Muda wenu si muda wangu, mawazo yenu si mawazo yangu

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MUDA WENU SI MUDA WANGU, MAWAZO YENU SI MAWAZO YANGU

Leo 14:30hrs 17/03/2021

Basi watu wakamwambia nenda kajionyeshe kwa Walimwengu, nae akawajibu.

Yohana 7:6

Basi Yesu akawaambia,wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. YESU hakuweza kuruhusu mtu kuingilia Muda Wake!

Ndugu zangu Watanzania nipo Mlimani, zamani tulikuwa tunakwenda Mlimani kufunga na kuomba ili Mwenyezi Mungu aikomboe nchi na kuibariki, hata wakati mwingine kupokea maono juu ya mapenzi ya Mungu kwa Watanzania, Kwaresma ni kipindi cha mfungo, nasi tunapaswa kumrudia Mungu kwa sala na toba.

Sala na mfungo vinaweza kuamisha milima, sala na mfungo unaleta attention ya Mungu kwako,ni sawa na kuwakaribisha malaika waje wakuwekee kipaza sauti nawe uweze kuongea clearly moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, mahali patulivu penye uasili (nature) wanyama, ndege, miti na upepo mzuri ni mahali pazuri pa kuongea na Mungu, hivyo nipo mlimani nikiwaombea Watanzania wenzangu, kila mtu ana muda wake, lakini wa bwana ni pale anaposema sasa nenda ukajionyeshe kwa Walimwengu.

Mungu awabariki,awalinde na kuwatunza, Mungu yupo nasi, ametutetea na kutulinda dhidi ya corona hata sasa anatulinda na ataendelea kutulinda, tuendelee kumuomba Mungu na kumuamini yeye tu ndiye mlinzi wetu na mponyaji wetu. Kumbuka, maono na muujiza ni siri ya Mungu nae siri hiyo uwaonesha marafiki zake ambao ni watakatifu waliopo hapa duniani.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 
Waamuzi 14:4
....hawakujua kwamba huo ulikuwa mpango wa Mwenyezi-Mungu ambaye alikuwa anatafuta kisa cha kuchukua hatua dhidi ya Wafilisti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom