Mubarak anafuata ya waMisri au waMarekani?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Kabla Mubarak hajatoa hotuba yake, tayari vyombo vya habari vilikwishatangaza kwamba Obama amemwambia atangaze kutokugombea urais Septemba 2011. Siku chache zilizopita walionekana Kama kusema Mubarak andoke madarakani kabla ya Ushawishi wa Israel.

Madai ya wananchi ni moja tu muda wote huu, kwamba Mubarak ajiuzulu mara moja. Sauti hii ya wananchi inaonekana haipendwi na marekani ambao ndio wanaoamua Mubarak afanye nini. Do people matter?

Kama hii ndiyo demokrasia, nadhani tutafakari zaidi, pengine ndiyo maana kila tukipiga kura matokeo yanakuwa tofauti na matarajio ya wapiga kura.
 
Mubarak ni kibaraka wa america na ndio wanaompa jeur mpaka sasa,wanamuunga mkono,ila ataondoka madarakani kwa nguvu ya umma.
 
Marekani wanatoa msaada mkubwa wa kijeshi kwa Misri pia kumbuka kuwa pia Misri ni kibaraka mkubwa mno wa Marekani linapokuja suala la mgogoro wa middle east na ndio maana Marekani hawataki kikundi cha Muslim Brotherhood kichukue hatamu ya nchi maana wale one of their targeted mission ni Israel wanataka kuhakikisha they bring down that nation
 
Mubarak ni kibaraka wa america na ndio wanaompa jeur mpaka sasa,wanamuunga mkono,ila ataondoka madarakani kwa nguvu ya umma.
Kuna watawala hasa hawa wa Bara la Afrika yaani mambo yameishaharibika lakini yeye bado anaona kuwa hali ni shwari tu na anaendelea kuongoza nchi yaani mtu umekaa madarakani miaka 30 lakini bado haujatosheka kiasi kwamba unataka kurithisha na watoto wako sasa
 
Nilimsikia Museveni akihojiwa na BBC akadai anagombea tena kwa sababu kazi aliyoianza ya kuimarisha uchumi wa Uganda ndiyo kwanza inaanza hasa baada ya kuvumbua mafuta!!
 
Nilimsikia Museveni akihojiwa na BBC akadai anagombea tena kwa sababu kazi aliyoianza ya kuimarisha uchumi wa Uganda ndiyo kwanza inaanza hasa baada ya kuvumbua mafuta!!

Museven, aliahidi kuwa kaingia nguvu ya kijeshi na atatolewa labda kwa nguvu za kijeshi lakini haachi ngazi hadi kufa. Sasa naona waUganda wanahaja kabisa ya kutumia njia ya wa Misri kama hawaridhiki na utawala wake, lakini kama bado wanamuhitaji wamuache. Aliita yeye ni kama kota-pini ya baiskeli; inaingizwa kwa kugongwa na inatolewa kwa kugongwa. Viongozi wa Afrika wote ni waroho wa madaraka na ndio maana wanadiriki hata kuiba kufa ili waendelee kuwepo madarakani. That's so sad!
 
Marekani wanatoa msaada mkubwa wa kijeshi kwa Misri pia kumbuka kuwa pia Misri ni kibaraka mkubwa mno wa Marekani linapokuja suala la mgogoro wa middle east na ndio maana Marekani hawataki kikundi cha Muslim Brotherhood kichukue hatamu ya nchi maana wale one of their targeted mission ni Israel wanataka kuhakikisha they bring down that nation

There personal interest between American and Hosni Mubarak! ndio maana sikumshangaa pale Obama alivyokua anaongea na waandishi wa habari kua eti waliongea kwenye simu na Mubarak kuhusu Blablabla Bul ***shit tutaendelea kunyanyasika mpaka lini sisi waafrika tutoke kwa hawa MABWANYEYE?
 
Back
Top Bottom