Mubage Rais wa Zimbagwe ni Rahis Msahaulifu kuliko wote Duniani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,534
24,083
kulikuwa na mkutano wa Marais ulikuwa unafanyika Huko New Work Marekain. Marais wote walikuwepo na kila rais alitoa ushuhuda namna gani dawa ya kuondoa usahaulifu imemsaidia baada ya kuwa wengi walikunywa dawa hiyo na kukutana kutoa ushuhuda.

MC. tunakuomba raisi wa Tanzamania usimame utupe ushuhuda wako baada ya kunywa dawa hii.
1. RAIS WA TANZMANIA.nashukuru sana, aisee mimi nilikuwa msahaulifu sana. kiukweli nimepata madaraka ya kuwa rais hata sikuwah kukumbuka ahadi zangu kwenye kampeni zilikuwa ni nini. basi nikawa nazunguka tu dunia nzima kuuliza nchi mbalimbali kuwa nliahidi nini kwenye kampeni zangu wanikumbushe.kutaamaki miaka 10 imekatika. mi nikawa nadhani ndo mitano.wakanikumbusha kuwa ni kumi hivyo nimpishe mwingine. toka nimekunywa dawa sasa nakumbuka kabisa kwa mfano nakumbuka nimekuja hapa new work zaidi ya mara 200 kutembea. hii dawa ni nzuri kwa kweli.

MC. tunakuomba raisi wa Penya usimame utupe ushuhuda wako baada ya kunywa dawa hii.

2. RAIS WA PENYA. Mimi nlikuwa msahaulifu mpaka nilishasahu mara kadhaa nikasema Mlima kilimanyaro upo kwetu kumbe ni kwa jirani zetu.wazungu wengi walikuja kwetu wakiamini upo kwetu.nimemeza hii dawa imenikumbusha hata tanzmanite huwa tunasema ni yetu kumbe tunakosea si yetu ila inapatikana kwetu

MC. tunakuomba raisi wa Zimbagwe usimame utupe ushuhuda wako baada ya kunywa dawa hii.

3. RAIS WA ZIMBAGWE : kiukweli sijui hapa nipo wapi na nafanya nini. nani kanileta hapa? ninyi wabunge wote mlioko humu bungeni naona mna mtizama mke wangu kwa macho makali sana. sasa naamuru wote mtolewe nje na pia mimi na mke wangu huyu hapa tulale (akimshika rais Musaba wa Ugando.

MC. naomba tuharishe kwa muda kidogo..............................................................................
 
Huyo wa tanzania ni mzee wa Msoga. Angesimamishwa Ngosha angesemaje?
 
Back
Top Bottom