Mugabe afanya njama za kumpaisha mkewe

Mugabe afanya njama za kumpaisha mkewe

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Harare, Zimbabwe: Rais Robert Mugabe amekubali kugeuza kongamano la mwaka la Zanu PFlililopangwa kufanyika Desemba kuwa mkutano mkuu wa congress unaotarajiwa kutumika kumshusha Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa na kumpaisha mkewe Grace kuwania urais katika chama.

Kamisaa wa Taifa wa Zanu PF Saviour Kasukuwere ndiye aliyependekeza suala la mkutano wa congress alipokuwa anawasilisha ripoti yake kwenye kamati kuu ya chama Jumatano lakini ilibainika kuwa kinara huyo wa kundi la G40 alikuwa amepata ushauri kutoka majimbo matatu tu.

"Mugabe alisema utakuwa ukiukwaji wa taratibu hivyo akaagiza kamati ya maandalizi kuhakikisha ushauri umepatikana kutoka majimbo yote. Kutakuwa na vikao vya uratibu wa majimbo kutafakari suala hilo kuanzia mwishoni mwa wiki hii.

"Mkutano mkuu wa chama umepangwa ili kufanya mabadiliko ya katiba ili kuingiza kifungu cha kuwa na makamu wa rais mwanamke au kuanzisha makamu wa tatu wa rais,” mtu wa ndani alidokeza.

"Suala la urais limekamilika lakini misuguano ya ndani kuhusu kuwania mamlaka na umri wa Mugabe vimelazimisha kutafakari na Nyanja mbalimbali. Kumbuka kuwa Grace anataka madaraka na amekuwa akiomba awe makamu wa rais sambamba na Mnangagwa".

Msemaji wa Zanu PF, Simon Khaya Moyo amekataa kuzungumzia suala hilo.

Miezi miwili iliyopita Mugabe aliwataka wajumbe wa Zanu PF kufikiria kuingiza katika katiba nafasi ya makamu wa tatu wa rais.

Hii ilikuwa baada ya mkewe kumtaka kiongozi huyo mkongwe wa Zanu PF kumtangaza mrithi anayempendelea katika mkutano mkuu wa wanawake.

- Mwananchi
 
HABARI,
Kwa mwenendo huu wa mugabe na mkewe mwisho wake ni mbaya huyu mama ataaibika vibaya na atadhaliliswa sana kama akitaka madaraka hayo ni heri mugabe angebaki pembeni na kuenziwa kama baba wa taifa la zimbabwe.

Na hilo zoezi la kumweka mkewake kamwe halitafanikiwa.

LUMUMBA
 
Afrika aliyeturoga sijui ni nani aisee!!

Hivi kuna utamu gani kufia madarakani? Ina maana bila familia ya Mugabe Zimbabwe haiwezi kuendelea kuwapo? Uganda nako kuna unyoko unaendelea,, sijui shida ni nini aiseee!! Na mishabiki yao nayo inakera sana!!
 
Kwa siasa za Afrika hapo hakuna geni ingawa wengi haturidhishwi nayo, lakini hakuna namna. Ukishindwa kumpa uraisi ndugu utampa hata ubunge wa viti maalum bint yako nk
 
Back
Top Bottom