Mugabe Kugombea Urais Kwa Mara Nyingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mugabe Kugombea Urais Kwa Mara Nyingine

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Mar 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe Friday, March 05, 2010 12:10 AM
  Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 86 amesema yuko tayari kugombea urais kwa mara nyingine kuliongoza taifa la Zimbabwe. Akiongea na waandishi wa habari mjini Harare, rais Robert Mugabe ambaye anaendelea kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 30 sasa, alisema kuwa yuko tayari kugombea tena urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika miaka miwili ijayo.

  Mugabe alisema kuwa iwapo chama chake cha ZANU-PF kitampitisha kugombea urais basi atasimama kwa mara nyingine kugombea urais.

  Mugabe ambaye alianza kuitawala Zimbabwe tangia ilipopewa uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980, alishinda uchaguzi wa urais uliopita ingawa kambi ya upinzani iligoma kukubali matokeo ya uchaguzi ikisema kuwa hila zilifanyika.

  Hali hiyo ilisababisha mtafaruku nchini Zimbabwe ambapo uchumi wake uliyumba kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na mataifa ya magharibi.

  Pesa ya Zimbabwe ilipoteza thamani yake na kuifanya Zimbabwe izitose pesa zake na kuanza kutumia dola za kimarekani na Rand za Afrika Kusini kama mbadala wa pesa zake.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hakuna la ajabu kwa Bob.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Kwani sheria yao Zimbabwe inasema nini kuhusu kugombea urais na rais anayemaliza ngwe yake?

  - Max vipi ndugu yangu longtime salama sana?

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #4
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ghadafi mara ya mwisho aligombea lini?
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Ndio ma-dictactor wa hali ya juu Africa waliobaki, wamerithi kutoka kwa Mobutu et al.
   
 6. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,339
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  No no no no no Bob, enough is enough!!!! Let them breath another type of air Bob.
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duu,huyu jamaa maezidi anakuwa kama Kakobe,muhubiri pekee kanisani kwake..
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...