Muhimbili vs Agha Khan

Muhimbili vs Agha Khan

Muhwelo

Senior Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
136
Reaction score
32
Ndugu wanajukwaa, Waswahili husema kwamba Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kumbe ni kweli! Sikuwahi kujua kuwa Hospitali ya Agha Khan ni bora kuliko ile ya Taifa, Muhimbili. Kitendo cha kumhamisha DCI Manumba kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenda Agha Khan kimenifanya niamini kuwa hali ya Muhimbili kihuduma ni mbaya sana. Madaktari walipogoma miezi michache iliyopita, moja ya madai yao ilikuwa ni kudai mazingira bora ya kazi kama vile kuwa na vifaatiba vya kisasa. Reaction ya serikali ilikuwa ni kupuuza madai yao. Je, kwa nini serikali haitaki kuboresha huduma za afya nchini? Kwa uelewa wangu, napata majibu haya: kukosekana kwa uzalendo miongoni mwa viongozi wetu, kuwepo kwa ufisadi, na kwamba hospitali zetu ni kwa ajili ya walalahoi kama mimi, kwa sababu wao wana uwezo wa kwenda kutibiwa katika hospitali kama Agha Khan na nchi za nje. Au taifa letu ni maskini kama wanavyosema wao? Kama ni kweli, mbona tuna rasilimali lukuki nchini? Iweje Hospitali ya Agha Khan (hospitali binafsi) iwe na huduma bora kuliko ile ya Taifa inayomilikiwa na serikali? Ipi iliyo na nguvu, taasisi binafsi au serikali? Kama taasisi ina nguvu kuliko serikali, hivi Watanzania tunaweza kujivuna kuwa tuna serikali makini? Naomba majibu yenu, siasa tuweke pembeni! Waingereza husema, 'One finger can not crush a louse'. Katika nchi yetu, mambo ni kinyume kabisa. Serikali inakusanya kodi nyingi sana, lakini hali si shwari kabisa. Tafadhali, naomba mawazo yenu!
 
Mbona Zito Kabwe alihamishwa kutoka Aga Khan kwenda MUHIMBILI ? Kibaya zaidi alikuwa na malaria ambayo haikuonekana huko ikaja inekana na wataalam wa MUHIMBILI. Cha msingi hapa ni huduma gani ipo mahali fulani ambayo haipatikani sehemu ambapo mgonjwa amelazwa.
 
sijui ni lini viongozi wetu watakuwa na uzalendo wa kutetea uhai wa watanzania wengi ambao hawanapakukimbilia isipokuwa hospitali ya serikali. naamini pesa zipo ya kuifanya muimbili kuwa ya kisasa zaidi kwasababu hii nchi sio maskini. SHIDA YA TANZANIA NI KWAMBA VIONGOZI WETU WAKATI WA CAMPAIGN WAPOLE SANA ILA BAADA YA UCHAGUZI utasikia ya pinda liwalo na liwe utazania nchi ni ya baba yake!
 
Mbona Zito Kabwe alihamishwa kutoka Aga Khan kwenda MUHIMBILI ? Kibaya zaidi alikuwa na malaria ambayo haikuonekana huko ikaja inekana na wataalam wa MUHIMBILI. Cha msingi hapa ni huduma gani ipo mahali fulani ambayo haipatikani sehemu ambapo mgonjwa amelazwa.

hapo mkuu kuna kitu . inawezekana AGA KHAN HOSPITAL IKAWA MAJENGO TUU LAKINI NDANI HAMNA KITU!!
 
Hayo ya DCI kuna behind the scene,mbona pale Agha karn weupe tu,wahindi wanajua nin ndugu yangu zaidi ya biashara tu,tuchunguze tutajua what behind the scene kuhusu hilo DCI.
 
kauli yake imekatika leo
sijakuelewa hatunaye au? ok turudi kwa mada hivi mimi niliwachapa virungu wkt wa kudai haki za msingi leo hii nije mnitibu dhubutuuu nani aje mummalizie? maneno yangu tu hayo!
 
sijakuelewa hatunaye au? ok turudi kwa mada hivi mimi niliwachapa virungu wkt wa kudai haki za msingi leo hii nije mnitibu dhubutuuu nani aje mummalizie? maneno yangu tu hayo!

yupo ICU bado roho haijatoka ila kauli ndio imekatika kwa ujibu wa magazeti na vyombo vingine vya habari.
 
hapo mkuu kuna kitu . inawezekana AGA KHAN HOSPITAL IKAWA MAJENGO TUU LAKINI NDANI HAMNA KITU!!

mkuu sikia. Kwanza kuna kitu wanakificha kuhusu ugonjwa wake hata kama ni siri yake na daktari akiwa mnh habari zitaleak tu na kuja mtaani. Hivyo wameamua kumhamishia kwa wahindi ambako vitisho vya kufukuza kazi watakaotoa taarifa ni kubwa. Pili kumbuka huyu ndo muhusika wa uchunguzi wa makosa ya jinai. Hawa ndio waliotaka kumuua dr ulimboka ila Mungu wake akamuokoa. Kitendo kile kiliwaumiza madaktari mpaka leo wengine bado wana kinyongo na viongozi wa serikali. Kitendo kile kiliwahukumu hata wao ndo maana wanajishuku kila wanapoenda hospitali. Tatu icu ya mnh iko kama bwalo hivyo mtu yeyote atakayeingia anaona kila kitu(wameshindwa kuimodernize). Viongozi wetu huwa wanajiona wako tofauti kabisa na sisi hivyo hawataki muwe mnapata huduma sawa, ndo maana wakamuondoa mnh na kumpeleka agha khan japo wanaomhudumia wanatoka mnh. Hili pia hutokea wilayani ambako wakuu wa wilaya wanalazimisha daktari amfuate nyumbani kwake kwa kuona kinyaa kulala kitanda anacholalia na maskini. Hii nchi chini ya maccm ni ngumu sana
 
Hayo ya DCI kuna behind the scene,mbona pale Agha karn weupe tu,wahindi wanajua nin ndugu yangu zaidi ya biashara tu,tuchunguze tutajua what behind the scene kuhusu hilo DCI.
Basi watanzania tuwe tunaongea vitu kwa kujua tusemayo!Unawezaje kuwaponda eti wahindi wanajua nini?Pengine nakushangaa wewe huenda hata shule hujaenda ndo maana hujui mchango wa hawa jamaa kwenye fani hasa ya medicine!Jiulize tu kwa nini viongozi wengi hupelekwa Apolo kama kweli wahindi wana nini?
 
Huyu mtu inaonekana amepishana na shule japo anajitahidi kuponda. Hata bila kwenda kutibiwa nje maktaba nyingi kubwa haziwezi kukosa vitabu vilivyoandikwa na wahindi. Wahindi wamebobea kila fani siyo kama sisi tuliobobea katika porojo.
 
we inawezekana haupo medical field tuliokwenye hii field ndo tunajua we tulia.
 
Huyu mtu inaonekana amepishana na shule japo anajitahidi kuponda. Hata bila kwenda kutibiwa nje maktaba nyingi kubwa haziwezi kukosa vitabu vilivyoandikwa na wahindi. Wahindi wamebobea kila fani siyo kama sisi tuliobobea katika porojo.

usilolijua ni sawa na usiku wa giza,unajua nin ndugu every thing is about exposure,hawa jamaa ni exposure walioipata at the begining of this field kawa huamini watoto wako wa expose stand alafu uone watakua wakina nani,nawajua sana walivyo mashuhuri kwa hii field but nowdays they are much after money.
 
Mbona Zito Kabwe alihamishwa kutoka Aga Khan kwenda MUHIMBILI ? Kibaya zaidi alikuwa na malaria ambayo haikuonekana huko ikaja inekana na wataalam wa MUHIMBILI. Cha msingi hapa ni huduma gani ipo mahali fulani ambayo haipatikani sehemu ambapo mgonjwa amelazwa.

Kwahiyo kuna huduma ilikosekana MNH sio? What a shame!
 
Mbona Zito Kabwe alihamishwa kutoka Aga Khan kwenda MUHIMBILI ? Kibaya zaidi alikuwa na malaria ambayo haikuonekana huko ikaja inekana na wataalam wa MUHIMBILI. Cha msingi hapa ni huduma gani ipo mahali fulani ambayo haipatikani sehemu ambapo mgonjwa amelazwa.

Je, Zitto alitibiwa Muhimbili?
 
Muhimhili ni muhimbilu na Aghkhan ni Aghakan cha msingi ni matibabu Get well soon Afande Manumba
 
Back
Top Bottom