Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by sulphadoxine, Jun 16, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MWENYEKITI wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni zilizopo nchini, Ali Mufuruki amesema vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini, wanashindwa kupata ajira kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa katika soko la ajira.Mufuruki alisema vyuo vingi nchini vinazalisha watu wasio na sifa na kushindwa kupata ajira katika soko la ushindani.Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi jioni, wakati wakurugenzi hao walipokutana kwa ajili ya kula chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.Umoja wa maofisa hao wamekuwa wakikutana mara moja na pia kupata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zinazohusiana na uchumi na biashara.“Vyuo vinazalisha watu ambao kampuni na mashirika mbalimbali hawahitaji wahitimu ambao wamesoma nadharia.

  “Kwa mfano, kama mtu umesoma Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, ukaajiriwa kwenye kampuni fulani inayohusika na shughuli hizo, itabidi kampuni iliyokuajiri iingie tena gharama ya kukusomesha ili uweze kufanya kazi kwa vitendo zaidi,” ,” alisema Mufuruki.Kwa mujibu wa Mufuruki, hali hiyo ndiyo chanzo cha kampuni nyingi kuajiri watu kutoka nje ya nchi, licha ya kuingia gharama kubwa.Alisema pamoja na mambo mengine, hali hiyo inachangiwa na mitaala ya vyuo mbalimbali, kufundisha vitu ambavyo kwa sasa havihitajiki kwenye soko la ajira.
  “Ndiyo maana leo tumeamua kumwalika Mkuu wa Shule ya Bishara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS, Dk Marcellina Chijoriga ili tubadilishane mawazo, tuangalie ni kwa namna gani kwa pamoja tutaweza kukatatua tatizo hili,” alisema Mufuruki.
  Kwa upande wake Dk Chijoriga alisema shule hiyo imebaini kasoro hiyo na kwamba katika kuipatia ufumbuzi, wameamua kuanzisha mfumo mpya na kwamba wanafunzi sasa watapaswa kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka sita.Alisema mfumo huo utaanza mwaka huu na kwamba wanafunzi watafanya mafunzo hayo mwaka wa mwisho tofauti na mwanzoni walikuwa wakiyafanya kwa miezi miwili tu.
  “Hivi karibuni nilitembelea baadhi ya vyuo huko Denmark, kule mwafunzi akimaliza mwaka wa kwanza anaenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu, pia mwaka wa pili na wa tatu anafanya hivyo hivyo, hii inamjengea uzoefu mzuri sana,” alisema Dk Chijoriga.
  Alisema wanafunzi wanapaswa kufanya mafunzo hayo bila kujali kama watalipwa na kampuni husika. “Huko kwa wenzetu, mwanafunzi akienda kufanya haya mafunzo, anailipa kampuni, sasa hapa kwetu hiyo hali haipo, ni vyema sasa wanafunzi wetu wakabadilisha mitizamo yao, wajue wanachoenda kufanya katika kampuni hizo ni kujifunza na siyo vinginevyo,” alisema Dk Chijoriga.

   
 2. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  But they are good in STRIKING
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Sijaona kipya,ukisema field miaka yote mtoto awapo chuoni,mbona imeshakuwepo nchini? Ukiangalia chuo cha usimamizi wa fedha, IFM mwaka wa kwanza mpaka wa tatu wote uenda mafunzo kila mwaka,cha muhimu makampuni na waajiri wapunguze mizengwe ktk soko la ajira.
   
 4. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii mizee ya zamani ndo inakwamisha vijana, sasa hizi kauli gani za mzalendo huyu mufuruki, unadhani mtu bila kupewa nafasi ya kufanya practical huo uzoefu ataupataje, tupeni nafasi, field zenyewe ishu utadhani unaomba kazi. Hii nchi sijui vipi, huyo mwenyewe mufufruki anasema hivyo leo kwa sababu alipewa nafasi akapata uzoefu, muongo mkubwa sidhani kama hata kama engineer wa ulaya fresh from school anaweza direct kufanya kazi field bila ya kuwa chini ya usimamizi wa engineers wazoefu then ana take off baada ya kupata experience mradi nadharia anayo. Na ndivyo ilivyo kwetu bongo. Bora kujiajiri mizengwe imekuwa mingi sana hapa bongo.
   
 5. Adu gida

  Adu gida Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  , kaka hapo umesema na tatizo undugu ni mwingi wanataka mtu mwenye degree na wa2 wanaomba ila mwisho wacku anachukuliwa mtoto wa mjomba kamaliza form 4, sasa hapo unaraumu nn lazima yapate watendaje wabovu na wapoteze hela we ofisi nzima wanaongea kiruga alafu wizara, mi naona tatizo lipo kwao watendaji
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hivi vijana wengi wa kisomali somali aliowajaza kwenye biashara zake wasiojua kiswahili wala kiingereza kwa ufasaha, walisoma vyuo gani na mwaka gani kule mogadishu?
   
 7. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG] Re: Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira[/h]

  [​IMG] Originally Posted by Rutashubanyuma [​IMG]
  Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira Wednesday, 15 June 2011 22:29 Fredy Azzah MWENYEKITI wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni zilizopo nchini, Ali Mufuruki amesema vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini, wanashindwa kupata ajira kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa katika soko la ajira.Mufuruki alisema vyuo vingi nchini vinazalisha watu wasio na sifa na kushindwa kupata ajira katika soko la ushindani. Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi jioni, wakati wakurugenzi hao walipokutana kwa ajili ya kula chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.Umoja wa maofisa hao wamekuwa wakikutana mara moja na pia kupata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zinazohusiana na uchumi na biashara."Vyuo vinazalisha watu ambao kampuni na mashirika mbalimbali hawahitaji wahitimu ambao wamesoma nadharia. "Kwa mfano, kama mtu umesoma Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, ukaajiriwa kwenye kampuni fulani inayohusika na shughuli hizo, itabidi kampuni iliyokuajiri iingie tena gharama ya kukusomesha ili uweze kufanya kazi kwa vitendo zaidi," ," alisema Mufuruki.

  Kwa mujibu wa Mufuruki,
  hali hiyo ndiyo chanzo cha kampuni nyingi kuajiri watu kutoka nje ya nchi, licha ya kuingia gharama kubwa.  Kwa maoni yangu huyu Mr Mfuruki is just another thick headed executive who wines and dines without knowing what is at stake.
  Ni maoni kama haya ya watu walio mbali na hali halisi ya sekta ya mafunzo nchini.
  Taasisi zilizo nyingi huwa zina mawasiliano ya karibu sana na wadau wao katika vyuo vya mafunzo-and this is a long term and lasting strategy.
  Kwamba Mfuruki and co. wanakimblia Kenya kuajiri, mi ningemuuliza je hao Wakenya wanao waajiri wanatoka straight out of college au vile vile wamekuwa trained baada ya kumaliza mafunzo yao?
  Kwamba hataki kuwa train vijana wanaotoka vyuoni ni kukwepa wajibu kama Mtanzania, kuendeleza vijana wetu, and at worst it is selfish.

   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Tunasoma tupate vyeti sio tupate elimu...migs et al zikiwa kazini
   
 9. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Taasisi zetu nyingi hazijakomaa sana kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa mwanafunzi kujifunza kitu cha maana awapo field.Mfano unakuta mtu wa IT anapokuwa field anaishia ku-print tu documents na kibahatika ata-scan virus. Wanafunzi wengine, hawaendi sehemu ambayo wanaweza wakajifunza kitu, bali sehemu ambayo atalipwa pesa, hata kama hiyo kazi haiendani na anachosomea. Pia, kutokana na kukua kwa udahili na kuongezeka kwa gharama za elimu ya juu, muda wa field umepunguzwa sana na baadhi ya vyuo kuondolewa kabisa.

  Sababu ya msingi kabisa ni wanafunzi wenyewe. Yaani kwa mfano, mtu anajua kabisa communications skills zake sio nzuri (na wapo wengi, hasa kujieleza kwa kiingereza), lakini bado hafanyi bidii kujifunza, anaishia kusema hiki mimi siwezi. Wengi wanasoma kupata cheti na sio maarifa-hapo kuna kudesa kwa sana na uvivu wa kusoma. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza akafanya lakini hafanyi-mfano kama ni mwanafunz wa IT badala ya kununua PC ananunua TV au redio kubwa(music system), unakuta mwanafunzi wa IT hajawahi hata kufungua PC yake aone ndani kuna nini. Pia, IT inabadilika kwa kasi sana, humwoni akijisomea vitu ambavyo hafundishwi darasani. Hali ni hivyo hivyo kwa kozi zingine.
   
 10. Nguchiro

  Nguchiro JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 365
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mada imetulia ila ukweli usemwe kwamba matatizo yapo sehemu kibao, 1.Course nyingi mambo 2nayoyasomea leo katika 2000s ndo yaliyosomwa 1980s handout imepigwa copy hadi haisomeki tena2.Cc 2ko bongo huyo dokta ana2pa mifano ya denmark wapi na wapi bwana,we r miles away economically from where denmark is,we unaniambia dent wa chuo ailipe kampuni anayoenda kufanya field!that is pathetic wakati haohao msosi ukiongezeka 300 tu wanagoma3.Ila na sisi magraduate wa bongo wengi ha2ko creative katika kujua mambo ila inatia aibu graduate kushindwa kujitetea kwa 20 min katika interview panel ilihali umeweza kujitetea kwa miaka 3/5/7 kusomea degree au 2likuwa 2nafundishwa kwa kiswahili?2nadesa? 2nakula simbi?mi niliwahi kwenda katika interview fulani hapa jijini 2 years ago kuna wa-Tz waliaga kabla hata ya kuingia katika interview panel kisa interviewer ni mzungu na mainterviewee wengine ni wakenya4.Kampuni yenye HR department yenye wa2 wanaojua taaluma yao hawalalamiki suala la kumtrain new employee aweze kuwa competent na kufanya kazi zake kwa ufasaha coz wanakuwa wako focused ila kampuni inayodai kumtrain new employee wao wanaingia hasara i doubt them by 200% kama kweli Human Resource Manager/ Officer wao alikidhi vigezo vya kuwa HRM/O au kampuni yenyewe haijui suala la Human Resource Development ni nini? Placement?5.Kabla ya kumjadili huyo Mufuruki cjui inabidi 2angalia wakati anaongea alikuwa mzima au kalewa?kama alikuwa amelewa 2tamsamehe ila km alikuwa hajalewa wat he said is the most stupid thing to say in public conference ever,nawasilisha hoja
   
 11. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jama kwa manufaa ya nchi ukweli usemwetu!
  vjana wetu wengi wa sasa ni kama wanatoka vyuoni wakiwa bado
  hawajakomaa sio kitaaluma/professional bali hata akili tu ya kawaida ya kudili na masuala
  mbalimbali ya kiofisi.
  Mwakajana nilikua na wanafunzi wawili ofisini kwangu.
  walikuamwaka wa tatu by tyhen, lakini ukweli ni kua hata copy and pest ya kompyuta hawakua wanajua.
  sasa hapa jamani mtu akisema kauli kama hii mtamkatalia!?
  kuna level ambayo mtu akiwa amefika tunaassume kua anujua vitu flaniflani, hata kama ni asignment unamwachia labda
  utakujatu kumpa correction kidogokidogo, na huku ndiko kujifunza na kupata uzoef,
  lakini sas kama mtu hata ku taip hawezi kweli unamsaiiaeje??

  wadogo zangiu viuoni, nachowashauri ni kua hakuna kitu rahisi mtaani, kila kutu ni changamoto,;'jitahidini kujiweka
  pazuri.
   
 12. Nguchiro

  Nguchiro JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 365
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Thanx Tasia,kwa wenze2 mnaotoka vyuoni we want u 2b ready 2 face challange na ni aibu graduate wa chuo kutojua basics za computer coz ujuzi wa computer ni muhimu ktk applicatn na sasa mambo ya jumuia ya afrika mash. hiyo c ndo tutai aibu,hata kama ndugu yangu ndo unataka nikusaidie jamani katika hali kama hiyo ni kuleteana mitihani sasa
   
 13. herrypeter1

  herrypeter1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1000 per cent true..
   
 14. P

  Positive Thinker Senior Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi ninachosema ni kuwa watu wapewe nafasi huwezi kutoka chuo ukawa experienced lazima upewe nafasi ili ujifunze then utake over.Kingine wanachuo wanapenda kulipwa sana wakati wakiwa Field nakumbuka wakati nipo 2nd Year chuo nilifanya Field sehemu fulani for Six weeks jamaa wanakutrain 2 weeks kama kichwa chako hakiko sawa wanakutrain for 3 weeks after that wanajua upo fit unaanza kupiga mzigo kama muajiriwa ukimaliza 6 weeks na upo safi wanakupa mkataba wa kufanya kazi for temporary Evening,Weekend and Night shift hadi utakapomaliza chuo pesa sio nyingi sana kama unataka kujifunza kazi ni nzuri sana na utakuwa na exposure na ukiangalia majority ya wafanyakazi kwenye Technical department walifanya Field pale na kuajiriwa hii hata cost ya kuajiri inakuaje ndogo kwenye kampuni kwani mtu anakuwa ndani ya kampuni na anaelewa kampuni vizuri kikubwa watu wawe willing kujitolea tu na kujua kazi kwani market yako itakuwa kubwa sana.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Msimlaumu Mufuruki, huenda anachosema ni kweli.

  Mimi nimetoa opportunities kwa vijana wengi sana lakini kila mmoja ni kama sifuri. Tumejaribu kupata vijana wa kufanya kazi ambazo hata mtu wa form four anaweza kufanya lakini ni ngumu sana kwa TZ.

  Nafikiri tatizo ni elimu wanazopewa vijana siku hizi na pia culture mpya ya kukosa uwajibikaji na ujanja ujanja.

  Tusipokuwa waangalifu wageni watachukua hata kazi zile ambazo vijana wetu wanaweza kuzifanya.

  Mimi nimekuwa nikiongea na wafanyabiashara au wenye makampuni wengi. Inaelekea tatizo ni hilo hilo, kila mtu anasema vijana hawajitumi, sio wabunifu na wanaiba kila wakipata nafasi.

  Inafika mahali mtu uzalendo unakushinda mpaka unafikiria kuchukua Mkenya maana hakuna mtu anayetaka kuangushwa kwenye miradi yake.

  Mambo matatu ni muhimu mno; kujituma, ubunifu na uaminifu. Mtu unamwamini na kumwachia madaraka makubwa lakini hata miezi haipiti anaanza kukuibia.

  Kuna jamaa yangu mwingine naye ana biashara zake Iringa yaani kahangaika mpaka na ndugu na wote wanashindwa kufanya kile anachotaka yeye. Mpaka kaamua amlipe mshahara mdogo wake akae bure Dar aondoke kwenye biashara yake maana kuwepo pale ni hasara tupu. Anataka kujaribu watu wengine.

  Najua sio wote lakini kwa Tanzania ya leo, nakuhakikishia kijana kama ni mchapa kazi, mbunifu na mwaminifu waajiri watakukimbilia na kukulia maana waajiri wengi hasa kampuni ndogo ndogo tayari wameshakiona cha mtema kuni kwenye kuwa na wafanyakazi bomu. Huo ni ushauri wangu na experience yangu, ufuate au utupe jalalani.
   
 16. M

  Mtanganyikan Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo neno. Maana kwani hata kijana akipata nafasi ya kwenda field, kazi anazopewa zinaweza kuwa si za kumpa changamoto kujiandaa na ajira halisi
   
 17. egbert44

  egbert44 JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2006
  Messages: 361
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  matatizo ni mengi 1. vyuo vinatoa mitaala isiyoenda na wakati na mingi ni ya kuchoshana tu kwa mfano ajira inatoka unaona kabisa ni ya majungu eti wanataka uwe na MCSE, JAVA, PHP, na mauongo mengi tu sasa hapa hutampata kijana wa vyuo vya serikali zaidi waliopita short cut akaenda kwa mdosi na chuo cha gorofani na kiti kimoja anatusua. 2. vyuoni hamna nafasi ya kuzama mambo mengine zaidi ya kufukuzia marks tu maana hayo masomo mnayolundikiwa usipime ukizubaa umekwaa sup na kama siyo disco. 3. Waajiri wenyewe wengi wameiba tu na kutoka kimtindo leo wanaanza nyodo tunawajua wengi tu walianza na viofisi vya mazabe wakapewa tenda za undugunization leo wametoka wanaanza matuc hadharani. 4. Mi naona elimu ingebadilika watu wakafundishwa proffessional course tu kama wanavyofanya veta mambo yangekuwa pouwa maana kama ni kujua umombo mbona wachina hawajui na kazi wanafanya na washwahili tu wa mitaani ni miradi inanyooka, haya mambo ya interview bin umombo miyeyusho tu.Nawakilisha
   
Loading...