Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Muheshimiwa sana Nape Nauye hii ni shule ya Msingi Litingi iliyopo kijiji cha Litingi kata ya Nyangao Jimbo lako la Mtama.
Hali ya shule hii ni mbaya mno, watoto wanakalia mabenchi na haina milango, wala ubao wa kufundishia, wala vyoo .
Walimu na wanafunzi wanajisaidia porini, wananchi wako wanakuomba sana Muheshimiwa uisaidie shule yao hii angalau ipate vyoo tu.
Mvua sasa zinanyesha, kuna hatari ya kulipuka ugonjwa wa kipindu pindu.
Juzi wananchi wako wamepata habari namna ulivyotoa Tshs Millioni 3 kwenye tamasha moja la muziki kununua album moja tu, hawakuzuii kutoa maana ni utashi wako, lakini muheshimiwa Wapiga kura wako hawa wanakuomba sana uelekeze huo moyo wako wa utoaji na huku kwao.
Wapiga kura wako wanahitaji Tshs Millioni 2 tu kukarabati kashule kao haka, wasukumesukume siku msimu huu wa mvua upite. Tshs millioni 1 wataitumia kununua mabati mapya 50 waezeke na shilingi millioni 1 nyingine wataitumia kuzibaziba milango na madirisha watoto wasinyeshewe mvua, na kununua ubao mpya wa kuegesha chini ili watoto wasome maana ule uliopo umeliwa na mchwa.
Mmoja wa wananchi wako amenituma nikuambie haya maana jimboni juzi uliahidi kwenda, lakini ghafla ukapotea ila wanasema wakakusikia uko kwenye matamasha mazito huko Darisalama.