singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
.............Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.
..........................
ndio wamethubutu wameweza je hiyo cath lab itamsaidia vip mwananchi wa kawaida? tunaona ni watanzania wangapi wenye hali za chini wanaoweza kumudu gharama za muhimbili? unadhani wote waliopo mwananyamala wanapenda kwenda kulundikana pale? ni pongezi kwa kuweza kufanikisha hilo ila usibeze upinzani kwa kuwa hilo bado halina manufaa ya moja kwa moja kwa watu wa kipato cha chini.
Naona kichwa cha habari na habari haviendani, Wapinzani ndio waliokuwa wanapiga kelele viongozi kwenda kutibiwa nje, madaktari kupiga dili kupitia tiba za nje, iweje leo wabeze,Siku ukiugua utajua umuhimu wake
ni wangapi wanashidwa kuhudumiwa muhimbili kwasababu hawana hela? kama hujjashuhudia mtu anarudishwa hom kisa hawezi kuaford cost za muhimbili sio mbaya ila kwa wale walioexperience hata kwa kuona tuu kwa jirani wanaelewa unachomaanishaSiku ukiugua utajua umuhimu wake
Aisee Wapinzani wamebeza nini sasa. Ungeelezea vizuri. Hilo ni jambo jema japo limechelewa sana kufikia nchi yetu. Ila vipi tathmini ya hali ya huduma za afya kwa Tanzania nzima? Maana naona serikali imefanikiwa sana kupandisha hadhi hospitali na sio kuongezea ufanisi majengo, vifaa tiba ni vile vile kasoro majina tu. Muhimbili bado sana katika moyo. Wataalam wachache mnoo. Ila tutafika kaka..
Naona kichwa cha habari na habari haviendani, Wapinzani ndio waliokuwa wanapiga kelele viongozi kwenda kutibiwa nje, madaktari kupiga dili kupitia tiba za nje, iweje leo wabeze,
ni wangapi wanashidwa kuhudumiwa muhimbili kwasababu hawana hela? kama hujjashuhudia mtu anarudishwa hom kisa hawezi kuaford cost za muhimbili sio mbaya ila kwa wale walioexperience hata kwa kuona tuu kwa jirani wanaelewa unachomaanisha
umemaliza kila kitu , mimi naondoka kabisa , mtu kukamuliwa jipu kwa ufanisi basi anaona miuuujiiiiiza !Haya waambie wale wananchi wa Lupeta, Mpwapwa(Dodoma) wanaotibiwa chini ya mti walioonyeshwa na ITV habari jana.
nani kakudanganya kwamba ccm ina hela za kuboresha chochote nchi hii ?Ha ha ha ha kwani Wapinzani ndo wamekarabati,kujenga na kuboresha hali hiyo au ni serikali ya CCM ndo imefanya vitu vyake?
Mkuu ni majanga, yahani taifa lenyeTakataka! Miaka 54 ya uhuru leo ndo haya yanatangazwa! Tena unatibu kwa kusaidiwa na wayahudi! Niliyeko mtwara nije Dar es salaam kupanga foleni ya tiba?
Mwaka 2005 Dr Masau alipotangaza haya, mbona tuliona hao hao wanafiki wa Muhimbili wakijitokeza na kusema ni kinyume cha maadili kujitangaza? Leo hii unaleta tangazo lile lile ili iweje?
Walioanza ni THI Tanzania Heart Institute ya marehemu Masau.
Kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.
Kwamba wagonjwa wenye matatizo hayo ya moyo, wataweza sasa kuzibuliwa matundu hayo kwenye moyo bila kufanyiwa upasuaji kifuani. Hii, kwa hakika ni habari njema, tena yenye kustahili kupongezwa.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mafanikio haya, ni kwamba kufungwa kwa mtambo maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili, "Cath Lab" ndiko kutafanikisha huduma hizo muhimu katika maisha ya binadamu.
Kwa ufafanuzi tu ni kwamba, Cath Lab ni mtambo maalumu unaotumika kufanya uchunguzi, kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kuziba matundu ya moyo bila kufanya upasuaji.
Kwa kuzingatia ukubwa wa magonjwa ya moyo nchini na gharama ambayo serikali na hata watu au taasisi binafsi zimekuwa zikiingia kusafirisha wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa tiba za aina hii nje ya nchi, hakika, kwa kiasi kikubwa hatua hii itasaidia kuipa sura mpya sekta ya afya hapa nchini.
Tunajivunia wataalamu wetu nchini ambao tayari wameutumia mtambo huu kwa ufanisi mkubwa, kupitia Kitengo cha Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakifanikiwa kufanya tiba ya moyo kwa kuziba matundu ya kwenye moyo bila kufanya upasuaji wa kifua.
Lakini si tu wataalamu wetu hapa nchini bali hata wenzao kutoka nje ya nchi ambao, kwa pamoja, wamefanikisha tiba hiyo, hao ni pamoja na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.
Tunaungana na Watanzania wengi katika kuamini kwamba hi ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya tiba na afya nchini baada ya kushuhudia ushirikiano wa aina hii na hospitali nyingine kadhaa za kimataifa kwa kutumia mifumo ya habari kama Video Conference ambayo huwawezesha madaktari kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao walioko nje ya nchi.