Mufti mfikishie salamu zetu Mh rais atapofika kama mgeni rasmi katika hilo baraza la Eid...!

Status
Not open for further replies.
2020 sio mbali The Big Show. Vumilia si unajua wenzetu wanasema hatujasoma sisi wazee wa kariakoo japo vyuoni na uraiani wasio na kazi na degree vijana wetu wapo wengi.
 
1.Tulia kijana nikupatie darsa kiduchu.Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 1967 wapagani walikuwa wengi kuliko wakristo na waislam hilo sijambo geni hata Babu yangu hakuwa na dini aliamini dini za mizimu ya kabila lake kama matambiko na nk.Mambo hayo yote yanapingana na mafundisho ya dini ya kikristo nadhani uislam unakubaliana na mambo ya utabiri na nk ndio maana Sheikh Yahaya alikuwa akifanya hivyo na bado alikuwa kiongozi mashuhuri wa kiislam.Sensa ya mwaka 1967 ndio ilikuwa sensa ya mwisho yenye kipengele cha dini baada ya hapo kiliondolewa kwakuwa serekali waliona kipengele hicho hakina maana labda wewe unaona kina maana.

2. Takwimu zinasema idadi ya watu 362,161 walihesabiwa lakini hawakujibu kipengele cha dini.Therefore hatujui kama walikuwa wapagani,wakristo au waislam walkwepa kutoa taarifa za kipengele hicho.Sijui kwanini unakimbilia kutoa majibu wakati swali bado haujalielewa.

3. Tembelea dayosisi za wakatolic,walutheri,waanglikan,wapentekoste... kote huko wana idadi ya waumini wao walio katika taratibu zao na walio nje ya taratibu zao.Kwa lugha rahisi hawahitaji msaada wa serekali ili kufahamu idadi ya waumuni wake.Ukitembelea dayosisi ya kaskazini ukitaka taarifa za mahudhurio ya waumini miaka kumi au mwaka mmoja na sakada walizotoa utapewa bila wasiwasi wowote kwasababu upo utaratibu wala sijambo geni.Waislam waligoma kuhesabiwa kwasababu hawana utaratibu wa kujua idadi ya waumini wake ndio maana baadhi waligoma kuhesabiwa pengine wakitarajia msaada wa serekalli uwawezeshe kujua wako wangapi.

4. Refer majibu ya number 3.

Mwisho rejea number 3 wakristo wana utaratibu wa kujua idadi ya waumini wake,idadi ya watoto waliozaliwa,idadi ya watu walikufa ambao wanastahili kuhudumiwa na kanisa (taratibu za kanisa) na sasa kanisa lipo katika level ya mtaa kwa mtaa,kila jumamosi kuna ibada katika level hiyo so ushishangae ukiambiwa sasa wakristo ni 74% tulia tu hiyo ndio hali halisi.
Takwimu zako ziweke vizuri 2020 utazihesabu vizuri, si mlikuwa mnapigia debe mgombea wenu wa mabadiliko na yule mwengine padri, na kote mkashindwa. Sasa subirini maajabu 2020.
 
WAISLAM DINI YETU INAKUWA KWA HARAKA DUNIANI KOTE, UKRISTO ZAIDI UMEBAKI AFRIKA MSIWE NA WASIWASI , HII NI FURAHA KUBWA KWETU KULIKO VYEO VYA KIDUNIA AMBAVYO HAVITUFIKISHI POPOTE

kumbukeni kusoma na elimu dunia siyo mkalie elimu ahera peke yake. hapo mtazidi kutawalaliwa na wakristo hadi mwisho Wa dunia.
 
Sikubakubaliani na hiyo hoja angalau wewe umesema waislamu wapo takribani 20% vipi sisi Wa Adventista Wasabato mbona hata 1% hatufiki lakini hatulalamiki? Ikifika wakati tukaanza kumwamrisha Rais amteue Nani kwa nasaba za dini zetu tutaligawa taifa.Au ulitaka uteuliwe wewe ndipo ujue waislamu wamepewa fursa? Acha uchonganishi usio na maana.
 
Kweku kabisa. Mimi ni mkristo halisi, lakini nilipoangalis mf uteuzi wa makatibu tawala nilishtuka sana. Kweli hawa ndugu zetu wamesahaulika kidogo!
 
Hatuchagui mtu kwa dini yake wala kabila ata dini moja wakijaa aimanishi dini nyingine imebaguliwa kumbuka tuna chagua watendaji wa serikali atuchagui imamu wala padre
 
Hoja ni za msingi lakini nafasi ya waislamu nchi hii mungu ndo anajua
Lengo la serikali ni huduma bora kwa wananchi wote bila kujali dini wala jinsia wala kabila. Hebu niambieni kama barabara bora, afya bora, elimu bora, maji safi na salama, umeme wa uhakika, n.k vinatofautiana kati ya dini, makabila au jinsia!
 
Kigezo muhimu iwe uwezo alionao mtu na wala siyo dini ya mtu tuzingatie hilo maendeleo yatakayoletwa na viongozi walioteuliwa ni kwa ajili ya watu wote bila kubaguliwa kwa dini zao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom