Mufti ataka Waislamu waiombee dua Libya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mufti ataka Waislamu waiombee dua Libya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Issa bin Shaaban Simba amewataka Waislamu kuwaombea dua wenzao waliouawa katika vita inayoendelea Libya na wengine wanaodhulumiwa haki zao duniani.

  Alitoa mwito huo kwenye hotuba yake katika Msikiti wa Gaddafi mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

  Alisisitiza waumini wamwombee Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Waislamu duniani na wanyonge katika nchi zote bila kujali kama ni za Kiislamu.

  Mufti Simba alisema maadui wa Waislamu wanachochea watu wakorofi kuanzisha fujo na vurugu kwa kuwaunga mkono ili misaada inayotolewa na kiongozi wa Libya duniani kote ifikie mwisho.

  “Sisi hapa Dodoma tumepata msaada mkubwa kutoka Libya ni huu msikiti tuliuomba na tukaupata bila matatizo,” alisema Mufti Simba.

  Hata hivyo, alisema maombi yamewezesha maadui wa Gaddafi waliolenga kupiga nyumba yake kumkosa kwa kuwa ana hifadhi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa ibada anazofanya ni kubwa na ni mtu aliyehifadhi Kurani katika mwili wake.

  Aliyashutumu mataifa makubwa ya Magharibi kwa kuelekeza vita nguvu zao kuipiga Libya kwa kutoa mali kuwasaidia waasi.

  Wakati huo huo, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaaban aliwahimiza waumini kulinda utamaduni na kuenzi ustaarabu wa Kiislamu kwa kuepuka sera na utamaduni wa nchi za Magharibi unaolenga kutumia nguvu kuathiri mila na desturi za Kiafrika.

  Alisema utamaduni wa Magharibi unalenga kuvuruga tabia za vijana kwa kuwafanya waige mambo yanayokiuka maadili.

  Alitoa mwito wa kuiga mfano wa China na Japan zilizokataa kufuata sera na utamaduni wa nje na hivyo kuweza kupiga hatua ya maendeleo.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Issa bin Shaaban Simba amewataka Waislamu kuwaombea dua wenzao waliouawa katika vita inayoendelea Libya na wengine wanaodhulumiwa haki zao duniani. Huyu jamaa vipi? Dua lilihitajika kwa Osama!
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Anayepaswa kuombewa ni yeye Mufti ambaye anachanganywa na vijisenti toka kwa Gadaffi kiasi cha kutaka kuuingiza umma kwenye utumwa wake wa pesa. Koma mufti tafadhali.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee bana yaani hoja zake ni afadhali ya mwanangu gaude anayesoma chekechea!gadhafi kahifadhi korani mwilini mwake?duuh kazi kweli kweli
   
 5. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndiyo. Akikumbuka mchango alioutoa kwa wa Tz wakati wa vita ya kumng'oa nduli Amin, Uganda. Kwa hilo anaona Ghadafi anafaa sana. Ghadaf oyee, hoi? Oh Wadanganyika wepes kusahau. Kweli Wabongolala.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  watanzania ndiyo twahitaji dua ili Mungu atupe serikali mbadala, hii iliyopo inatuingiza jehanamu kabla ya wakati.
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Hivi Qatar ni miongoni mwa mataifa ya Magaribi?
   
 8. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,075
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280

  Dodoma........... Basi wao pekee ndio wamuombee dua!!!!!!!!!!!
   
 9. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waislamu tafuteni Mufti mwingine, manake huyu mzee naona kazi ishamshinda duh
   
 10. A

  Anold JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
   
 11. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Itakuwa kazi kama na aksofu wa Lutheri akisema tumuombee Lowasa , Sheikh wa Tabora akisema tumuombee RA na may be Pengo akisema tumuombee Chenge.

  Just bcs wanatoa sadaka kubwa kubwa na kusaidia jamii isifanye watu watu wawe vipofu na viziwi.

  Wanahohitaji kuombewa ni wanachi wa kawaida wa libya. na wala si Gaddafi.
   
 12. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kiongozi kwa hili nitawatetea wadanaganyika wengi wenye akili kidogo, huyu anaye mtetea Ghadaf ni kuwa upeo wake mdogo alionao. Misaada ya kujengewa nyumba za ibada nayo tunaiona kuna ina tija...huu ni uwezo mdogo sana wa kufikiri. It's like mdogo wangu mmoja nilikuwa nae middle east wakati Uprising inaanza, alilia sana na kusema kwanini wana mpiga Ghadaf mtu mwema, mcha mungu na aliwajengea Msikiti mkubwa sana Dodoma. Nilidhani aliyasema hayo kwa sababu ya umri wake...kumbe hata viongozi wake nao the same...aibu sana. Eeeh vita ya 1978-79 wakati huyu ndugu akimsaidia Idd Amini ( bila shaka kwasababu ya Imani yake pia) ilikuwa ni sahhihi? Mbona mnajifanya hamnazo wazee wazima?......Nachukua sera za Magharibi sometime lakini si kwa hili, tumtetee Ghadaf kwa kuzingati mambo mengine kabisa tofauti na huu upupu unaoelezwa na the so called Kiongozi.
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ile dhana ya money speaks imetimia.
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Aibu Mufti kajiingiza kichwa kichwa.
   
 15. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Sasa yupi kati ya Gadafi au wananchi wa Libya ndio wa kuonewa huruma?kwenye familia ya Gadafi wamekufa watatu je wananchi ni wangapi wameshafariki na maelfu kukosa makazi????Mufti umechemka sn
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hii ni sawa na kumwombea dua hitler, osama,sadam na waislamu wengine wachafu km hao............kweli uislamu ni unafiki................kuombea adui mkubwa wa haki?....ili iweje?.....km wananchi hawataki uwaongoze wewe unang'ang'ania ili umuongoze nani?.......jeuli na kiburi cha viongozi wa kiafrica na wale wengi wa kiislamu wasiotaka mabadilijko ndiyo chanzo cha migogoro mingi duniani.....
  Waislam wa tz msipoteze kuombea magaidi iombeeni tz yenye neema ambayo watu wake ni masikini wa kutuopwa isonge mbele acheni unafiki
  .-muombeeni kikwete aachane na mafisadi
  -iombeeni ccm iache kuwagawa watz kwa misingi ya dini kwa kuweka kwenye ilanai yao baadhi ya mambo ya dini fulani
  -vinginevyo tutakuwa km wabwbwajaji wazuri wa kitz
   
 17. x

  xman Senior Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mufti try to think before you speak, ghadafi anaonewa kwa lipi? haya ndio matokeo ya mtu kung'ang'ania madaraka kwa muda mrefu na pale wananchi wako wanapokuja juu kuhoji mtu anatumia nguvu ya jeshi kuwazima, ningemshauri mufti amuangalie ghadafi kama ghadafi namatendo yake kama kiongozi na sio ghadafi kama muislam.
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mufti acha kahawa maramoja moja jaribu castle,utafikiri vizuri tu
   
Loading...