Muamala wanipatia mke

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Nikiwa nimekaa nakutafakari ni vipi siku itakwenda kwani sikuwa na chochote mfukoni na kama ujuavyo tumbo lenyewe lilitakiwa lipate stahiki zake pasipo kuangalia ni nini unapitia. Wakati bado nipo kwenye tafakuri zito juu ya nani nitampiga mzinga kwa siku hiyo ili mkono uende kinywani na njia ya chooni isiote nyasi. Ghalfa nilitolewa kwenye lindi hilo la mawazo na mtetemo wa simu yangu ulioashiria kuingia meseji. Ilinilazimu kuacha kila kitu kwa wasaa huo na kutoa simu yangu kutazama ni nani alitumia meseji hiyo. Kiuvivu zaidi nilitoa simu mfukoni na kubonyeza kitufe ambacho kiliwezesha simu kuwaka na baada ya kuwaka tu nilikutana na muamala ambao ulikuwa kama laki na nusu (150,000).

Macho yalinitoka utafikiri natafuta hela niliyopoteza baada ya kutumwa mafuta dukani. Niliifungua ili nipate uhakika zaidi na kukuta kweli ni fedha taslimu imeingia kwenye simu yangu huku jina la aliyeituma ile pesa likisomeka Jenipher Joseph. Huu ndio ulikuwa mshangao wangu kwani sikuwahi kuwa na mahusiano ya aina yoyote yale na jina hili.

Lakini kilichonipa matumaini ni kuwa watu hutumia vitambulisho vya wengine kusajilia laini zao. Hoja hii ilikuwa na mashiko lakini bado haikuniingia akilini kuwa laki na nusu itumwe kwangu bila makubaliano yoyote yale na kwa kipindi hiko sikuwa na rafiki hata mmoja ambaye alikuwa anaweza kufanya hichi kitu zaidi ya kunitumia fedha za kula nazo zilikuwa chini ya elfu hamsini.

Kuingia kwa laki na nusu na bila kuwa na makubaliano na yoyote yule kuhusu kutumwa kwa hela hiyo kulinifanya niweze kusita kuitoa huku nikijipa matumaini kuwa aliyeituma lazima atanipigia kunipa taarifa labda hapo naweza kujua kazi ya hela hiyo ni nini.

Njaa yote iliisha huku mawazo wakishambulia akili yangu kwa kasi ya 5G kwani nilikuwa na machaguzi mawili niitoe niile au nisubilie aliye ituma anipigie simu. Wakati wote huo sikuwa na mawazo kuwa kuna mtu atakuwa amekosea na nimuhimu sana kwake hiyo hela. Nilijipa wasaa wa kusubiri ili nijipe uhakika zaidi na kweli hazikupita hata dakika kumi na tano simu yangu ilianza kutoa mtetemo.

Mtetemo huo sio kama wa mara ya kwanza kwani huu uliashiria kuwa mtu anapiga simu. Kivivu tena nilitoa simu yangu mfukoni na kutazama ni nani ambaye alikuwa akipiga. Nilikuta namba ambayo haikuwa kwenye hifadhi ya namba nilizokuwa nazo na ilikuwa ngeni machoni mwangu. Ila kulikuwa na kahisia ka kuwa namba hii ndio ilikuwa yenye muamala kwa sababu ziliwiana namba za mwisho lakini sikuwa na uhakika sana hivyo nilipokea ili kujipa uhakika.

Baada ya kupokea niliweka sikioni na nilinyamaza kwa sekunde kadhaa kusikiliza aliyepiga alikuwa ni nani? Baada ya ukimya huo niliyafungua mazungumzo kwani na upande wa pili nao ulikuwa kimya kusubiri niongee mimi. Kwa utulivu kabisa nilisema "haloo" upande wa pili ukajibu huku ukionesha hauna utivu ndani yake "samahani kaka nimekosea kutuma hela na imekuja kwako hela hiyo ilikuwa ya mdogo wangu ambaye yupo shule. Nilikuwa naomba kama kuna uwezekano unirudishea hata laki hiyo nyingine chukua".

Baada ya maongezi haya kutoka upande wa pili tena yakiwa ya mfululizo yaliisha na kunipa nafasi ya kuongea na mimi nilisema machache sana kuwa "nakurudishia hela yako yote dada wala usijari". Wakati huo nilikata simu huku nikianza utaratibu wa kurudisha ile hela tena ikiwa kama ilivyokuja. Hamasiko hili sijui lilitoka wapi lakini nadhani ni kwa sababu ya imani niliyokuwa nayo juu ya kitu chochote kisichokuwa cha kwangu sipasi kuwa nacho.

Nilipokwisha kufanya mpango niliweza kurudisha muamala huo kama ulivyokuwa na nikabaki nikiwa na njaa yangu huku nayo sasa ikishambulia kwa kasi nadhani ilipanga kunikomesha kwa kujifanya mjanja. Nilipokea tena simu yake ikiwa imepita dakika kumi tangu nitume ile pesa na sasa ilikuwa kwenye utulivu na hapa ndipo niligundua kuwa sauti ile ilikuwa nzuri sana masikioni mwangu.

Alinipongeza kwa ukarimu wangu huku akiniuliza maswali kadhaa ambayo niliyajibu vyema na katika maswali hayo moja ambalo lilikuwa la umuhimu ni kuwa napatikana wapi? Mimi nilimjibu kuwa napatikana Mwanza mtaa wa Uhuru. Baada ya maelekezo hayo aliniambia pia yeye yupo Mwanza lakini makazi yake yako Nyegezi. Kwa kuhitimisha akaniambia kuwa itakuwa vyema siku ambayo nitakuwa sina kazi tuonane.

Kila kitu kilikuwa vyema kuanzia siku ya kwanza tunawasiliana baada ya kukutanushwa na muamala. Ukaribu wetu uliongezeka kwa ghalfa kama unyeshaji wa mvua wakati wa masika. Hatukupitisha siku bila kuwasiliana kujuliana hali ikiwa mimi sijampigia basi yeye alikuwa na jukumu la kunipigia au hata kutuma ujumbe mfupi. Haya yote yalinogesha zaidi urafiki wetu na kutufanya tuwe karibu zaidi na unafahamu urafiki ukisogea karibu mapenzi yanazaliwa na ndio ilikuwa hivyo.

Taratibu mapenzi yakaanza ndani yetu na kwa kuwa kila mmoja alikuwa hana pingamizi kwa mwenzake basi tuliingia kwenye mapenzi na baadae tukaingia kwenye uchumba kisha tukakamilisha na ndoa. Mpaka leo uwa nashukuru hawa walivumbua hela ya mtandaoni (digital money) kwani bila wao pengine nisingekuwa na mke. Asanteni!
 
utakujaga kuzolewa kizembe



mimi wki lililopita nilikuwa tyt kipesa nawaza na kuwazua ghafla msg ya NMB inanitaarifu pes a imeingia laki tatu na nusu.

sikushughulika na msg hiyo maana walisema kwenye ac inayoishia na ooo (mfano tu) na wakat hyo ac sina.

wiki limepita et msg ikaja ya NMB nimetoa ile laki tatu wakati hata sijahangaika nkajisemea hili ni tego zito wamefeli.


so be carefully man.
 
Back
Top Bottom