Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,231
- 21,421
Mugabe akimwaga cheche.
Wednesday, June 25, 2008
Raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe, leo ameondolewa cheo cha Knight Commander of the Bath au KCB.
Taarifa imetolewa leo na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza kupitia waziri wake bwana David Millband ambae amemshauri malkia wa Uingerea atengue cheo hicho.
Cheo cha KBC ni muhimu sana katika nchi za jumuia ya Madola na hupewa wale watu ambao wanatambulika kwa mchango wao katika shughuli mbalimbali katika nchi zao na ushiriki wao na mkoloni wa zamani.
Mugabe alipewa cheo hiki mwaka 1994 na aliekuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati huo bwana John Major.
Kwa mujibu wa wizara hio , Mugabe anaondolewa kwa sababu za ukiukaji wa haki za kibinadamu na kutoheshimu demokrasia.
Kuondolewa kwa cheo hicho kumechukua wiki kadhaa kwani kunahitaji ushauri na uangalifu katika sheria na pengine marejeo ya sheria ya kutoa vyeo hivyo na pia Malikia hupaswa kusikilizwa.
Pai hatua hio itarahishisha hatua mbalimbali kuchukuliwa ili kumshitaki Mugabe akiwa huru kutoka katika vyeo kama hicho ambacho kingechelewesha hatua hizo.
Haya hayo ndio mambo ya wakubwa wa dunia.
Na World Media.