DC Rorya: Usipotatua mgogoro wa ardhi kati ya Kijiji cha Nyamaguku/Iryenyi na Rabuor madhara yake yatakuwa makubwa!

Ihayabuyaga

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
413
479
Imenenenwa na wahenga, "usipoziba UFA utajenga UKUTA"

Katika tembeatembea zangu kikazi wilayani Rorya nimekutana na mpogoro wa ardhi unaohusisha MIPAKA kati ya kijiji cha Rabuor na Nyamaguku. Inasemekana kwamba baadhi ya wanakijiji wa Rabuor wamekuwa wakivamia eneo la kijiji cha Nyamaguku hususani kwenye bonde la mpunga lililoko kwenye scheme ya kilimo cha mpunga Iryenyi.

Wanakijiji hao wamevamia eneo hilo na kulima wakiwa na silaha za jadi. Katika kuchukua hatua wazee wa kijiji cha Nyamaguku walikutana jana na kuzungumzia namna watakavyotatua mgogoro huo kwa njia za kidiplomasia.

Mapema leo wazee wa mila wa kijiji hicho wamekutana na vijana wote wa kijijini hapo na kuwataka kuandaa silaha za jadi kwa ajili ya kulinda ardhi yao pindi juhudi za kidiplomasia zitakapogonga mwamba.

Bwana DC wa Rorya, hilo jumba bovu litakunagukia...chukua hatua sasa..
 
Back
Top Bottom