Mufindi: Watu 18 wamefariki katika ajali ya Coaster na lori

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Watu 18 wamefariki dunia papo hapo, katika ajali ya gari Wilayani Mufindi katika barabara Kuu ya Iringa-Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Coaster ilikuwa inatokea Dar kwenda Mbeya

Aidha, amesema kwa taarifa za awali chanzo cha ajali hiyo ni kulikuwa na lori lililoharibikia barabrani na dereva wa Coaster hakuchukua tahadhari akaligonga lori hilo hali iliyosababisha kupatikana kwa majeruhi

Ameongeza kuwa wakati majeruhi wanaokolewa likaja lori jingine likawagonga tena waliokuwa wameanza kuokolewa na hivyo ajali ikawa mara mbili

Kuhusu majeruhi amesema wapo ila hajapata idadi kamili

2A3A5713-1008-47B6-AFCB-51515BA63BC4.jpeg

EF3A8C07-B8BF-444F-A9CD-33D3C60FE131.jpeg


Source: ITV
====


Eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40
 
Sad indeed.

Hii coaster siyo zile wanajiita Hakuna Kulala huwa wanasafiri usiku tu hao jamaa mwendo wao ni kama kimondo kuna siku nilimsikia nadhani mkuu wa mkoa wa Iringa akitoa tamko zisionekane barabarani na ajali hii inawezekana ikawa uchovu wa driver pamoja na hali ya ukungu ktk mikoa mingi kwa sasa,ukiiangalia hiyo picha ni kama Coaster ilikuwa wrong lane lorry likamkataa kwa kurudi kulia kisha Costa tena akataka arudi upande wake ndo akajaa.

Mungu azipokee roho za wahanga majeruhi awape afuweni na pole kwa wote waliowapoteza wapendwa wao.
 
duuh yani sehemu peupee hivyoo jamani au ndo ajali haina kinga.. wapumzike kwa amani
 
Watu 18 wamefariki dunia papo hapo, katika ajali ya gari Wilayani Mufindi katika barabara Kuu ya Iringa-Mbeya.
View attachment 2255971
View attachment 2255981

Source: ITV
Barabara kati ya Iringa mpaka Makambaku ni nzuri sana na inazo alama nyingi sana za barabarani ambazo huonekana vizuri hata wakati wa usiku, ajali kama hii hutokana na madereva kutokujua udereva wa kujihami ambao ni muhimu sana kuliko vyote kwenye udereva.
 
Back
Top Bottom