Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira Wednesday, 15 June 2011 22:29 Fredy Azzah MWENYEKITI wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni zilizopo nchini, Ali Mufuruki amesema vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini, wanashindwa kupata ajira kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa katika soko la ajira.Mufuruki alisema vyuo vingi nchini vinazalisha watu wasio na sifa na kushindwa kupata ajira katika soko la ushindani. Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi jioni, wakati wakurugenzi hao walipokutana kwa ajili ya kula chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.Umoja wa maofisa hao wamekuwa wakikutana mara moja na pia kupata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zinazohusiana na uchumi na biashara.“Vyuo vinazalisha watu ambao kampuni na mashirika mbalimbali hawahitaji wahitimu ambao wamesoma nadharia. “Kwa mfano, kama mtu umesoma Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, ukaajiriwa kwenye kampuni fulani inayohusika na shughuli hizo, itabidi kampuni iliyokuajiri iingie tena gharama ya kukusomesha ili uweze kufanya kazi kwa vitendo zaidi,” ,” alisema Mufuruki.Kwa mujibu wa Mufuruki, hali hiyo ndiyo chanzo cha kampuni nyingi kuajiri watu kutoka nje ya nchi, licha ya kuingia gharama kubwa.Alisema pamoja na mambo mengine, hali hiyo inachangiwa na mitaala ya vyuo mbalimbali, kufundisha vitu ambavyo kwa sasa havihitajiki kwenye soko la ajira. “Ndiyo maana leo tumeamua kumwalika Mkuu wa Shule ya Bishara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS, Dk Marcellina Chijoriga ili tubadilishane mawazo, tuangalie ni kwa namna gani kwa pamoja tutaweza kukatatua tatizo hili,” alisema Mufuruki. Kwa upande wake Dk Chijoriga alisema shule hiyo imebaini kasoro hiyo na kwamba katika kuipatia ufumbuzi, wameamua kuanzisha mfumo mpya na kwamba wanafunzi sasa watapaswa kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka sita.Alisema mfumo huo utaanza mwaka huu na kwamba wanafunzi watafanya mafunzo hayo mwaka wa mwisho tofauti na mwanzoni walikuwa wakiyafanya kwa miezi miwili tu. “Hivi karibuni nilitembelea baadhi ya vyuo huko Denmark, kule mwafunzi akimaliza mwaka wa kwanza anaenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu, pia mwaka wa pili na wa tatu anafanya hivyo hivyo, hii inamjengea uzoefu mzuri sana,” alisema Dk Chijoriga. Alisema wanafunzi wanapaswa kufanya mafunzo hayo bila kujali kama watalipwa na kampuni husika. “Huko kwa wenzetu, mwanafunzi akienda kufanya haya mafunzo, anailipa kampuni, sasa hapa kwetu hiyo hali haipo, ni vyema sasa wanafunzi wetu wakabadilisha mitizamo yao, wajue wanachoenda kufanya katika kampuni hizo ni kujifunza na siyo vinginevyo,” alisema Dk Chijoriga.
 
Comments 0 #1 Kipili 2011-06-16 01:14 Huyu Mufuruki anajua anachoongea au ndiyo siasa za kiukurugenzi?, ni kwa nini watanzania haohao wanaomaliza vyuo vya Tanzania wapoenda nje ya Tanzania hufanya kazi kwa ufanisi sana? Hii ni kasumba waliyon nayo waajiri wa Tanzania kudharau home made resources na kuthamini wale wanaosoma nje ya Tanzania hata kama wamesomea vyuo vya grade 4
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira Wednesday, 15 June 2011 22:29 Fredy Azzah MWENYEKITI wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni zilizopo nchini, Ali Mufuruki amesema vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini, wanashindwa kupata ajira kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa katika soko la ajira.Mufuruki alisema vyuo vingi nchini vinazalisha watu wasio na sifa na kushindwa kupata ajira katika soko la ushindani. Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi jioni, wakati wakurugenzi hao walipokutana kwa ajili ya kula chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.Umoja wa maofisa hao wamekuwa wakikutana mara moja na pia kupata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zinazohusiana na uchumi na biashara."Vyuo vinazalisha watu ambao kampuni na mashirika mbalimbali hawahitaji wahitimu ambao wamesoma nadharia. "Kwa mfano, kama mtu umesoma Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, ukaajiriwa kwenye kampuni fulani inayohusika na shughuli hizo, itabidi kampuni iliyokuajiri iingie tena gharama ya kukusomesha ili uweze kufanya kazi kwa vitendo zaidi," ," alisema Mufuruki.

Kwa mujibu wa Mufuruki,
hali hiyo ndiyo chanzo cha kampuni nyingi kuajiri watu kutoka nje ya nchi, licha ya kuingia gharama kubwa.

Kwa maoni yangu huyu Mr Mfuruki is just another thick headed executive who wines and dines without knowing what is at stake.
Ni maoni kama haya ya watu walio mbali na hali halisi ya sekta ya mafunzo nchini.
Taasisi zilizo nyingi huwa zina mawasiliano ya karibu sana na wadau wao katika vyuo vya mafunzo-and this is a long term and lasting strategy.
Kwamba Mfuruki and co. wanakimblia Kenya kuajiri, mi ningemuuliza je hao Wakenya wanao waajiri wanatoka straight out of college au vile vile wamekuwa trained baada ya kumaliza mafunzo yao?
Kwamba hataki kuwa train vijana wanaotoka vyuoni ni kukwepa wajibu kama Mtanzania, kuendeleza vijana wetu, and at worst it is selfish.

 
kwa upande mmoja mufuruki yupo sahihi; hebu jiulize wanafunzi wa UDOM waligoma kwa sababu waliambiwa hamna field.. unatgegemea mwanafunzi anayetoka UDOM atakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi bila kupatiwa mafunzo ya ziada!! hilo ni lazima tulione jamani!! tusilaumu tu..

tena mimi nashauri wanafunzi wanaosoma masuala ya uhandisi wa mitambo wawe wanakuwa attached SIDO kujifunza ubunifu wa mitambo. ukienda muhimbili hali imebadillika, zamani wanafunzi walikuwa wanapata mafunzo ya vitendo ya kutosha lakini sasa imekuwa taabu kwa sababu idadi ya wanafunzi imekuwa kubwa mno hivyo muda wa mafunzo kwa vitendo imepungua (nani atakubali kutibiwa na output hii). hebu jaribu kwa wanaosomea marketing.. utashangaa mtu anamaliza chuo hawezi hata kutayarisha hata a marketing flier.. hebu waulize wafamasia wanaomaliza Muhimbili au St. John kama wanaweza kutengeneza dawa bila kupata mafunzo ya ziada wakiwa kazini.
watu ambao wamekuwa mstari mbele (kwa maoni yangu) katika elimu vitendo ni angalau walimu na architecture (naomba nisahihishwe kama nimekosea).

kwa ufupi vyuo vijirekebishe!!
 
Huyu Mafuruki may be anaongea anachokijua. Nina imani amejionea yote hayo during the job interviews.
 
Ukweli mtupu, elimu inayopatikana vyuo vingi (hata vya nje) haiendani na waajiri wanachotaka, kuna disconnect kati ya elimu tunayopata na hali halisi ya job market.
 
mkuu mimi nipo botswana na elimu yangu ina heshimika kiwango cha hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom