real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,303
Harare, Zimbabwe. Mamlaka nchini Zimbabwe zimekubaliana kuwa Robert Mugabe aliyejiuzulu wiki hii hatafunguliwa mashtaka na badala yake ataendelea kupata haki zake zote kama kiongozi mstaafu.
Duru za habari zinasema makubaliano hayo yalifikiwa kabla ya kiongozi huyo kutangaza kuachia madaraka ikiwa Mugabe, mwenye miaka 93 alilazimika kujiuzulu Jumanne wiki hii baada ya wabunge wa nchi hiyo kuanzisha mchakato wa kumuondoa madarakani.
Hajaonekana hadharani tangu alipolihutubia taifa Jumapili iliyopita na kukataa wito wa kujiuzulu.
Inaelezwa kuwa kiongozi huyo bado yuko mjini Harare pamoja na mkewe, lakini haijafahamika wazi zaidi ni kwa mazingira yapi.
Makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo, Emerson Mnangagwa, aliyefutwa kazi na Mugabe mapema mwezi huu, anatarajiwa kuapishwa kesho Ijumaa, baada ya kurejea jana nchini humo.
Ripoti nyingine zinasema Mugabe ataendelea kupata haki zote kama rais mstaafu ikiwamo kupokea mshahara anaochukua rais aliyeko madarakani.
Mugabe amewahi kuzungumzia mshahara wake na katika moja ya mahojiano aliyofanya mwaka 2015 alisema mshahara wake kwa mwezi ulikuwa Dola za Marekani 12,000. Iwapo angesubiri kuondolewa madarakani kwa azimio la bunge angekuwa amepoteza haki zake lakini hatua ya kujizuru kwa hiari alindwe na katiba.
Chanzo: Mwananchi