tatizo ni je hizo (character zake ) ni interesting kwenye ears za watanzania? Kila jamii inamambo ambayo inashabikia then it means Boniface being a Tanzanian na kwa culture ya watanzania hiyo siyo habari maana watu wachapakazi na wasiopenda usanii na sifa za kijinga siyo watu wanaopendwa kusikika katika kile ambacho watanzania watakiita habari..'News'....Wa kumleta Boniface kwenye ears za watanzania ni wanahabari nao hawawezi leta habari ambayo siyo 'news' maana siyo preference ya consumers wao...Then we come back to the conclusion wengi wa watanzania wanapenda watu wanafiki na wasanii...

Ukipenda kujua ukweli wa hili angalia thread zinazoshabikiwa na wana JF ambao ni representative wa informed group ya watanzania.....Leta habari ya fisadi fulani kasikika yupo so and so.....Kiongozi fulani kafumaniwa.....Kikombe cha babu kimetibu na kuua wangapi....utakuta ni uzinzi, wizi, ushirikina ndiyo news za wengi wetu....So hizi habari za wakili mahiri utazisoma sangapi wakati thread za jinsi hizi hazisomwi na wengi? Je waleta habari wataleta thread za jinsi hiyo?

Kuna rafiki yangu mmoja alinipa ushauri..mzuri tu kwakweli..kwamba nikipenda wengi wanisome basi niache kuandika habari kuhusu imani yangu na niandike za profession yangu...Swali likanijia hivi mimi objective yangu ya kuhabarisha wengine ni ipi? Kama preacher basi ni kuhusu imani yangu kwanza na taaluma yangu inafuata baada ya imani yangu..Sasa nikiacha hivi nitakuwa naishi ndani ya dhamira yangu au nitakuwa na ishi kwa kuiga wengine? its either na endelea kuandika hizo habari kwa as few as watakaopenda kusoma ama naacha kabisa maana ni kupoteza muda kufanya jambo ambalo si objective yangu...

Watanzania wengi wanatatizo la kujitambua na kujiamini...sababu bado sijaijua lakini naitafuta na soon will be informed of why watanzania wanashindwa kujitambua na kujiamini badala yake wanapenda kuiga mno na kufuata mkumbo.
 
Usiwalaumu.kina nape wao wanachofafanya ni kutafuta misiba inayogusa watu wengi ili wapate kuonyesha hurumabyao kwa maslahi zao kisiasa zaidi. Ila la kaka boniface inawezekana hakupata kusikiza sana sababu ya mazingira ya kazi yake.
 
hata mimi nilishiriki kwenye msiba, si kweli kwamba viongozi hawakushiriki kwani DPP, Mwanasheria mkuu walikuwa wanashinda kwenye msiba, pia niliwaona mawaziri kadhaa na hata wakati wa mazishi kinondoni alikuwepo Waziri wa Sheria na naibu wake yaani Chikawe na yule Mama, pia walikuwepo wabunge kadhaa na viongozi wa kisiasa, watu wa Ikulu, DPP, mwanasheria mkuu nk. labda ungesema hakuwepo JK au Nape lakini waliwakilishwa
usimwongelee dpp wala mwanasheria mkuu. jua kuwa huyu jamaa alikuwa acting deputy dpp, hivyo walikuwa wanakaa floor moja na dpp walitengana tu vyumba, walikuwa wanafanya kazi pamoja pale sukari house, wala mwanasheria mkuu usiseme, ni watu wa ndani ya ofisi. ongelea mawaziri wengine wa nyanja zingine, ongelea watu walioshabikia sana na kulia kwaajili ya mafisadi wa epa na wengine wote hadi kukamatwa kwa watuhumiwa. lakini yule anayewashughulikia hakuthaminiwa na mzigo wote ulibwagwa mikononi mwake. frankly speaking, ilihitajika zaidi ya vile ilivyokuwa, na ninamuunga mkono mtoa mada kwasababu nilikuwa namjua bon pia, alifanya kazi pale kwa miaka nadhani zaidi ya 15.
 
Nakubaliana na mleta mada kuwa kifo cha Bonifasi na mazishi yake yalichukuliwa katika Low profile sana!!!! Kuna walioshangilia!!! But nasikia alitoka katika safari na umauti ukamkuta usiku!!! Hivi ni kifo cha ghafla au nini? Haieleweki!!! Ni siri ya Dr. aliyemfanyia uchunguzi!! Kwa hakika nilitegemea iwe ni pigo kwa serikali na wangeonesha ushiriki wao zaidi!! Hao viongozi waandamizi toka wizara ya sheria na kule kwa DPP ni lazima wangekuwepo tu kwa kuwa ulikuwa ni msiba wao!! Nilitegemea levels nyingine senior za serikali ziwepo pia!!! So sad, gone to soon kabla hujamaliza kuwaweka katika pilato wale wa EPA na wengine!! Mysterious death!!
 
KUNA MAKALA MOJA NILISOMA JUU YA KESI ZA EPA na uendeshaji pale kisutu. kwa bahati nzuri, mimi kama mwanasheria wa kujitegemea kwa muda mrefu, kuna jambo limekuwa likiniuma sana, na ni muhimu watu wajue.

wakati KANUMBA alipokufa, viongozi hata wa serikali wengi walihudhuria, wabunge walihudhuria, na watu wa vyama mbalimbali. WAKATI SHAROBARO alipokufa, NAPE alienda kule na wengine wakuu wa wilaya sijui. kanumba na sharo walikuwa watz waliotoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia sanaa zao, hilo halipingiki na walistahili misiba yao kufanyiwa vile ilivyofanyiwa. ajabu yake, kuna mtu mmoja alikufa pale kwa DPP, ni kijana ambaye nimefanya naye kwazi kwa muda mrefu yeye kama wakili wa serikali, anaitwa marehemu BONIFAS. huyu ni mashine ambayo imekuwa ikiendesha kesi nyingi sana na tegemeo kubwa kwa kesi za epa, na zile kuukuu, conviction nyingi zinatokea pale kisutu , appeal zote, kesi ya MURO ambayo rushwa ilitembezwa sana ushaidi upo wazi lakini hakimu akaamua atakavyo pamoja na rushwa za mahakimu, yeye ndiye amekuwa kiongozi. ni mara nyingi ametishiwa hadi maisha kwasababu ya kesi za epa. lakini alipokufa, hakuna kiongozi hata mmoja alienda kumzika. hakuna wa chadema, wa ccm, mbunge, waziri, mkuu wa wilaya wala mkoa wala nani. pamoja na kwamba kazi aliyokuwa anafanya ni moja ya kazi hatari mno, ni kazi iliyofunga watu na kurudisha hela zilizoibiwa nyingi. IKUMBUKWE KUWA, PAMOJA NA KWAMBA WATU WENGI WANAFIKIRI WALE WEZI WA EPA HAWAFUNGWI, WENGI TU WAPO WAMEPEWA CONVICTION.

JAMBO KUU ninalopenda kuliongea hapa ni seriousness ya serikali yetu katika kuchangua maeneo ya vipaumbele. kwa bahati, kabla sijaenda private, nilishafanya kazi kama wakili wa serikali kwa muda mrefu, na bado kwenye damu yangu kazi hiyo ipo pamoja na kwamba kwa nje simo tena, niliondoka kwasababu ya maslahi.

ukitembelea pale kisutu, au mahakama yeyote ila ya wilaya, mkazi, mahakama kuu au rufaa, utawakuta mawakili wa serikali na visuti vyao vyeusi, wanashitaki watu badala ya serikali. hawa ni watu wanaobeba maslahi ya umma sana, wanaitetea serikali na kushitaki watu badala ya serikali ili uhalifu upungue. lakini mchango huu hautambuliwi sawia na serikali kiasi kwamba ilishindwa HATA KWENDA KUMZIKA BONIFAS, ambaye kwa kifo chake ni furaha kubwa kwa akina MRAMBA na akina KATITI etc ambao kesi zao bado zinaendelea pale kisutu. hakika yake, bonifas akiwa anatoa submissions zake, hadi mahakimu wengine walikuwa wanaacha mahakama zao wanaenda kumsikiliza ili wajifunze, kwasababu alikuwa na uzoefu wa muda mrefu mno na mahakimu wa kisutu wenyewe walikuwa wanajifunza toka kwake. wakili gani wa kujitegemea alikuwa na ujasiri wa kutosha mbele yake? amehatarisha maisha yake kwa kitambo kwa kazi hizi za kujitoa mhanga, lakini HATA SERIKALI NGAZI ZA JUU WALE WALIOENDA KUMZIKA KANUMBA HAWAKUJA KWAKE. sijui niseme ni aibu kwa serikali au ni nini, au tuseme hujali ili waonwe tu ila haitoki moyoni.

pamoja na polisi kujitahidi kuharibu ushahidi wa kesi mara nyingi (wao ndio wapelelezi, prosecutors wanaletewa tu vitu ili wa present mahakamani kisheria), mawakili wa serikali bado wameendelea kufanya kazi katika mazingira magumu, fungu na hawatambuliwi sana. hivi wakila rushwa tutawalaumu? wakiharibu kesi tutawalaumu? ulinzi wao uko wapi? mbona ulinzi wao tofauti na ule tunaouona pccb? unajua ni wangapi wanaikimbia hiyo ofisi karibia kila mwezi? watu wanaajiriwa wanaona uzushi wanaacha wanakuja kwenye private, kwasababu ya mambo kama haya. unaitumikia serikali kwa kujitoa mhanga kwenye mazingira magumu ya kutishiwa na washitakiwa ambao haujui watakuvamia saa ngapi, halafu mtu kama bonifas akifa mawaziri hata rais hawaji; kama kazi ya yule jamaa ingekuwa imeandikwa kwenye magazeti na kesi zake zote zile, hakika rais angekuja kwasababu ule mchakato wa mafisadi wa epa na wengine bonifas ndiye aliyekuwa mashine pale kisutu na mahakama kuu etc kuhakikisha kesi zinaenda vizuri. NI JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKINIUMA KWA MUDA MREFU, NASHUKURU NIMELITUA KWA JAMII ILI MZIGO MOYONI MWANGU UTULIWE. kama tunataka wahalifu, mafisadi etc wafungwe na kurudisha mali zetu, ni lazima wale wanawashugulikia tuwapromote na kuonyesha tunawajali. mishahara yao midogo, hata kwenda kuwazika jamani mmeshindwa? kama kuna mtu alihudhuria ule msima atajua ninachoongea hapa.....yule jamaa likuwa na hadhi ya jaji, hata majaji wenyewe akiwa high court akiongea walikuwa wanamsikiliza kwa makini ili wapate vitu toka kwake, ilikuwa mashine kubwa sana, na taifa hili limepoteza mtu muhimu sana ambaye mchango wake kwa jamii haujatambulika hadi sasa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Deleloitte & Touche of South Africa recomended legal action against 12 officials it deemd were implicated in the EPA transactions. He deliberately discarded the ample evidence found by the audit firm and instead diluted the list to only 4 officials. U call that "jembe"? No my learned brother, allow me to differ. In this particular case professionalism was sacrificed at the expense of natural justice.
 
Pole sana ubungoubungo, ukweli inatia huzuni kuona watu muhimu hawatajwi, na hata hawazikwi!!
Hapa najifunza mengi, mojawapo, tunapoteza uzalendo, hatuna vipaumbele na zaidi hatuna waandishi wa habari wenye weredi wa kutosha kwenye tasnia mbalimbali, hivyo habari nyingi hazipatikani accordingly!!

Ndugu unataka mtu ajitangaze nje ya ofisi yake? au atangazwe kwa kazi zake? watu leo tunasoma udaku tu, wangapi wanajua kesi za EPA, DOWANS, etc ( kwa kifupi habari za mahakama, afya, Elimu, etc) zaidi siasa na udaku!!
watu walijaa kwenye kesi ya Mh Lema, mbona kwa kezi za DOWANS, EPA, hawajai????????
Waandishi mpo wapi kutupatia habari?
wakatabau

Ngagarupalu:
Ni kweli kuna Fumba ya magazeti na vyombo vingine vya Habari, kwa bahati mbaya haviendi kwa MAADILI ya kazi zao, Wameweka mbele UDAKU, UBINAFSI na TAMAA na hayo yamekuwa ndio mchango wao MKUU kwa jammi>
 
Deleloitte & Touche of South Africa recomended legal action against 12 officials it deemd were implicated in the EPA transactions. He deliberately discarded the ample evidence found by the audit firm and instead diluted the list to only 4 officials. U call that "jembe"? No my learned brother, allow me to differ. In this particular case professionalism was sacrificed at the expense of natural justice.
sijakuelewa, do you know what the story is all about? and do you know how state attorneys operate their prosecutions and the limits of their duties visa vi that of investigation and arresting policemen?
 
mara nyingi nafikiri watu hufanya wema ili waonwe na wengine wapate sifa, wapate cheo, wapate kura, wafanikiwe kimaisha etc. ni aina moja wapo ya unafiki kutofanya jambo kwa moyo.
 
Back
Top Bottom