Muda huu nimetoka lock up, kisa mapenzi

Muda huu nimetoka lock up, kisa mapenzi

Mpaka miaka ii watu wanapigania wanawake, wote awa, mi nikikufuma nakwambia kaioshe na mimi nitandike manake inawashwa washwa,
 
Asiyetaka kwenda mahakamani ni yy, aliyeingilia, nyumba yako ni yy.kwa vipi sasa ww uingie gharama hiyo? Wewe ulimkanya Kwa kakofi kadogo tu (ingawa kalimtoa vijno viwili) nani asiyejua uchungu wa jambo hili ? Ikizingatiwa kwamba ulikuwa unakaa pamoja na huyu mama, kama mke na mume,(hapo,tayari pana dhana ya ndoa) huyu ni dhalimu ! Afadhali ungelikata kabisa lile linanihii ! (Kama umekosa uvumilivu)
 
Wewe tena ulipe gharama?za nini?mchukue huyo mwanamke waambie akitaka ufute kesi amuoe huyo malaya wako.
 
Mapenzi kitu cha ajabu sana.Yaani unajeruhi mtu kisa pale kati tu,My brother achaga kupigania mapenzi pigania pesa,mwanamke akikusaliti move on tafuta mwingine maana utakuja kuua bure uende jela.
 
Bado mnanishauri kuoa? Imagine mabinti almost wote wasioolewa na michepuko ya waliooa! Then unataka mie nitangaze ndoa? Hapana....ngoja na mie niendelee kumega kisera,,,upumbavu huu
 
Popote ulipo agiza kitimoto kilo mbili na na ndizi sita nakuja kulipa sasa hv
 
hahaha..yani wewe jamaa nimesoma nikafurahi kuona sipo peke yangu...
bora wewe na rungu ndani..mie ndo ningepelekwa mahabusu kabisaa na huu mzigo wangu
 
Tukiwa bado tunatafakari miaka miwili ya Rais Magufuli, kuna majanga yamenikuta mwenzenu. Kwa kifupi toka Jumapili nilikua lock up, sababu kubwa ikiwa ni mapenzi yani kuna mwanamke nilidhani nimepata kumbe nimepatikana.

Mwishoni mwa week nimetoka kwenye mizunguko yangu sikumkuta ghetto, ufunguo kaacha kwa jirani na kaondoka bila kuniaga, nikasema ngoja nimuwekee mtego nione atarudi na nani na akiwa katika hali gani.

Nikamtumia text nikamwambia niko nacheck game ya man u na chelsea,so nitachelewa kurudi na nikiwahi sana basi itakua ni saa 5 usiku, muda huo huo nikaweka patrol mitaa ya pale gheto ili kumnasa adui, mara nikashangaa prado nyeupe inapark pale gheto na yule mwanamke akashuka na lijamaa flani wameshikana mikono, nikaona wamesimama na lile janaume pale muda mrefu.

Mara paa na mimi nikawaibukia pale, sikutaka kuuliza nani ni nani nikatembeza kichapo kwa wote kwa kutumia rungu langu ambalo hua nalihifadhi ndani kama silaha ya kujilinda in case nikivamiwa, yule jamaa nikamg'oa meno mawili ya mbele pale pale na ngeu za kutosha, msichana nikampiga mpaka nikamvunja mkono, tunavyoongea saivi kawekewa POP tayari, jamaa yake kashonwa nyuzi sita usoni, so police waliokua doria wakasikia zile kelele wakaja wakanikamata wakanipeleka central.

Toka Jumapili nilikua lock up, nimefunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru miili ya watu wawili kinachoendelea ni kwamba jamaa niliyembonda hataki masuala ya mahakamani ni mume wa mtu anasema anaona aibu watu wakijua kuwa nimemdunda kisa alikua na kidosho mwingine, kwa hiyo ameniomba haya mambo yaishie police tu me nilipe gharama za kufuta kesi, nimerudi gheto muda huu cha kwanza nimefika nikachukua kila kitu cha yule mwanamke na nimetia kiberiti.

Ahsanteni.
mwisho wa hii story ni upi???
 
Back
Top Bottom