Muhimu: Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA iliyobeba Mtazamo wa UKAWA

Matokeo tarajiwa

• Nchi kupata katiba ya wananchi itakayoharakisha

maendeleo yao na kuwa na Muundo wa Muungano

14

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

unaozingatia haki kwa Tanganyika na Zanzibar

• Wananchi wenye kuwajibika na kuwajibishana katika

shughuli za maendeleo

• Mapato kuongezeka kutokana na kupunguza matumizi

ya serikali na kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma

• Nchi kuwa katika mchakamchaka (mwamko,

matumaini na hamasa mpya katika utendaji wa kazi)

kuelekea maendeleo ya kweli ya kiuchumi, kisiasa,

kijamii na kiutamaduni.
 
ELIMU BORA KWA WATANZANIA WOTE

Hali halisi:

Ili kujenga uchumi imara na kuleta ustawi endelevu wa jamii,

wataalamu ni nguzo thabiti katika kufikia malengo haya. Kwa

miaka zaidi ya hamsini elimu yetu imeshindwa kukidhi mahitaji

ya nguvu kazi katika kuendeleza Taifa letu. Mazingira duni ya

kujifunzia, Uhaba wa walimu na vifaa vya elimu vimekuwa ni

changamoto kubwa.

Shule ya awali

• Elimu ya awali ambayo kwanza inajenga msingi bora na

kumuandaa mtoto kuwa mdadisi, mbunifu na mthubutu

haijapewa kipaumbele.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

Elimu ya msingi:

• Bado watoto hawana madarasa ya uhakika, hawana

madawati kabisa au ya kutosha na shule nyingi zina

uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo.

Sekondari:

• Hakuna maabara, vifaa na wataalamu wa maabara;

hakuna maktaba na vitabu vya kutosha; hakuna walimu

wa kutosha wenye kiwango cha elimu cha kutosha.

Kiwango cha elimu inayotolewa ni duni na haimuandai

vya kutosha mwanafunzi kujiajiri na kuajiriwa.

Vyuo:

• Vyuo vinavyofundisha kuongeza thamani ya malighafi

mbalimbali kama mazao ya kilimo bado havijatiliwa

mkazo. Idadi kubwa ya wanafunzi kuliko miundo mbinu

katika vyuo vikuu, wanafunzi wanaofuzu hawana

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

ujuzi (skills) na hivyo hawana uwezo wa kujiajiri na pia

hawaajiriki kirahisi. Ukosefu wa fedha za kugharamia

kulipia wanafunzi wote waliofaulu.

Maswala mtambuka:

• Walimu wenye ujuzi hasa masomo ya sayansi ni wachache,

waliopo hawathaminiwi, hawapewi mafunzo kazini,

maslahi duni na hakuna nyenzo za kujifunzia za kutosha.

• Ukosefu wa chakula na lishe kwa wanafunzi hasa elimu ya

awali.

• Kutokuwepo na utamaduni wa kujisomea na kuandika.

• Kuna tofauti kubwa katika ubora wa elimu baina ya

matabaka ya kijamii hususani katika ufundishaji, vitabu

vya kiada na ziada, walimu waliobobea, miundombinu na

vifaa vya kujifunzia

Fursa:

Ujenzi mkubwa uliofanyika wa shule za kata na vyuo; pamoja

na shule na vyuo vya sekta binafsi vinaweza kuboreshwa na

kutoa elimu inayokidhi mahitaji ya uchumi na maendeleo ya

Taifa letu.
 
CHADEMA/UKAWA itafanya nini:

• Elimu bora itakayogharamiwa na serikali kuanzia elimu

ya wali mpaka chuo kikuu kwa kila Mtanzania na hivyo

hakuna mtanzania atakayeachwa nyuma.

• Kuanzisha tume au baraza la taifa la Ushauri juu ya elimu

likijumuisha wadau wote

• Kuimarisha elimu ya sekondari, teknolojia, ustadi na ufundi

inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la

ajira.

• Kuimarisha SIDO na vyuo vya ufundi stadi ili kuandaa

vijana kuweza kujiajiri.

• Kubadilisha malengo ya jeshi la kujenga Taifa ili lijikite

katika kutoa mafunzo ya ufundi na uzalendo.

• Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni

pamoja na shule za Kata.

• Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.

• Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.

• Kutengeneza utaratibu kati ya vyuo vya elimu na sekta

binafsi ili vyuo vitekeleze mitaala inayoendana na mahitaji

halisi ya waajiri hususani sekta binafsi.

• Kuboresha afya za wanafunzi kwa kupanua programu ya

lishe mashuleni kama njia ya kuongeza mahudhurio kati

ya wanafunzi na kupunguza utoro.

• Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa waalimu ikiwa ni

pamoja na kuwawezesha kupata nyumba, usafiri na zana

za teknolojia.

• Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

20

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuimarisha elimu ya watu wazima kwa kuwatumia

wanafunzi waliomaliza vyuo ambao hawajaingia kwenye

ajira rasmi kufundisha watu wazima.

• Kuwekeza vya kutosha katika tafiti

• Kujenga utamaduni wa kujisomea, kuandika na kutafakari.

• Kutoa elimu bora ambayo itawawezesha Watanzania

kushindana kimataifa kwa kuzingatia na kusisitiza masomo

ya Sayansi na Tehama.

• Kuanzisha mchakato wa kuona ni jinsi gani Kiswahili

kinaweza kuwa lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya

awali mpaka chuo kikuu.

Matokeo tarajiwa

• Elimu bora itakayomwezesha muhitimu kwa kila hatua

ya elimu kujitegemea na kuchangia kikamilifu katika

maendeleo ya nchi na jamii aliyomo.

• Elimu bora itakayo jenga soko la ajira la ndani na nje kwa

vijana.
 
AFYA NA HIFADHI YA JAMII

Hali halisi:

• Ujenzi wa uchumi imara unategemea sana wananchi

wenye afya njema na pia wenye uhakika na matibabu

pindi kunapokuwa na mahitaji.

• Ujenzi wa miundombinu ya afya lazima uendane na

huduma husika. Baada ya miaka hamsini ya Uhuru,

ujenzi wa miundombinu ya afya, mgawanyo wa

wataalamu na upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa

tiba umejikita katika maeneo machache ya nchi, hasa

mijini. Hali hii imepelekea kutokuwepo kwa uwiano

katika upatikanaji na utoaji wa huduma hizi hapa

Tanzania.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Wananchi wengi bado wanagharamia huduma za

afya kwa kutoa pesa mfukoni pindi wauguapo.

• Kupanda kwa gharama za matibabu.

• Magonjwa ya kuambukiza kama UKIMWI na

kipindupindu kuendelea kuwa tatizo kubwa na

magonjwa yasiyoambukiza kama saratani na sukari

kushika kasi miaka ya karibuni kunazidisha umaskini kwa

mtu mmoja na Serikali kwa ujumla.

• Serikali kushindwa kugharamia huduma za afya kwa

kiwango tarajiwa kutokana na kutenga bajeti isiyokidhi;

na ubadhilifu wa fedha chache zinazotengwa kwenye

ngazi mbalimbali za utoaji huduma.

• Serikali Kushindwa kuendeleza programu mbalimbali

za afya (mfano mradi wa damu salama) baada ya

wafadhili kumaliza muda wao kunadhorotesha zaidi

huduma za afya, kunakopelekea kutokea kwa vifo

visivyokua vya lazima.

• Serikali kupoteza fedha nyingi kwa kugharamia

matibabu nje ya nchi hasa kwa viongozi na watendaji

wa serikali.

Hifadhi ya Jamii

• Kwa sasa wazee na wote wasiojiweza wamepangiwa

kupata huduma za afya bure ili hali upatikanaji wa tiba

na vifaa tiba katika taasisi za umma ni hafifu.

• Wazee na wasiojiweza wamekuwa wakikusanywa

kwenye nyumba za matunzo (makambi) na kupatiwa

huduma zisizokidhi. Makambi haya yamewafanya

wazee kuishi kifungoni na kuwasababishia upweke,

msongo wa mawazo, kusononeka na hata sonona.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuwepo kwa mifuko ya bima na hifadhi ya jamii.

• Kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kwenye sekta ya

afya katika vyuo vikuu na vyuo vya kati kunatoa fursa ya

kupatikana watumishi wengi wa afya.

• Ongezeko la vituo vya afya vinavyoanzishwa na sekta

binafsi, pamoja na taasisi za kidini na zile za kijamii.

• Wazee ni kitovu cha busara cha Taifa wanahitaji matunzo

bora zaidi.

CHADEMA itafanya nini:

• Tutahamasisha idadi zaidi ya Watanzania wajiunge na

bima za afya za malipo nafuu.

• Kuimarisha afya ya msingi pamoja na kinga na kuendeleza

programu mbalimbali za afya baada ya wafadhili

kuondoka.

• Itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki

ikiwa ni pamoja na kusomesa kwa gharama ya serikali

wataalam bobezi (Specialists) katika fani mbalimbali za

afya. Pia wataalamu walio mafunzoni kwa vitendo(kama

vile intern doctors, pharmacists, lab scientist, nurses nk)

wanaohudumia wagonjwa katika vituo vilivyoainishwa

watapatiwa posho za kujikimu ili kuwavutia wataalamu

hawa kubaki katika sekta ya afya na kuhakikisha wananchi

wengi wanapata huduma kwa haraka.

• Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuimarisha miundombinu

ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali za kisasa

na kuboresha mifumo ya rufaa ili kusogeza huduma za

afya karibu na jamii, kuanzisha utalii wa huduma za afya

(medical tourism) na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.

• Kurejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea

kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na mishahara,

nyumba za kuishi na usafiri.

• Kuthibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila

kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile

serikali na hospitali za sekta binafsi/kijamii/kidini.

• Kuboresha huduma za afya kwa kurejea na kutunga

sheria za kusimamia taaluma za afya ikiwa ni pamoja na

kuhakikisha kunakuwepo na mafunzo endelevu katika

taaluma hizo.

• Kuharakisha upatikanaji wa dawa za bei nafuu za

magonjwa sugu kama kisukari na serikali kugharamia

magonjwa hatarishi "terminal illnesses' kama saratani na

UKIMWI.

• Kurejea na kuboresha Taasisi za afya kama MSD, NIMR,

TFDA, NHIF ili ziweze kutoa huduma bora na haraka kwa

wananchi.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuhamasisha na kugharamia tafiti za afya hasa

zinazolenga kuimarisha kinga na kupunguza gharama za

huduma za afya.

• Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu

inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi

kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii

zao. Pia kwa wale wenye matatizo ya macho watapatiwa

miwani bure.

• Kuanzisha nyumba mpya na kuboresha nyumba za

matunzo ambazo zinahudumia wasiojiweza ambao

hawana fursa kuishi na jamii zao.

Matokeo tarajiwa

• Wanachi kupata huduma za afya kupitia bima ya afya

na mifuko ya jamii bila malipo kutoka mfukoni mwao pindi

wauguapo.

• Huduma za afya zitatolewa kwa gharama iliyo rafiki kwa

mtumiaji na kwa ubora zaidi.

• Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaojali afya zao ili

kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambuzwa.

• Kupungua kwa tatizo la rasilimali watu katika sekta ya afya

kupitia ongezeko la vituo vya mafunzo na mafunzo kwa

vitendo.

• Watumishi wa afya kufanya kazi kwa ufanisi na hivyo

kuwawezesha kutoa huduma bora zaidi.

• Wazee na wasiojiweza kuishi na jamii zao wakiwa na uwezo

wa kujikimu ki maisha.
 
ARDHI, MAJI ,KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

Hali halisi:

Ardhi na Makazi:

• Ukiritimba wa umilikishaji ardhi kwa ajili ya makazi

umepelekea migogoro na taabu ya upatikanaji

wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makazi, na hivyo

kusababisha ujenzi holela mijini na vijijini.

• Wakazi wengi hasa mijini wamepoteza mali na gharama

kubwa kutokana na makazi yao kubomolewa bila

kulipwa fidia na hivyo kutupwa kwenye lindi la umaskini.

• Wanachi wengi kukaa katika makazi yasiyo rasmi

ambayo hayajapimwa na kuwekewa miundo mbinu ya

kijamii yanahatarisha maisha ya wakazi wa eneo husika

kama kutokea kwa mioto ambayo inaweza isithibitiwe,

uchelewashaji wa kufikisha wagonjwa mahututi vituo

vya afya n.k.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Maeneo ya hifadhi kama vile maeneo ya mabonde

na ardhi oevu kupimwa kinyemela na mamlaka husika

kumepelekea hali hatarishi kwa wakazi wa maeneo

husika kama vile kutokea kwa mafuriko katika njia za

mifereji au mito yanayosababisha maafa yanayoweza

kuzuilika.

• Kutoboresha na kujenga Miundo mbinu ya maji taka

mipya na kutegemea iliyochoka (iliyojengwa wakati

wa mkoloni) hasa sehemu za mijini kumepelekea sio tu

kutapakaa kwa maji taka yenye vinyesi pia mafuriko ya

mara kwa mara hasa sehemu za mijini.

• Gharama za Vifaa vya ujenzi kuendelea kuwa bei juu

siku hadi siku na hivyo kupelekea ukosefu wa makazi

bora hasa kwa watu wa vijijini.

Maji:

• Tanzania ni nchi pekee barani Africa yenye maji baridi

mengi na ya kutosha ikiwa imezungukwa hifadhi kubwa

ya maji kila upande; hata hivyo wananchi wake hawapati

maji safi na salama. Ni asilimia kumi na tano tu (15%) ya

30

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

Watanzania wanaopata maji safi na salama na wengi

wao wakiwa mijini.

• ukosekana kwa maji safi na salama kunaleta athari nyingi

sana ikiwemo watoto kukosa masomo wakitumia muda

mwingi kutafuta maji, uwepo wa magonjwa ya kuambukiza

hasa yale ya matumbo, ngozi na upofu.

• Kilimo hubaki kuwa cha kutegemea mvua, na shughuli

nyingi hukwama kwa kukosa maji.

• Maji mengi ya mvua yamekuwa yakipotelea baharini bila

mkakati madhubuti wa kuyavuna kwa shughuli mbalimbali

kama kunywa mifugo, na umwagiliaji.

Kilimo na Mifugo:

• Matumizi sahihi ya ardhi huondoa chuki baina ya wakulima

na wafugaji na wakazi na wawekezaji kwa upande

mwingine. Migogoro ya ardhi hupelekea athari kubwa

katika jamii kama vile kuchomeana mashamba na/au

makazi na pia hata mauaji ya kutisha.

• Hakuna sera na mikakati ambayoina nia ya hadhi ya

kufanikisha kilimo cha kisasa chenye tija kwa watanzania.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuvunjika kwa ushirika kumepelekea kukosekana kwa

masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo na mifugo.

• Kukosekana kwa mafunzo endelevu katika kilimo na ufugaji

kumechangia kwa kiasi kikubwa kudolola kwa sekta hizi.

Uvuvi:

Kutokuwepo kwa mafunzo na usimamizi endelevu katika uvuvi

na kukosekana kwa mitaji na mafunzo kumepelekea sekta

hii kutoa mchango usiokidhi mahitaji katika pato la Taifa.

Wananchi kutopatiwa elimu ya kutosha kuhusu uvuvi endelevu

kumepelekea mali na zana zao kuharibiwa kama adhabu ya

kukiuka sheria, mfano ni uchomaji wa nyavu za wavuvi kanda

ya ziwa ambao umechangia umaskini mkubwa katika jamii

husika. Kulegalega kwa uvuvi mkubwa hasa wa bahari kuu na

kukosekana kwa viwanda vya kutengeneza minofu ya samaki

kumepelekea sekta hii kuendelea kudumaa.

32

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

Fursa:

• Kuwepo kwa ardhi ya kutosha yenye utajiri mwingi wa

maliasili.

• Uwepo wa hifadhi kubwa ya maji baridi ya kutosha katika

pande zote za nchi.

• Hazina kubwa ya mifugo na ardhi murua inayofaa kwa

kilimo.

• Uwepo wa vyuo vya uvuvi vyenye miundombinu ambavyo

vikitumiwa vizuri vitasaidia kukuza uchumi wa uvuvi.

• Uwepo wa bahari, mito na maziwa kwa ajili ya uvuvi

endelevu.

CHADEMA itafanya nini:

Ardhi na Makazi:

• Kuimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania

na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na

wafugaji.

• Serikali ya CHADEMA itahakikisha kila kiwanja

kinachopimwa kinakuwa na huduma za maji, umeme na

barabara kabla ya mwananchi kumilikishwa.

• Kama ambavyo ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya

mwaka 2010 vivyo hivyo ilani hii inaendelea kusisitiza kuwa

tutapunguza gharama za vifaa vya ujenzi ziwe na uwiano

sawa kwa nchi nzima ili kila mwananchi ajenge nyumba

bora na salama na kuondokana na nyumba za tembe na

manyasi.

• CHADEMA itapanua miundo mbinu ya maji taka na

kujenga mingine mipya ili kuendana na kasi ya ukuaji wa

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

miji na kupunguza maafa yanatokana na mfuriko pamoja

na magonjwa ambukizi

• Tutahakikisha mapato yatokananyo na ardhi na makazi

hasa ya kibiashara yanachangia kiasi kikubwa katika

pato la Taifa.

Kilimo:

• Kutekeleza kilimo cha kisasa na kukinyanyua kikue kwa

asilimia sita mpaka nane;

• Kuweka sera na mikakati ambayo itainua hadhi ya

kilimo kimapato na kiutendaji ili kilimo kivutie vijana na

Watanzania kwa ujumla na ibadilishe fikra potofu juu ya

kilimo;

• Kuhakikisha kwamba wakulima wanaweza kupata

mikopo ya muda mrefu ya kuanzia miaka 5 hadi 15 na

kuendelea na kwa riba nafuu. Mkakati huu utaimarishwa

na msaada kwa wakulima kuunda SACCOS na VICOBA

kwa ajili ya kukopeshana wenyewe;

• Kutoa elimu na kuwajengea wakulima miundombinu ya

kuendeleza kilimo chao pamoja na miradi ya umwagiliaji

na majasho ya mifugo;

• Kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi

na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka

jembe la mkono;

• Kuwapa wakulima (extension services) maafisa ugani na

ushauri wa kilimo cha biashara ili wazalishe kulingana na

upatikanaji wa masoko;

• Kuhakikisha upatikanaji kwa wakati wa mbegu bora na

pembejeo;

34

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuimarisha na kuongeza vituo vya utafiti katika sekta

ya kilimo na kuvipa fungu la fedha litakalo ziwezesha

kutimiza mahitaji ya shughuli zao. Tutahakikisha kwamba

matokeo na mbegu zinazotokana na vituo vyetu vya

utafiti vinakuwa ‘commercialized;

• Kujenga maghala zaidi kuhifadhi mazao ya wakulima na

tutanua mazao hayo kwa bei ya soko kwa utaratibu wa

kulinda bei za mazao hayo kwa wakulima;

• Kuondoa upigaji marufuku wa kuuza mazao ya wakulima

nje ya nchi ili kuwapa uhuru wa mahali pa kuuza mazao

yao na motisha ya kuzalisha zaidi. Pale inapokuwa lazima

Serikali itanunua mazao hayo kwa fedha taslimu kwa

bei ya soko na ikitokea kukopa wakati wa kulipa italipa

pamoja na riba;

• Ushirika ni nguzo muhimu katika maendeleo ya wakulima

na kilimo kwa kuzingatia hilo tutajikita kwenye kujenga na

kuimarisha vyama vya ushirika na kuvijengea uwezo ya

kutafuta masoko ya mazao yao;

• Kuunda mamlaka itakayokuwa na jukumu la kusimamia

mipango na maendeleo ya sekta ndogo ya mboga

mboga na maua (horticulture and floriculture) kwa

utaratibu wa kuwasaidia na kuwaendeleza wakulima wa

sekta hiyo ili sekta hii ifikie mauzo ya mpaka shilingi trilioni

nne (USD$ 2 billion) katika miaka yetu mitano ya kwanza

ikilinganishwa na kiwango tulichowahi kufikia cha chini ya

shilingi trilioni moja (USD$ 500 million);

• Kusimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi

ya nchi na ya Watanzania.

• Kuanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya

Tanzania hususani mkonge.

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Tutaweka mikakati ya ‘kubrand' mazao ya kilimo ya

Tanzania;

• Kusimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na

kuunganisha sekta hizo na ya viwanda;

Maji:

• Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo

vya maji;

• Kuweka mazingira rafiki yatakayowahakikishia Watanzania

walio wengi wanapata maji safi na salama;

Mifugo na Uvuvi:

• Kufuta kodi zote za mazao na mifugo zisizo na tija kwa

wakulima na wafugaji;

• Kuuza nje ya nchi samaki bora.

• Kuanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.

Matokeo tarajiwa:

• Mwananchi kunufaika na ardhi katika nchi yake na kuishi

katika makazi yaliyo bora yenye hadhi na heshima, na miji

iliyopangiliwa vizuri.

• Wananchi kuwa wamiliki wa adhi yao na kufaidika na

uwekezaji wowote juu na chini ya adhi (Rasilimali zilizopo

ardhini). Matumizi ya adhi yatakuwa kwa ubia na si kwa

fidia.

• Kutokuwa na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na

wafugaji, na pia wawekezaji na wananchi.

• Idadi ya wananchi wanaopata maji safi na salama na

wanaotumia mfumo maji taka kuongezeka.
 
MIUNDOMBINU: RELI, BANDARI, BARABARA,

USAFIRI WA ANGA NA USAFIRI WA MAJINI

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Kuimarika kwa soko la ndani na kupunguza anguko la bei

wakati wa mavuno. Na pia, kuongezeka kwa soko la nje

kwa mazao ya kilimo yaliyo chakatuliwa nchini.

• Wananchi kunufaika na uwekezaji kutoka nje katika kilimo

kwa kuingia mikataba na wawekezaji katika maeneo yao.

• Kuwepo na ongezeko wa viwanda vidogovidogo na vya

kati vya kusindika na kuhifadhi matunda na mboga mboga;

viwanda vikubwa vya kuchakata mazao mbalimbali ya

kilimo, uvuvi na mifugo.

Hali halisi:

Bandari na barabara:

• Ujenzi wa miundombinu ya bandari na barabara

umekuwa ukiendelea katika sehemu mbalimbali nchini.

Bandari za Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar na Mtwara

zimekuwa zikifanyiwa matengenezo mara kwa mara

ili kuleta tija. Ki nadharia bandari hizi zingekuwa nguzo

mojawapo kubwa ya uchumi wa Tanzania.

• Sekta ya bandari imeghubikwa na rushwa pamoja na

utendaji mbovu kiasi kwamba mrundikano wa mizigo

umekuwa mkubwa sana bandarini na kupelekea

mapato yake kuwa madogo kulinganisha na fursa za

usafirishaji mizigo zilizopo.

37

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Barabara zimejengwa kwa kiwango cha chini kiasi

kwamba hubomoka katika muda mfupi na kuwa ni

chanzo cha ajali za barabarani.

Miundombinu ya Reli:

Serikali ya CCM imeamua kutelekeza mtandao wa reli na

kujikita zaidi kwenye usafirishaji wa mizigo nchi kavu kwa

kutumia njia ya barabara. Hali hii imeongeza gharama za

usafirishaji, uharibifu wa barabara na kusababisha kutokea

kwa ajali mbaya mara kwa mara na kudumaza uchumi wa

nchi.



38

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

Usafiri wa Anga:

Shirika la ndege la Tanzania lilikuwa ni shirika lenye ufanisi

mkubwa katika usafiri wa anga barani Afrika. Hata hivyo shirika

hili kwa sasa lina chechemea likiwa na watumishi wengi na

likitegemea Hazina kulipa mishahara.

Usafiri wa Majini:

Usafiri wa majini umekuwa ni tatizo sugu ambalo linahitaji

mkakati wa haraka katika maeneo yote yanayohitaji usafiri

huo hasa maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Katika

maziwa haya Vivuko ni vya kizamani na havitoshi na meli

zilizopo ni mbovu sana. Hii inapelekea wananchi kutegemea

mitumbwi na njia zingine mbadala ambazo ni hatari kwa

maisha yao na pia wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi

kama usafirishaji wa bidhaa.

Fursa:

• Ujirani na nchi nyingi zisizo na bandari, kunatoa fursa kwa

Tanzania kujenga uchumi wa bandari na usafirishaji.

39

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

• Uwepo wa malighafi nyingi za mazao ya kilimo na mifugo

zinatoa fursa ya kukuza miundombinu ya usafirishaji.

• Tanzania kuwa nchi mwanachama wa jumuiya mbalimbali

za kimataifa, hivyo kuongezeka kwa huduma ya usafirishaji.

• Kuwa na fukwe za bahari na maziwa yenye mandhari

inayohitajika kujenga bandari.

• Kuwa na akiba (deposit) ya kiasi kikubwa cha chuma na

fursa ya kuzalisha kiasi kikubwa cha nishati nyingi na ya bei

nafuu

• Kuwepo na wasafiri wengi wa ndani na nje kunatoa fursa

ya kuwekeza katika usafiri wa anga.

CHADEMA itafanya nini:

• Kujenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa viwango vya

kisasa kwa kuzingatia maslahi ya nchi . Hii ni pamoja na

kujenga uwezo wa kuzalisha mataluma ya reli nchini.

• Kuboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega

uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa

bandari za nchi jirani.

• Kujenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile

za vijijini.

• Kujenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa

misingi ya faida.

• Kujenga miundombinu ya kisasa ili kuondoa misongamano

ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza,

40

Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015

Mbeya, Arusha na miji mingine inayokuwa kwa kasi nchini.

• Kuimarisha usafiri wa majini kwa kuboresha na kuweka

miundo mbinu mipya.

Matokeo tarajiwa:

• Bandari kuwa njia kuu ya uchumi kwa kuhudumia kilimo na

viwanda. Na pia, kuchangia zaidi ya theluthi moja ya pato

la Taifa.

• Shirika la ndege la Taifa (Air Tanzania) kuimarishwa ili kutoa

huduma nchini na nje ya nchi huku likijiendesha kibiashara

zaidi na kwa fiada.

• Wananchi hasa wa visiwani kupata huduma muhimu za

kiuchumi na kijamii.

• Mizigo yote mizito kusafirishwa kwa njia ya reli na meli ili

kupunguza gharama na kuongeza tija katika uzalishaji.

Kupunguza ajali na kulinda miundo mbinu.

• Barabara zinazodumu na zilizo salama zaidi kwa watumiaji.
 
Hicho kipengele cha kukuza na kuendeleza uchumi wa soko huru lisilokuwa holela ni muhimu sana. Haya ni MABADILIKO. Sera za soko holela (neoliberalism) ambazo ndio zimekuwa zinakumbatiwa kichwa kichwa na serikali za CCM tangu utawala wa Mwinyi ni majanga na ndio zimeifikisha nchi hapa ilipo. Msingi wa hizi sera ambazo zilipigiwa sana chapuo na Reagan & Thatcher katika miaka ya 1980 ni kuhakikisha wawekezaji (kwa hapa kwetu wengi ni kutoka nje) wanapata faida kubwa iwezekanavyo bila kujali maslahi mapana ya taifa na ustawi wa jamii. Chini ya hizi sera dhana ya wote kunufaika (public good) na rasilimali za nchi haipo; ni kila mtu na lwake na serikali inageuzwa kuwa ni wakala tu wa makampuni makubwa ya kigeni (multinationals). Ndio maana serikali ya CCM imejiweka pembeni katika kushughulikia matatizo ya kimsingi ya wananchi. Kila mtu anatakiwa atafute ufumbuzi kivyake wa matatizo ya afya, elimu bora, ajira na hifadhi ya jamii na akishindwa anaitwa "LOFA na MPUMBAVU" na pia anaambiwa ana "UVIVU WA KUFIKIRI".
 
Kutoka FB:

" Slaa alinishangaza...kabla hajasafiri alisema mwenyewe kuwa kinywa chakekuwa Ilani ya CHADEMA ambayo Mh.Lowassa anainadi leo, iliandaliwa kabla Mh.Lowassa hajaingia CHADEMA na yeye Slaa alishiriki vyema kuiandaa (akitegemea kuja kupeperusha bendera ya CHADEMA).
Baada ya kurudi safari ..anasema Ilani ya CHADEMA haizungumzii ufisadi..!!! Duh huyu Daktari vipi..mbona anajikologa...!!??

Hii imenibidi niperuzi tena Ilani ya CHADEMA..na nikakutana na hichi kipengelee...

Nukuu......

" UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
TUTAPIGA VITA RUSHWA/UFISADI NA UBADHIRIFU katika sekta ya Umma na binafsi
Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia "
.....Mwisho wa kunukuu.
Hivi ina maana Daktari mara hii kasahaua Ilani aliyoandika mwenyewe ??


KWELI UTUMWA WA PESA UNALETA OPOFU WA FIKRA.
R.I.P FIKRA ZA DAKTARI.
VIVA MABADILIKO.

ilani.jpg
 
Ukishakula pesa za watu lazima uwatumikie tu, Huyo Dr mihogo anazidi kujidhalilisha kila uchao
 
Dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi inatoka kwenye nafsi ya mtu. Kitendo cha CHADEMA kumsimamisha fisadi kuwa mgombea Urais mmejiondoa kwenye kundi la vyama vinavyopambana na ufisadi. Ijapokuwa kwenye ilani yenumkuna mstari mmoja unaoeleza ufisadi, mgombea wenu hajawahi hata siku moja kunadi ilani hiyo
 
Chadema haikuwa na ilani,ilichofanya ni kucopy na kupaste ilani ya ACT
 
Mkitaka tuwaelewe andikeni hivi : hatutafungama kabisa na watuhumiwa wa ufisadi siku zote za uhai wa chadema kwani tuhuma hufuata wanaofanana nayo. Haya karekebishe upesi kisha uje
 
Wana ukawa jaman mwenye kuijua ile webusait yetu,tafadhal aiweka hapa ili tuperuzperuz kusoma ilan ya chama pamoja na mikakati!Maana kwenye mikutano ya mhe hakuna anachoeleza,tafadhal pliiiz
 
Hahahahahahah!hata nami nina hamu sana ya kuisoma,tokea ile siku aliposubiriwakwa masaa 12 alaf akasem hotuba tukaisomee
 
Wana ukawa jaman mwenye kuijua ile webusait yetu,tafadhal aiweka hapa ili tuperuzperuz kusoma ilan ya chama pamoja na mikakati!Maana kwenye mikutano ya mhe hakuna anachoeleza,tafadhal pliiiz

Wensite imetolewa, mzee nae haongei
 
Back
Top Bottom