Muhimbili 'kwachafuka'

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
07 FEBRUARY 2012



*Madaktari bingwa nao wagoma, huduma zasimama
*JWTZ wakosa ushirikiano, wauguzi wabaki wapweke
*Wagonjwa: Nasi tutaandamana tukafie wizarani getini

Grace Ndossa na Goodluck Hongo

MGOMO wa madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana ulichukua sura mpya baada ya madaktari bingwa waliokuwa wakiendelea na kazi, kuanza mgomo rasmi ili kuishinikiza Serikali isikilize madai yao haraka.

Leo ni siku ya tatu tangu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, ianze kusikiliza madai ya madaktari waliogoma kurudi kazini na kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro uliopo kati yao na Serikali.

Uamuzi wa madaktari bingwa kufanya mgomo huo, ulifikiwa katika kikao cha pamoja ambacho kilifanyika hospitalini hapo na kuanza mgomo rasmi saa nne asubuhi.

Akizungumza kwa niaba ya madaktari hao, Dkt.Catherine Mg'ong'o, ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya madaktari bingwa watano waliochaguliwa wiki iliyopita kwenda kuonana na Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda, alisema hawatafanya kazi hadi Serikali itakaposikiliza madai yao.

"Mgomo umeanza rasmi leo (jana), hatutafanya kazi hadi madai yetu yatakaposikilizwa, huduma zitasimama hadi tupate haki yetu kwani Serikali inafanya mzaha," alisema.

Kutokana na azimio hilo, baadhi ya madaktari hao walionekana wakiingia katika magari yao na kuondoka huku wagonjwa wakiwa wameshika tama.

Mgomo huo ulisababisha hali ya matibabu hospitalini hapo kudorora na kuwaacha madaktari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wasijue la kufanya.

"Kimsingi madaktari bingwa wametupa ushirikiano mkubwa sasa kutokana na mgomo huu, hatujui nini cha kufanya," alisikika akisema mmoja wa madaktari wa JWTZ.

Wauguzi nao walisimama katika vikundi wakijadili mgomo huo nyuso zao zikionekana zenye huzuni. Katika wodi mbalimbali, wagonjwa walikuwa wakilalamika huku baadhi yao wakisema ni bora waandamane hadi katika Ofisi za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wakafikishe kilio chao.


"Umefika wakati na sisi tunapaswa kuandamana, ni bora tufie mbele ya jengo la Wizara ijulikane moja kwani umaskini wetu ndiyo unaotutesa," alisema mgonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Ally Abdallah anayesumbuliwa na maradhi ya moyo.

Katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), huduma zilisimama kabisa huku wagonjwa wakiambiwa hakuna matibabu yanayotolewa.

Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, jana iliendelea na vikao vyake jijini Dar es Salaam ikizungumza na wadau mbalimbali kwa lengo la kutafuta suluhu ya madaktari waliogoma.

Wakati hayo yakiendelea, Serikali imeshauriwa kuorodhesha majina ya madaktari wote walioshiriki katika mgomo, kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwafutia leseni zao.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo (Mzee wa Upako), aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Hawa madaktari wanajiona wao ni zaidi ya wengine, wanasahau kuwa watumishi wote wanategemeana katika kazi zao, Muhimbili hali ni mbaya sana, madaktari wamekuwa wakatili zaidi ya wale wanaoua albino (walemavu wa ngozi) kwa kukataa kutoa huduma," alisema Mchungaji Lusekelo.

Aliipongeza Serikali kwa kutaka suluhu na madaktari hao na kuongeza kuwa kiburi hicho, ndicho kimewafanya wakatae kwenda kuzungumza na Bw.Pinda.

Alisema katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), madaktari wanalipwa dola 10, lakini wanafanya kazi kwa uzalendo mkubwa na kuongeza kuwa inawezekana Serikali ina makosa lakini pamoja na kutaka suluhu, madaktari walikataa.



 
Hii hapa ndipo itaonyesha jinsi Serikali ya CCM kama itaweza kushughulikia migomo dhidi yake

Kama haitaweza waangalie nchi nyingine... they resigned the post na kuwaachia wengine wenye akili kujaribu kujadilianan na hao wanaanchi

Viongozi wa CCM hawakuchagulikwa kwa Maisha...
 
Hii hapa ndipo itaonyesha jinsi Serikali ya CCM kama itaweza kushughulikia migomo dhidi yake

Kama haitaweza waangalie nchi nyingine... they resigned the post na kuwaachia wengine wenye akili kujaribu kujadilianan na hao wanaanchi

Viongozi wa CCM hawakuchagulikwa kwa Maisha...

Ndo umeamka ukaanza kusoma magazeti ya net?
 
Ndo umeamka ukaanza kusoma magazeti ya net?

So, Kupeng'e... kama ulikuwa unajua hii issue kwanini usingeweka tuijadili? Mimi siishi bongo kwahiyo sipati habari kama wewe, kwahiyo pia acho unyambwele wa kujifanya unayajua yooote; hayo ndio matatizo ya sisi Watanzania kujifanya tunajua Mengi...
 
Back
Top Bottom