Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,618
Mufti Simba awasha moto
Tangu September 20, 2013, na | Imesomwa
mara 278 | Haina maoni
*Amvaa Sheikh Kilemile, amwambia afuate
sheria
Na Eben-Ezery Mende
MUFTI wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(Bakwata), Issa Shaban bin Simba amesema
yeye si msanii kama anavyoshutumiwa na
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mazungumzo
kati ya Waislamu na Serikali, Sheikh Suleiman
Kilemile.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu
jana, Mufti Simba alisema shutuma
anazotupiwa zinatokana na malalamiko yake
kwa Serikali kuhusu kupuuzia suala la
Mahakama ya Kadhi.
Kutokana na hali hiyo, Mufti Simba alisema
yeye yupo sahihi na kwamba anayemshutumu
atumie sheria badala ya kulalamika kwenye
vyombo vya habari.
Simba alisema anachofahamu ni kwamba
kupatikana kwa Kadhi hakuhitaji ushirikishwaji
wa taasisi zote za Kiislamu na kubainisha kuwa
kama kuna kosa lililofanyika sheria ndiyo
itatengua kitendawili hicho na si malalamiko.
Huyo Sheikh Kilemile kama anadhani
kulalamika ni dawa waulizwe Waislamu kuhusu
Mahakama ya Kadhi na mimi sitaki kuendeleza
mvutano kwenye vyombo vya habari, alingaka
Mufti Simba.
Kauli ya Simba imekuja baada ya Sheikh
Kilemile kudai kuwa Mufti huyo ni msanii katika
kupata Mahakama ya Kadhi.
Sheikh Kilemile alidai hatua ya kumuona Mufti
Simba msanii imekuja baada ya kujitokeza
akiilaumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa
kupuuza maoni ya Waislamu ya kutaka
kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Alisema lawama zilizotolewa na Mufti Simba
zinashangaza kwa sababu zaidi ya miaka mitatu
iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimuagiza Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda awasiliane na Bakwata ili
kumtaka Simba aunde jopo la masheikh kutoka
taasisi mbalimbali za Kiislamu ili liwe chombo
cha kuwakilisha Waislamu wote nchini.
Sheikh Kilemile alifafanua kuwa baada ya
kufanyika kwa vikao vingi chini ya uenyekiti wa
Mufti na vingine na Pinda mchakato huo
ulionesha kufikia hatua nzuri.
Alisema kikao cha mwisho cha jopo hilo chini ya
waziri mkuu kilihudhuriwa na baadhi ya
watendaji wa Serikali na mawaziri kadhaa
wakiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias
Chikawe, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina
Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge) William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Jaji Frederick Werema. Kwa vile
mahakama za kadhi zinapatikana pia katika nchi
nyingine za kisekyula kama Uingereza, India,
Kenya na hata Zanzibar, Wasira alimshauri
waziri mkuu upatikane ujumbe utakaokwenda
kutembelea nchi hizo na utakaokusanya
wajumbe kutoka serikalini na jopo la masheikh
kujionea taratibu za uendeshaji wa mahakama
za kadhi katika nchi hizo ili utakaporudi nchini
uweze kuelekeza jinsi ya kuziendesha
mahakama hizo hapa nchini.
Pinda alikubali na kuibariki rai hiyo. Aliamuru
upande wa jopo la masheikh utoe wajumbe
watatu na upande wa Serikali wajumbe wawili.
Ilikubaliwa kuwa gharama za kupeleka ujumbe
huo Uingereza, India, Kenya na Zanzibar zilipwe
na Ofisi ya Waziri Mkuu. Ujumbe huo ulitakiwa
uwe umekamilisha ziara hizo kabla ya Aprili,
2013, alisema.
Sheikh Kilemile alidai kabla ya kufanikisha
hayo, Mufti Simba alipuuza yale maazimio ya
kikao hicho na badala yake aliamua kuitisha
mkutano wa viongozi wa Bakwata mjini
Dodoma na kutangaza jina la kadhi wake mkuu
pamoja na wasaidizi wake bila kushauriana na
jopo la masheikh lililoteuliwa kushughulikia
mchakato mzima wa kupatikana Mahakama ya
Kadhi.
Source: Jamba Leo