Muda sahihi wa uchumba ni upi?

Fungo N.

JF-Expert Member
May 20, 2011
252
43
Nilibahatika kuwa na m penzi tangu 2006,ambapo pia nilifaulu kuendelea na kdt 5 na baadae chuo na sasa nahitimu mwaka wa 3,wakati wote huu 2mejitahidi kuwa wapya kila mwaka na bado 2napendana.HOFU yangu ni kwamba lengo nataka 2fikie azma ya kuoana lakini naogopa kuwa tutawahi kuchokana mara baada ya kuanza maisha.Naomba ushauri
 
mh! Mtawahi kuchokana kisa mmedumu muda mrefu au unamaanisha nini? :nono:
 
Kama mtachokana mapema yote hii fikiria baada ya miaka kumi itakuaje!!Haya harakisheni ndo ili kuchokana kuje wakati mshafungwa pingu!!!
 
itabidi muendelee kujitahidi kulifanya penzi lenu upya kama mlivyokuwa mnafanya.....jiulize tu maswali,by the time unamaliza utajua kama unamuhitaji huyo kama mke au la.....manake sioni hiyo hofu ya kuchokana ina uhusiano gani na kwenda hatua nyingine kiuhusiano kama mnapendana kweli.....!
 
Hongera mpendwa hadi kufikia hapo mlipo na naomba usitangulize swala la kuchokana endelea kulifanya penz lenu liwe jipya kila kulicha na muweke mungu mbele ktk mambo yenu, kila mtu awe na upendo wa dhati kwa mwenzie na muheshimiane hakika mkifata hayo mambo hamtachokana na mda sahihi wa uchumba ni ule mda mtakaokuwa tayari wewe na mwenza wako kuanza maisha mapya na mkakubaliana
 
kuchokana kwenye ndoa kupo na ndoa inahitaji uvumilivu sana .........
pia uchumba usizidi zaidi ya miaka miwili zaidi ya hapo itakuwa ni uchumba sugu.
 
Hongera mpendwa hadi kufikia hapo mlipo na naomba usitangulize swala la kuchokana endelea kulifanya penz lenu liwe jipya kila kulicha na muweke mungu mbele ktk mambo yenu, kila mtu awe na upendo wa dhati kwa mwenzie na muheshimiane hakika mkifata hayo mambo hamtachokana na mda sahihi wa uchumba ni ule mda mtakaokuwa tayari wewe na mwenza wako kuanza maisha mapya na mkakubaliana

kama ameshaanza kuhisi watachokana mapema bc ujue yy ndo anataka kumpotezea ashamuona wa kawaida.
 
si ndo mwafahamiana uzuri, km mnaishi mbalimbali miaka hyo ni michache sn
 
Usiogope kuingia kwenye ndoa kama upo tayari kwa hilo. Kikubwa unachotakiwa kujua ni nini maana ya ndoa na kama mwana ndoa wajibu wako ni nini! Ukishajua hayo hakuna kuchokana kwenye ndoa. Kwani wewe umeshawahi kumchoka mshikaji wako? Karibu sana na All the best!
 
Mimi nadhani once you are engaged na hamna kinachowazuia kuoana why keeping all those years? Kwa sababu uchumba si mahala pa kuangaliana tabia! Unatakiwa umchunguze mtu kabla hujawa na uchumba nae kwani uchumba una involve lots of people including parents.

Na si vizuri kumchumbia mtu kama kigezo cha kumfanya awe kifungoni. Mchumbie mtu kwa kuwa uko tayari kuoa. Kuna wengi kwa sababu ya kutokujiamini akimpenda mtu tu basi mpaka kujitambulisha kwa wazazi eti nataka kuoa.

Kuna rafiki wa dadangu alikuwa na mchumba for more than 10 years. Binti yuko dar na mambo yake safi sana, jamaa yuko Tanga sijawahi kumuoan so I don't know kama alikuwa na uwezo kifedha or not. Hivi navyoadika dada ni positive. Maana alikuwa na vi affair ingawa ana mchumba, na mchumba wake sijuhi kama alikuwa ametulia au la. Maana nasikia ni yeye mwanaume ndio alikuwa mgumu kufunga ndoa.
 
kama uko tayari
funga virago anza safari

kama unadhani bado na una
duku duku fulani jipe muda

maoni yangu ni bora mtu uwe single au
partner/ bf/gf wa mtu kuliko kuingia kwenye
ndoa kiusanii...
 
Usiogope kuingia kwenye ndoa kama upo tayari kwa hilo. Kikubwa unachotakiwa kujua ni nini maana ya ndoa na kama mwana ndoa wajibu wako ni nini! Ukishajua hayo hakuna kuchokana kwenye ndoa. Kwani wewe umeshawahi kumchoka mshikaji wako? Karibu sana na All the best!

thank u stay blessed
 
Hongera mpendwa hadi kufikia hapo mlipo na naomba usitangulize swala la kuchokana endelea kulifanya penz lenu liwe jipya kila kulicha na muweke mungu mbele ktk mambo yenu, kila mtu awe na upendo wa dhati kwa mwenzie na muheshimiane hakika mkifata hayo mambo hamtachokana na mda sahihi wa uchumba ni ule mda mtakaokuwa tayari wewe na mwenza wako kuanza maisha mapya na mkakubaliana

be blessed aisha asante kwa ushauri na kunipa moyo kila laheri
 
Back
Top Bottom