Muhenga aliyesema Mwanamke tabia yuko wapi??

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,883
Si umewahi kusikia falsafa ya Wahenga kwamba, ‘Uzuri wa mwanamke ni tabia, sio urembo?’ Basi nakushauri ishia kuisikia hivyo hivyo, usije ukaamini, na zaidi ukataka ifanye kazi katika enzi hizi... utakufa kabla ya muda wako kwa mfadhaiko wa moyo.


Ninachojaribu kukwambia ni kwamba, kama bado hujaoa, hakikisha haujisumu kuoa mwanamke ambaye hakuvutii kwa chochote unapomtazama kwa jicho la kawaida la kiume, mwanamke ambaye ulipoanza kumuona siku za mwanzo, wala hukuwa unashikwa na matamanio naye.

Nakwambia achana na huyo mwanamke hata kama ana tabia za malaika, hakuumbwa kwa ajili yako.

Simaanishi Wahenga waliposema mwanamke tabia walikuwa wanatupotosha, hapana. Tabia ni moja ya nguzo muhimu tena ukiwa na mke mwenye tabia safi unapunguza hata uwezekano wa kupata presha za ajabu ajabu, lakini chunga hiyo isiwe sababu ya kukutoa ufahamu na kujifanya huelewi raha ya kuwa na mke mzuri kwa muonekano au mke mrembo.

Na kabla hatujafika mbali tuelewane kitu kimoja, tunaposema mwanamke mzuri hatumaanishi mwanamke anayenyongorota shingo ya kila mwanamume anapokatiza njiani, hapana.

Tunazungumzia mwanamke ambaye wewe binafsi ukimuona unasikia faraja tu mpaka unahisi ‘kamoyo kanakuwa na ubaridi fulani hivi— huyo ndo mwanamke mrembo.


Sasa ukioa mwanamke ambaye havutii jicho lako utakufa kwa mfadhaiko wa moyo kwa sababu siku hizi bwana kuna mitoko lukuki inayokulazimu kwenda na mkeo. Kuna harusi za rafiki zako uliosoma nao, send off za watoto wa mama mkubwa, sherehe za kiofisi zinazoruhusu kwenda na mama watoto na mitoko mingine mingi. Niamini mimi, umuhimu wa kuoa mwanamke mzuri utaugundua unapokwenda kwenye hii mitoko.


Hujawahi kukutana na mtu anamtambulisha mke wake kwa kutumia majina ya watoto wao nyumbani? Unasikia, ‘Huyu ndo mama John. Ushawahi kukutana na mtu wa aina hiyo? Basi huyo ni miongoni mwa waliojisumu wakaoa wanawake ambao hawawavutii kwa mwonekano, walioa tabia, sasa baadaye ndiyo anagutuka, anagundua kuwa kumbe kuoa mwanamke anayekuvutia kunakupa uhuru na amani na kukufanya ufurahie popote unapokuwa naye.

Wahenga wa kidigitali wanakwambia kuoa mwanamke ambaye hakuvutii machoni ni sawa na kuvaa nguo ya kawaida lakini ya gharama kubwa sana, hakuna mtu atayekujua thamani ya nguo yako, itathaminishwa kwa mwonekano tu na kwa sababu hata mwenyewe huamini kwamba ni nguo nzuri, ndo unajikuta muda wote unaongelea fedha nyingi zilizokutoka kuinunua.


Wanaume waliooa wanawake wa hivi wanaelewa nazungumzia nini, wanajua jinsi inavyolazimu kuishi na moyo wa chuma unaovumilia maumivu yanayokuja kila wakati hasa linapotokea suala la kutambulisha— kwa hiyo fanya juu chini hakikisha huwi miongoni mwao.
Ukiendelea kuishi kwa kusikiliza kila wanalolisema Wahenga, utaumia. Hii ni karne ya 21 aisee.

Gentleman.
 
Mapenzi tu ndio kila kitu. Uzuri na tabia ni subjective. Ona TI yuko radhi kupigana na Floyd kwa ajili tu ya Tiny.

maxresdefault.jpg
 
Kwenye suala la ndoa mambo yote yanategemeana yaani uzuri pamoja na tabia ya mwanamke,

Unaweza kuoa mwanamke mzuri mithili ya malaika lakini anagawa kama njugu lazima mgawane majengo ya serikali mmoja monchwari mwingine segerea.
Mwanamke kila akitoka wewe unapata msongo WA mawazo.

Na ukioa mwanamke mbaya ndiyo hivyo anaweza kuwa wa kwako pekee lakini hapo Sina uhakika.
Inapendeza zaidi ukiwa na mwanamke mzuri WA sura na tabia lakini hakuna kiumbe ambacho hakina upungufu change msingi uvumilivu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke tabia bhana
Uzur utapatka huko mbele
Kwa mbele

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
kiukweli mwanamke tako bana
mwanamke lazima uwe na tako
tako lisikosekane kwa mwanamke
mtoto wa kike tako linakuongezea CV

I wish snura angepita hapa

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Mwanamke K Sura inafuata ndio mnakaguana tabia

Rubiikimimi

[HASHTAG]#rubii[/HASHTAG],
Ukiandika huwa naelewa ila leo naona kabisa niko feri japo safari yangu nimekata tiketi ya bombadier kulekea Mwanza!!

Sasa sijaelewa kama nitafika salama au ndiyo nimepotea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom