Muhimbili health check dept.

sakilo

Member
Oct 13, 2012
5
0
Ndugu wan JF nilisoma hapa mtandaoni kuhusu kuanzishwa kwa idara hiyo pale muhimbili nikavutiwa sana.Nilienda pale jana tar 30 kuulizia nikaambiwa ipo na inafanyika siku ya jmosi tu.

Baada ya kupata packages zao amabazo ni sh 188000 kwa wanaume na 193000 Kwa wanawake.Leo asubuhi saa mbili nimefika hapa kwa kufanya check up nikapokelewa nikalipia sh 188000 pamoka na extra 35000 kwa ajili ya abdomen ultrasound ambayo haiko kwenye package.

Sasa cha ajabu nilipewa nurse wa kunizungusha sehemu zote za vipimo na sehemu pekee niliyokuta mhudumu ni maabara na xray ambapo nilichukuliwa vipimo.

Idara ya moyo hakuna mtu na cha ajabu wanadai hawana taarifa za hiyo idara ya health check.kwenye Ultrasound vilevile hakuna mtu na hawajui lolote kuhusu health check.

Nimeulizia kurudishiwa hela naambiwa haiwezekani. Sister wa health check dept amempigia Dr mmoja aitwaye Mwinyi amekubali kuja kunifanyia ultrasound ila anatoka nyumbani kwake kunisaidia tu.ECG nimeambiwa hadi jtatu.Majibu ya maabara nimeambiwa mashine inasumbua siwezi kupata majibu ya HIV wala PSA na na HDL sasa hivi ni saa 8.10 toka asbh niko hapa na ni mgonjwa mmoja tu niliyekuja leo.

Swali je tungekuwa kumi Ingekuwaje? Je toka saa 2 hadi sasa nafanya nini hapa? Majibu yenyewe siku tatu na nimelipa hela zote hizo nikijua ni huduma ya haraka.Kwa nini waanzishe wakati hawajajipanga?
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,565
2,000
Hao ni matapeli umekutana nayo.kwani hakuna private wanaoweza kukufanyia health checking hadi ukaenda hapo muhi2?.
 

wakubaha

Member
Nov 17, 2008
99
70
Pole ndugu na tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni katika taasisi za serikali ambapo unalipia huduma lakini unaonekana kama umeenda kuomba msaada...na hata taarifa zao nyingi si za ukweli na njoo kesho nyiiiingi inakatisha tamaa sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom