Ni vema wale wote wanafikiria kuwa fedha ni kila kitu wakajifunza kwa Mubarak, yeye anasemekana ni mtu wa pili tajiri duniani, akikadiriwa kuwa na utajiri upatao dola za marekani 53 bilioni; kwa kiwango hicho cha utajiri anasemekana kumzidi Billgates mwenye utajiri wa dola za marekani 52 bilioni. Pamoja na utajiri huo, hivi sasa mguu wake mmoja huko uraiani na mwingine jera.