muaji sehemu ya 4

muaji sehemu ya 4

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
Hii story inaanzia hapa Wakala wa kifo alivyowatesa polisi katika kesi ya aina yake

Kisa na mkasa cha mauaji ya William na Lilian.


Mwezi wa 8 mwaka 2003, Yung alikuwa hana makazi ya kuishi baada ya kugombana na aliyekuwa mpenzi wake na kufukuzwa kwenye nyumba. Yung alikuwa akiishi Kusini mwa Jiji la Florida na alikuwa akijihusisha na udokozi wa vitu mbalimbali. Kutokana na kutokuwa na makazi alikuwa akilala kwenye eneo la kupumzika kwenye bustani zilizoko Fort Lauderdale.

Siku moja akiwa amelala kwenye benchi asubuhi mara anaamshwa na mtu na mtu huyo siyo mwingine bali ni Henry Jones. Jones anamwambia kuwa anweza kumwita Badman hvyo hakumtajia jina lake halisi na anamwambia kuwa kuna sehemu anataka amsindikize akaonane na wazee flani kasha atamsaidiakuendesha gari atakalonunua hapo baadae kwa malipo. Kwakuwa Yung ahakuwa na sehemu ya kulala wala pesa hakuweza kukataa hiyo kazi. Hivyo yeye na Jones wanaingia kwenye gari dogo jeupe aina ya Ford lililokuwa likimilikiwa na Jones na kuongozana. Wanazunguka wote siku nzima na kulala wkenye hilo gari mpaka alfajiri ambapo wanaanza tena safari na mara hii wanaelekea Barlette Tennessee ambapo Jones anamwambia Yung kuwa anaenda kutembelea familia yake inayoishi huko.

Jones anaendesha gari mpaka nyumbani kwa William James, ambapo wanamkuta kaka nje kwenye kiti chake. Wanapofika a kuteremka Yung, anaona Jones na William wanasalimia kama watu wanaofahamiana sana na Jones anamwita William Papa. Jambo ambalo Yung hakujua ni kwamba Jones aliwahi kuishi Barlette na aliweza kufahamiana na William kipindi hicho.

Jones na William wanaanzisha mazungumzo huku Yung akiwa amesimama pembeni na hakuwa na shaka kuwa walikuwa ni familia moja, wakati wakiendelea kuzungumza William anamuomba Yung amsaidie kuingiza mashine ya kusukuma maji sehemu ya kuhifadhia vitu iliyokuwa upande wa pili wa nyumba yake na Yung anaibeba na kuondoka nayo kuelekea huko. Kumbe jones kutokana na ukweli kwamba aliwafahamu vizuri William na Lilian, alijua kuwa uwa wanakaa na ela ndani na aliona ni rahisi kwake kuwavamia na kuwaibia pesa yao.

William alimkaribisha Jones ndani ya nyumba kwa ajili ya mazungumzo zaidi, na Yung anadai aliporudi hakuwakuta pale nje, ila anaona mlango wa mbele wa nyumba ukiwa wazi na kuamua kuingia ndani na ndipo anamkuta Jones akiwa anamfunga kamba miguu na mikono mwanamama mtu mzima ambaye ndiye Lilian. Baada ya kumfunga anamuona Jones akimvua huyo mama heleni na pete yake na kuviweka kwenye mfuko wa suruali lake. Jones anaanza kumhoji Lilian amwambie ni wapi pesa ilikohifadhiwa, na Lilian anamjibu kuwa hawana pesa yoyote.

Jones anamuona Yung akiwa kasimama ukumbini akishangaa anamuita na kumwamuru akae pale na hakikishe Lilian hatoroki kasha yeye anaelekea upande wa kuhifadhia magari. Akiwa pale na lIlian, Lilian anamuuliza Yung unahisi atatuua? Yung anamjibu mbona yeye haelewi kwani Jones si mtoto wao, na Lilian anamjibu hapana wala yeye hajawahi kumuona ndiyo mara yake ya kwanza kumuona pale.

Wakiwa pale wanasikia sauti za William zikitokea sehemu ya kuhifadhia magari na sauti hizo zinaashiria kuwa Jones anamuua William kwa kumkata koromeo maana William alikuwa akitoa sauti za kukoroma. Jones anarudi akiwa kashikilia kisu chenye damu na kitambaa ambacho alikuwa akikutumia kupangusa damu iliyokuwa kwenye kile kisu. Anamwabia Lilian usinifanye nikakuuliza tena niambie wapi pesa iliko. Lilian anamjibu iko ghorofani, Jones anamnyanyua Lilian na kuondoka naye kwenda ghorofani ambako kulikuwa kuna chumba chao cha kulala huku akimuamuru Yung awafuate nyuma. Wanapofika chumbani Jones anachukua pesa kasha anachukua kamba na kumkaba Lilian na wakati huo anamkata shiko nusu kicha kitengane na kiwliwili wakati huo wote Yung anashuhudia.

Wakati wakitoka nje ya nyumba Yung alipita karibu na mlango wa kuingia sehemu ya kuegesha magari na hapo ndipo aliona mwili wa William ukiwa umelala chini kwenye dimbwi la damu. Wanaingia kwenye gari la Jones na kuondoka na wakiwa njiani Jones anamkabithi Yung dola 1500 alizoiba kwenye ile nyumba na kuwammbia huo ndiyo mgao wako sasa fungua mdomo wako kwa mtu yoyote juu ya kilichotokea na wewe utapatwa kama kilichowapate watu wale.

Wakiwa njiani kurudi Florida, Jones anasimama kwenye eneo la kuuza magari hapo Mississippi ambapo Jones ananunua gari la Ford toleo la miaka ya 90 kisha anamuamuru Yung aendeshe gari lake jeupe kuelekea Florida yeye anaamua kuendesha gari alilonunua. Kwa maelezo ya Yung alikuwa akiendesha hovyo hovyo makusudi kwa lengo la kuwavutia polisi ili wamkamate awekwe ndani maana ndiyo njia pekee ambayo aliona ingemsaidia kumkimbia Jones, ila mara zote walikuwa wakimpiga faini na kumwachia mpaka alipokutana na Kachero Carlos.

Alidai kwamba Carlos alipomsimamisha na kumkamata alifarijika sana maana alijua afadhali hapo kafanikiwa kumkimbia Jones ambaye alikuwa anahisi kuwa naweza kumuua hapo mbeleni. Hapo makachero walipata mwanga na kuwa na hakika zaidi kuwa mtu wao ni Jones hivyo walimaliza mahojiano na kuondoka pale kituoni.

Bonyeza Link hapo chini subiri sekunde tano kisha bonyeza next kuendelea kusoma sehemu inyaofuata
Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st
 
Back
Top Bottom