Muhimu: Kampeni, Uchaguzi na Matokeo - Je, haya yanawezekana?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
*Kampeni zinaanza tar 22/08/2015.
*Kampeni zinafungwa tar 24/10/2015
*Tar 25/10/2015 Siku ya uchaguzi .
*Tar 26/10/2015 matokeo ya uchaguzi yatatangazwa.
* Kampeni zitafanyika kwa jumla ya siku 70.
* Nchi ina mikoa 30,
* Kuna jumla ya majimbo 240,
* Kuna kata 2,880
* Kuna vijiji 19,800

Hivyo basi, ili mgombea ahutubie nchi nzima, ina maana anatakiwa ahutubie wilaya 3.5 kwa siku, anatakiwa ahutubie Kata 41 kwa siku (kila siku) na pia anatakiwa ahutubie vijiji 282 kwa siku.

Hili limekaaje wadau, linawezekana!?

 
Haiwezekani kumaliza sehemu zote kwa hesabu hizo. Hata hivyo, siyo lazima waende sehemu zote. Miaka yote ya uchaguzi hali imekuwa hivyo!
 
inawezekana kabisa kwani sio lazima aende kila wilaya kwa mfano kule Pemba kuna wilaya nne anaweza kuzifilia zote kwa kuwahutubia watu wote sehemu moja na kwa Ungujua anahitaji siku tatu kwa kuhutubia kila mkoa mara moja and so on
 
Pia ndo maana kuna timu ya kampeni. Kama UKAWA jinsi walivyogawana
 
Ukawa tutafikia kila kijiji, wala hakuna ambaye hatasikia kuwa tulifika na kuwaamsha walio lazwa miaka 54+. Msiogope, hatutishwi na muda sisi tunao muda. Hatulali mpaka kieleweke
 
Mimi nawashauri tu UKAWA wahakikishe kura za urais kwa kila kituo, kata na jimbo wanazipata kabla ya tume ya uchaguzi kutangaza mana tume ya uchaguzi wakishamtangaza tu rais kwa katiba yetu ndo imetoka hvyo ikirudi pancha na tunavyofahamu viongozi wa NEC wamewekwa na raisss ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala
 
Back
Top Bottom