Muenzi Mke Wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muenzi Mke Wako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Mar 27, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Muenzi Mke Wako

  Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.

  Atashiriki katika nyakati zako nzuri,siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.

  Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku,kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye,na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako.Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.

  Kielezo bora kabisa ambacho mimi binafsi nishawahi kusoma kinafafanua ukaribu wawanandoa juu ya wao kwa wao na kielezo hicho kipo katika aya ya Qur-aan ambayo inasema:

  Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao
  Al-Baqarah 2:187

  Na Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga (stara), msaada (tegemeo), na mapambo ambayo vazi linampa mtu. Hebu jaribu kufikiri msafara wakati wa siku za baridi kwenda sehemu kama vile Alaska bila ya kuwa na nguo! Wanandoa wetu wanatupa kiwango kile kile cha faraja (liwazo), ulinzi, na msaada katika msafara wa maisha yetu katika dunia hii kama vile nguo itakavyofanya katika msafara wa Alaska.

  Mahusiano baina ya wanandoa ni ya kustaajabisha kabisa katika mahusiano yote ya kibinaadamu: Idadi ya mapenzi na mahaba, undani na ukaribu, huruma na imani, amani na utulivu ambao unajaza nyoyo za wanandoa ni jambo lisiloelezeka kwa wepesi. Ufafanuzi pekee wa mantiki ambao unaweza kuelezeka juu ya haya mastaajabu makubwa katika hisia zote za kibinaadamu ni kwamba: Ni kitendo cha Allah Subhanahu wa Ta'ala,

  Na Mwenyezi Mungu Amekuumbieni wake [na wenza katika jinsi yenu
  An-Nahl 16:72

  Mola wetu tu Allah Subhanahu wa Ta'ala katika katika Utawala Wake usio na upeo wa huruma Yake isiyo na mipaka na Hekima Yake adhimu Anaweza kujenga na kuzididimiza katika akili hizi hisia za kustaajabisha na za kubarikiwa katika nyoyo za wanandoa. Kwa kweli Allah Subhanahu wa Ta'aala Anawakumbusha wale ambao wanatafuta ishara Zake katika ulimwengu huu kwamba hisia hizi katika moyo wa wanandoa ni katika ishara Zake ambazo zinatakiwa zimuongoze mwanaadamu katika kuwepo Kwake kama Alivyosema katika Qur-aan,

  Na katika Ishara zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri."
  Ar-Ruum 30:21

  Lakini Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’aala Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu. Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati unavyosogea. Mapenzi yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.

  Kumbuka kwamba Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipata nafasi ya kwenda kwenye majangwa na kushindana mbio na mke wake Bibi 'Aishah. Bibi 'Aishah alimshinda Mtume lakini baadae aliponenepa, Mtume alimshinda Bibi 'Aishah. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimchukua mkewe kwenda kuwatazama vijana wa Ki-Ethiopia wakicheza michezo ya utamaduni wao. Maonyesho ya hisia yanahitajika kuweza kuufanya mshikamano wa ndoa usifanye kutu na kuoza. Kumbuka kwamba utapata thawabu kutoka kwa Allah (Subhanahu wa Ta'aala) kwa hisia zozote unazomuonyesha mkeo kama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyosema:

  Mmoja wenu atapata thawabu kwa chochote ambacho atafanya ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu hata kwa tonge analomlisha mkewe

  Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.

  Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'ala) daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.
  Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake.

  Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

  Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao

  Mwishowe, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. amilia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe “Mimi siwapendi wazazi wako”. Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, “Na wako pia siwapendi”.

  Mapenzi yasiishe na pia tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzioIngieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo Az-Zukhruf 43:70]Pia wataungana na watoto wao.

  Na mfano bora katika mintarafu hii itakuwa ni Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mapenzi yake kwa Bibi Khadiyjah, mkewe aliyeishi naye kwa miaka 25 yalisogea mpaka kwa wale aliowapenda Khadiyjah; mapenzi yake haya yaliendelea hata baada ya kufa Bibi Khadiyjah. Ilikuwa miaka mingi baada ya kifo cha Bibi Khadiyjah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumsahau na kila panapochinjwa mbuzi katika nyumba yake basi hutuma kifurushi kwa familia ya Bibi Khadijah na marafiki zake na kila akihisi kuwa mgeni anayegonga mlango ni Dada ya Khadijah aitwaye Hala, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba huku akisema,

  “Ewe Mwenyezi Mungu Jaalia awe ni Hala
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Wewe wa kwako unamuenzi?
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  swadakta mkuu jamii inajengwa kuanzia ngazi ya familia,ndoa inayoenziwa ndio chanzo cha jamii bora kutoka na kizazi bora kitakachotarajiwa kupatikana hapo.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sana tu na ndio mana tupo kwenye ndoa ya furaha kwa zaidi ya miaka kibao sasa.
   
 5. upele

  upele JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  marhabaa ustadh au ni ustadhwi weye maana kuna jamaa yangu kwa mistari ni noma ila anakuwa oposite na hiyo mistari kaka kama kuna nusra home kwenu nipatie nimekukubali
  mie ni ustadh wa uswahilini
  Conquest
   
 6. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Ok. Lakini ukweli bado upo palepale: Mkapa Mwizi!
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Waweza nyoosha maneno yako? Sijakuhisi bado!
   
 8. upele

  upele JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i mean nimekukubali kwa mistari yako kama ni ustadh kweli basi kama kuna nusra kwenu basi nijaalie
  Conquest
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Nzuri. "Wanaume ishini na wake zenu kwa akili"
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hiyo nusra unayo itaka ni PM kisha tuelezane kiundani.
   
Loading...