Muamini Mungu kila jambo anaweza(story)

Muamini Mungu kila jambo anaweza(story)

Wewe si unamwamini mungu? Makubwa sana uliyoweza kuyafanya mpaka hivi sasa ni yepi?

Umevurugwa.si bure...kher uamin yupo siku ikifika usimkute...but sio ukatae hayupo alafu ukamkute...mmh
 
tangu nihitimu chuo ni mwaka wa tatu sasa, na nimekuwa nikihangaika kupata ajira bila matuaini na kuishia kufanya vibarua ambavyo bado havikuweza kukidhi mahitaji ya familia yetu na wadogo zangu wawili wanaosoma shule ya sekondari pamoja na mama yetu ambaye ni mgonjwa.
baba alifariki na mama ni wa makamo na amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kuathiri afya yake jambo ambalo mpaka sasa limemfanya ashindwe kuwa msaada kwetu na kututegemea sisi hasa mimi.
ilinibidi nije mjini ili kuweza kupata koneksheni za kazi jambo ambalo liliishia kuwa gumu na la kukatisha tamaa kwa miaka yangu yote miliwi niliyokaa hapa dar. Hebu fikiria huna kazi lakini unatakiwa kumsaidia mama apate dawa na wadogo waende shule vyema(yahitaji ujasiri na kujituma sana).
sikuwa na jinsi zaidi ya mimi kumtegemea rafiki yangu ambaye yeye alibahatika kupata kazi na akawa akinipa msaada mkubwa sana. Wiki iliyopita nilimwambia adhma yangu ya kurudi nyumbani kuwa karibu na familia lakini moyoni lengo lilikuwa kurudi kijijini na kujikita katika kilimo na kazi za kujitolea kwani niliona nakuwa mzigo kwake kwani nami nilitaka nimpe nafasi ajijenge. Kiukweli alinikatalia na kunisihi nibaki ila mimi moyoni nikawa nilishamaanisha.
juzi usiku nilijifungia chumbani mwangu na kumwambia mungu wangu,” eeh mungu, wajua mahitaji yangu na wakati mgumu nilio na unaona jinsi nilivyohangaika. Sasa nimeamua kurudi nyumbani,ila naomba uwe upande wangu na kumsaidia mama na wadogo zangu wapate matunzo, kwani wewe ndiwe mtunzaji mkuu”
baada ya salahii nililala, jana nilipigiwa simu na shirika moja la kimataifa ambalo niliomba kazi miezi miwili iliyopita na wakanifanyia usaili na kuniruhusu niondoke. Leo asubuhi nikaitwa na nilipofika pale nikapewa barua ya kuitwa kazini.
wakati nikiwa bado na mshangao nikaona katika mambo makuu nitakayopewa ni bima ya afya ambapo sasa naamini mama atapata matibabu kwani naruhusiwa kuwaweka watu wanaonitegemea wa umri wowote wasio zidi wanne.pia sasa kwa mshahara huu mkubwa nitakaoanza kuupokea naamini wadogo zangu watamaliza elimu yao bila shida.
mungu ni mwema na hamtupi mtu anayemtegemea na kumwita nakati za shida au raha.
asante


nimeikuta sehemu hii hakika nimeipenda, mungu anatutoa mbali, ni wakati wa kumshukuru, na kumsifia

daima mungu hamtupi kijakazi wake
 
hee hongera sana besti ila endelea kumwammini Mungu anaweza yote halafu mtegemee usitegemee akili zako na tena usianze kutapanya hela oovyo ukashindwa kumtibia mama yako na kuwasomesha wadogo zako tambua kuwa wako wale wanyang'anyi watakukomba zote kisha nawe ubaki mtupu halafu kumbuka fadhila za huyo rafiki yako aliyekufadhili bila yeye usingeweza kuwapo hongera jipe nguvu
Tangu nihitimu chuo ni mwaka wa tatu sasa, na nimekuwa nikihangaika kupata ajira bila matuaini na kuishia kufanya vibarua ambavyo bado havikuweza kukidhi mahitaji ya familia yetu na wadogo zangu wawili wanaosoma shule ya sekondari pamoja na mama yetu ambaye ni mgonjwa.
Baba alifariki na mama ni wa makamo na amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kuathiri afya yake jambo ambalo mpaka sasa limemfanya ashindwe kuwa msaada kwetu na kututegemea sisi hasa mimi.
Ilinibidi nije mjini ili kuweza kupata koneksheni za kazi jambo ambalo liliishia kuwa gumu na la kukatisha tamaa kwa miaka yangu yote miliwi niliyokaa hapa dar. Hebu fikiria huna kazi lakini unatakiwa kumsaidia mama apate dawa na wadogo waende shule vyema(Yahitaji ujasiri na kujituma sana).
Sikuwa na jinsi zaidi ya mimi kumtegemea rafiki yangu ambaye yeye alibahatika kupata kazi na akawa akinipa msaada mkubwa sana. Wiki iliyopita nilimwambia adhma yangu ya kurudi nyumbani kuwa karibu na familia lakini moyoni lengo lilikuwa kurudi kijijini na kujikita katika kilimo na kazi za kujitolea kwani niliona nakuwa mzigo kwake kwani nami nilitaka nimpe nafasi ajijenge. Kiukweli alinikatalia na kunisihi nibaki ila mimi moyoni nikawa nilishamaanisha.
Juzi usiku nilijifungia chumbani mwangu na kumwambia MUNGU wangu,” Eeh MUNGU, wajua mahitaji yangu na wakati mgumu nilio na unaona jinsi nilivyohangaika. Sasa nimeamua kurudi nyumbani,ila naomba uwe upande wangu na kumsaidia mama na wadogo zangu wapate matunzo, kwani wewe ndiwe mtunzaji mkuu”
Baada ya salahii nililala, jana nilipigiwa simu na shirika moja la kimataifa ambalo niliomba kazi miezi miwili iliyopita na wakanifanyia usaili na kuniruhusu niondoke. Leo asubuhi nikaitwa na nilipofika pale nikapewa barua ya kuitwa kazini.
Wakati nikiwa bado na mshangao nikaona katika mambo makuu nitakayopewa ni bima ya afya ambapo sasa naamini mama atapata matibabu kwani naruhusiwa kuwaweka watu wanaonitegemea wa umri wowote wasio zidi wanne.Pia sasa kwa mshahara huu mkubwa nitakaoanza kuupokea naamini wadogo zangu watamaliza elimu yao bila shida.
MUNGU ni mwema na hamtupi mtu anayemtegemea na kumwita nakati za shida au raha.
Asante


NIMEIKUTA SEHEMU HII HAKIKA NIMEIPENDA, MUNGU ANATUTOA MBALI, NI WAKATI WA KUMSHUKURU, NA KUMSIFIA
 
Hayo ndo miujiza ya MwenyeEzzi Mungu !! Ukarimu wake hujaga unapokuwa wewe mwenyewe upo serious, myenyekevu kwake na mkweli....
Good Luck and god Blessings.
 
Aisee!!!!!!! Kuna watu nilikuwa nawachukulia vivyo sivyo! Nways
God is good.I love I trust n forever i will
 
NYANI NGABU,wewe ni mjanja kuliko MUNGU,umeshinda,subiri matokeo na marks za ushindi wako!
 
Aisee!!!!!!! Kuna watu nilikuwa nawachukulia vivyo sivyo! Nways
God is good.I love I trust n forever i will

Kuna watu ni mashetani aisee...si unajua shetani yuko kila sehemu...wamefungua na id mpk jf
 
Napenda pale nnapojikumbusha kuwa "HAWAI WALA HACHELEWI ILA ANAJIBU KWA WAKATI" Lakini neno USIOGOPE kwenye Biblia limeonekana zaidi ya mara 250 hivyo kutupa sisi mwanga wa kulisoma kila baada ya page 7 kwa wale wasomaji wazuri Hivyo hatupaswi KUKATA TAMAA "Yupo aulindaye mji" Jina la Bwana Litukuzwe sana.
 
Mara zote Mungu huonekana pale tunapofika mwisho wa akili zetu za kibinadamu. Nilishawahi kuwa katika kipindi kigumu na wakati huo nilkuwa ni sha oa na ndo nina mtoto bado mdogo sana, nilikuwa nakwenda kanisani wakati wa asubuhi na kulia sana mbele za Mungu, Mungu alikuja kujitokeza kwangu kwa namna ya ajabu sana.

Mara zote huwa nikikaa na kutafakari naona ukuu wa Mungu, nikiangalia uwezo nilionao na afya njema niliyo nayo.

Ebenezer- Angela Chibalonza - YouTube
 
Pole mdogo wangu kwa wakati mgumu na hongera kwa kazi uliyopata. Fanya kazi kwa kujituma, waheshimu watu wote bila kujali cheo na usiache kutoa fungu la kumi kwa muumba wako...
 
Ooooh Glory to Almighty God.

Thus why the bibble states that
"INSTEAD OF THEIR SHAME, MY PEOPLE WILL RECEIVE DOUBLE PORTION"
(Badala ya aibu yao watu wangu watakwenda kupokea maradufu)

Sifa na utukufu ni kwake Yahwe Mungu wa Israel aliye hai.
 
Back
Top Bottom