Muafaka wa CUF na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muafaka wa CUF na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 12, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Waungwana,

  Kenya matatizo yao yalitotokea katika uchaguzi wa Dec, 2007 waliweza kuyamaliza kwa muafaka na kuunda serikali ya mseto. Zimbabwe matatizo kati ya vyama vya ZANU-PF na MDC yamemalizwa kwa muafaka na kukubaliana kuundwa serikali ya mseto. Je, huu muafaka wa CUF na CCM utafikiwa lini? JMK yuko serious kweli kuona muafaka huo unafikiwa au ni anafanya usanii wa kuchelewesha muafaka huo usifanyike mpaka hapo baada ya uchaguzi wa 2010?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa ufupi hakuna mseto Zenj... Hata CUF wanajua hilo... Labda 2010 lakini kwa sasa ni dana dana tu na wala si usanii wa JK
   
  Last edited: Sep 12, 2008
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na CUF hawautaki mseto ndio maana wameondoka mezani na hawatorudi tena ,kwani walipopahitajia wamepapata ,si mnaona CCM ndio wanaokwenda mbio kutaka kuwarudisha kwenye meza ,hivi Jeuri ya CCM imekwenda wapi ,naomba mjiulize kwa nini kwa wakati huu tulio nao only CCM ndio wanaosikika kupiga makelele eti warudi mezani kuendeleza pale walipo ishia ,hivi walisahau kama mazungumzo yalikwisha kufungwa na waraka wa yaliokubaliwa kusomewa wananchi kwenye mikutano.
  Ila hapa CCM Tanganyika wanataka kupindisha mambo yanayohusu Taifa (Zanzibar ni nchi au si Nchi) ,wanataka kutumia mambo ya muafaka kuwagawa tena Wazanzibari baada ya kuona wameungana kudai uhuru wa nchi yao kutoka kwa mkloni Tanganyika.
   
 4. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zimbabwe kweli kulikuwa na tatizo na lilihitaji suluhisho kama lililopatikana. Halikadhalika Kenya. Lakini Zanzibar hakuna tatizo kama hilo. Si umeona kuwa kama wao wanaelewana (hoja ya Bango la Zanzibar ni Nchi au si Nchi). Wao wa CUF na CCM hawahitaji suluhisho kama la Zimbabwe, Kwanza hakuna matatizo kule isipokuwa matatizo ni ya kupangwa. Wewe ( na wenzako wengine wa Tanzania Bara)wala wasikushughulisheni hao.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna mseto wa mchele na kokoto ( Salmin Amour - Komandoo )
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si kweli kuwa CUF hawataki Muafaka, CUF wanahitajia Muafaka leo kabla ya kesho ila wasichokitaka ni ile nyongeza ya kura za maoni iliyokuwa haipo hapo awali. Hata kwenye hotuba ya Muungwana bungeni alieleza kuwa mazungumzo yalikwisha ulibaki utiwaji saini na utekelezaji na huo ndio msisitizo wa CUF na sio kuongeza vipengele vingine kwenye yaliyoafikiwa.

  Napenda watu wajue kuwa CCM iliipiku CUF kuhusu Muafaka III ilipokutana kule BUTIAMA. Tulishuhudia maazimia mengi (Maazimio ya Butiama) kama kukumbatia mafisadi kwenye Chama na hili la kukusanya maoni ya wananchi kama wanataka Serikali ya mseto au ya choroko! CCM wameshindwa kusoma alama za nyakati au labda wanataka yatokee maafa mengine makubwa kuliko ya Jan 26/26 2001 ndio waweze kushinikizwa na mataifa makubwa kuingia kwenye Serikali ya Kitaifa!

  Angalizo:

  Kwa kutathimini siasa ya Tanzania inaonekana mwenye hati miliki ya kutawala nchi ni CCM peke yake. Hii imethibitishwa na matukio mengi hasa chaguzi za zanzibar tangu 1995,2000 na 2005 wao wanasema huwa wanachukua wanaweka waa!
  Wamesha wahi kusema kwenye baraza la wawakilishi wao walifanya mapinduzi nchi waliiipata kwa kumwaga damu hawataweza kuitoa kwa njia ya karasi (kura)
  Mhe Karume jr aliwahi kunukuliwa kwenye kampeni za mwaka 2005 akisema hata kama wazanzibar wote wakipigia kura CUF kura yake na ya mkewe tu zinatosha kuwaingiza ikulu. Pia akaenda mbali kidogo akasema ikiwa CUF watachukua nchi watatumia mapanga na silaha walizotumia Jan 24 1964 kwani wanazo wamezihifadhi. Kwa maana hiyo hawatakubali kuachia madaraka hata ikiwezekana kuua raia wasio na hatia ili muradi wabakie na ulwa wa madaraka! Kwa angalizo hilo Muafaka ni sawa na ndoto ya mchana ni sawa na kufungua macho usiku wa giza, ni sawa n a kukamua jiwe litoke samli! au kukamua chuma kitoke maji kama hayo yanawezekana basi na Muafaka Zanzibar utawezekana.

  Wasalaam
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Napingana na wewe mkuu kusema kuwa Zanzibar hakuna matatizo labda wewe unatoka sayari nyingine au ni mmoja wa makada wa CCM mliosomea chuo cha propaganda pale magogoni unataka kutueleza hujawahi kusikia watu waliuliwa kwa risasi za moto kule unguja na pemba tarehe 26 na 27 Jan 2001? Serikali wanasema waliuliwa watu 21 duru huru zinasema watu 51 na tupige hesabu! Wakati wanauliwa watu 21 Zanzibar pupulation iluwa ni watu 750,000.

  Kenya ina watu milioni 40 waliouwawa ni 1000 tunawaomba wajuzi wa mahesabu wakokotoe watupe ratio ya pupulation hizo mbili tujue wapi matatizo yalikuwa ni makubwa zaidi. Kwa uelewa wangu mdogo watu 21 kenye population ya watu laki saba na nusu ni wengi sana kuuliwa kuliko watu milioni moja kwenye population ya watu milioni 40 !

  Unaposema zanzibar hakuna matatizo sijajua una maana gani! au unataka yatokee makubwa kuliko ya 2001?ndio ujue kuwa kuna matatizo? tafadhali tueleze tukuelewe Mkuu Ndivyo ilivyo.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Siasa za Zenj zimejaa vijembe na hasa wakati wa kampeni... lolote linawezwa kusemwa ili mradi kubeza upande wa ushindani na kufurahisha umati kama si kuuvuta. CUF na CCM wanajuana vizuri na inapofika wakati wa kurushiana vijembe mengi husemwa kiasi cha kuweza kumshangaza mtu asie kuwa na ufahamu wa vijembe hivyo...
   
 10. C

  Chuma JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  JK anatakiwa achukue maamuzi mazito....JK ajue si kila mara anaweza kuwafurahisha watu wote....CCM seniors hawataki Mabadiliko ndani ya ZNZ, watafanya kila Hila ili JK asifanikiwe kuleta Suluhu ya Kwel ZNZ.....

  kitu kibaya ni kuwa tuna utamaduni wa kupinga Maendeleo yetu kisa tu, CREDITS zitakwenda kwa yule aliefanikisha hayo maendeleo...Ukiangalia Miradi Mingi tu Hupingwa au hucheleweshwa on the same reasons...Japo hii sababu huwa haisemwi!!!
   
 11. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesema matatizo yaliyopo ni yale ya kupangwa (au kutengenezwa makusudi ili yaonekane yapo). Haya si aina ya matatizo ambayo unaweza kuyafananisha na matatizo halisi kama yale ya Kenya au Zimbabwe.
   
 12. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wajameni
  unajuwa Zanzibar walipindua na walimwaga damu kweli, halafu wameitowa kwa karatasi tena baada ya mapinduzi tu na sasa wana serikali ya eneo, sasa wanasema nini? tumeichukuwa kwa mlango wa nyuma bila ya wao kujuwa, kelele za mlango humstarehesha mwenye nyumba kwani mwizi akija utasikia mlango unalia
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  ^^ Yakhe upo ndotoni?
   
 14. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sasa niambie hiyo serekali ipi mliyonayo? kama serikali ya mapinduzi hata chama cha mapinduzi jee na hiki chenu pia?
   
 15. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  naona Wazenj wapo usingizini wala hawaamki na wakiamka game ishageuzwa, lete maneno kibunango kwasasa ndio kwisha hebu niambie wale waliopindua wanatoka wapi ? na wapo wapi nyinyi mnapiga kelele tu kama kuna kura ya maoni basi two third ni watanzania wanaoishi zenj sasa mlie
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu maneno ya Karume hayakuwa vijembe. Nilikuwepo pale Chwaka siku alipotoa kauli ya kuwa silaha za mapi9nduzi bado zipo na zikihitajika zinaweza kutumika. Nilipomuangalia wakati anazungumza maneno hayo mazito, hakuonyesha kama anazungumza kisiasa.
  Nilikuwepo pia Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, yaliyotokea yalithibitisha yale Karume aliyoyasema siku ile
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Siasa ya Zenj sivyo kabisa unavyozania, ipo tofauti sana na mtazamo wako ambao nimeuona katika bandiko hili. Kumbuka kuwa hao waliopindua ndio wapo mbele katika kuona kuwa mapinduzi hayo yanaendelea kudumu na sio venginevyo. Jaribu kutathimini matamko mbalimbali ya wale walioshiriki mapinduzi hayo waliyoyatoa hivi karibuni, na utapata kujua mwelekeo wa Zenj upo upande gani...
   
 18. S

  Stone Town Senior Member

  #18
  Sep 13, 2008
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalamu alaykum.

  nimeona nami nichangia kidogo mada hii ingawa sitaki kwenda sana kwenye suala la mwafaka kama ufikiwe au usifikiwe na au kuna haja ya wajumbe wa pande mbili za CCM na CUF kurudi tena mezani au kuendelea na msomamo wa kutorudi mezani.

  Ninachotaka kuchangia mimi ni pale mjumbe mmoja aliposema kwamba zanzibar hakuna matatizo kama za bimbambwe au kenya.

  Mimi ningependa sana mwenzangu huyu asikubali kusikia maneno ila akubali na ajitume zaidi katika kuzungumza na kuona ukweli ulipo tukianzia uchaguzi wa 1995 ambao wagombe wake alikuwa Dk. Salmin Amour kwa CCM na Maalim Seif kwa upande wa CUF. kuhusu matokeo ya uchaguzi huo kila mmoja anafahamu kilichofanyika.

  mtu mmoja alipoteza maisha kwa kupandisha bendera ya CUF kisiwani Pemba na askari polisi mara baada ya mfumo wa vyama vingi kukubalika.

  Mwenzangu hapo juu umeeleza mengi ikiwemo zanzibar kukubwa na machafuko tukianzia kampeni za 1995 kulikuwa na kikundi kinachoitwa melody hiki kilikuwa kikipita nyumba hadi nyumba kupiga watu huku wakijua nyumba za wapinzani na kuwaadhibu.

  mwaka 2000 hali ilikuwa zaidi tokea kampeni hadi uchaguzi watu walikuwa wakipigwa ovyo na baadae kutokea kama alivyoeleza mwenzangu hapo juu maandamano ya tarehe 26/na 27 januri 2001 yaani rais karume ndio kwanza anaingia madarakani katika kipindi chake cha kwanza amesababisha vifo vya watu kadhaa amabvyo hadi leo hesabu yake ipo tata lakini kwa ufupi hata kama mtu mmoja ameuawa basi ndio roho imepotea.

  tukija mwaka 2005 mara baada ya kuletwa utaratibu wa daftari la wapiga kura CCM wametumia kila njia kuhakikisha watu wa CUF wanawakataa wasiandikishwe kwa kutumia masheha na kama uliwahi kusikia masheha akisema mimi huyu simtambui basi hakikisha haki yako hiyo huipati katu.

  zaidi ya watu 40 wamerejehiwa kwa mapanga wakiwa katika line ya kupiga kura mchana na picha zipo tele na majina tunayo ya watu waliopigwa.
  kuna nyumba zimeunguzwa moto, kuna wafanyabiashara kadhaa kwa kuwa tu wana asili ya kisiwa cha pemba wameharibiwa bidhaa zao kwa kutiwa moto mfano wa hao ni mfanyabishara mmoja wa kiwanda cha mbao amepoteza zaidi ya millioni 500 kwa wakati mmoja baada ya mbao zake, mabati na makontena manne ya vigae vya kujengea nyumba kutetetezwa pale mtaa wa saateni mjini unguja na vijana wanaoitwa janjaweed.

  watu wa maeneo ya jangombe walipigwa hadi kuzimia na vijana hao wa janjaweed huku maeneo ya mji mkongwe waliendewa mchana na kuvamiwa na janjaweed na kupigwa vibaya sana.

  ukwenda pemba ndio hakusemeki kuna shabiki mmoja wa kipemba anaitwa khamis kisone amewapigishwa watu wa CUF tokea 1995,2000 na pia 2005 amekuwa akitumia vikosi cha KMKM na JKU kuwapiga watu bure na kuvamia nyumba zao na kuiba bidhaa mbali mbali mimi kwa hakika miaka hiyo miwili ya mwanzo sijakuwepo ila nakumbuka mwaka 2005 nilikwenda pemba na kushuhudia mambo mengi sana ikiwemo watu ambao walikuwa wakielezea jinsi walivyoendewa ndani ya nyumba na kutakiwa kutoa kila kitu na baadhi yao kupigwa vibaya sana.

  kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini alithibitisha mbele ya waandishi wa habari kwamba khamis kisone ni kada wa CCM na ametumia cheo chake ya CCM kuwataka JKU kuvamia nyumba aneo la wete na kuwapiga watu waandishi wakamuuliza inakuwaje mtu wa kawaida tu atoe amri kwa JKU na wao watii amri kamanda akajibu hiyo gari ya JKU ilikuwa imeasi na ndio wakatoroka eneo lao waliopangiwa na kwenda mitaani kupiga watu alipoulizwa tena hatua gani atachukuliwa? kamanda akajibu atashitakiwa lakini siku moja baada ya waandishi kuhoji hayo walionesha huyo khamis kisone akiwa mitaani na hadi leo hajwahi licha ya kushitakiwa hata kuhojiwa au kukamatwa.

  na hayo mambo yote waliofanyiwa hatu wao husema alhamsulillah yaani wanamuachia mungu tofauti na wezetu bara mnapofanyiwa mambo kama hayo huwa mnalipiza kisasi huku watu bado wana ile kumuachia mungu ingawa sio sahihi ni vyema kukalipizwa kisasi maana naamini kama siku moja tu watu wataamua kufnaya hivyo basi hakutakalika.

  haya ninayo yasema nina ushahidi nayo ninayo hadi siku na tarehe ya mambo haya yaliotokea maana nina kumbukumbu nayo hata ukenda pale hospitali ya Alrahma utapata listi ya watu waliokuwa wakipigwa marungu na mapanga eneo la kinuni na sehemu nyengine nilizozitaja. picha zipo na DVD zipo hata zile za wakati wa uchaguzi jiznsi polisi walivyokuwa wakiwapiga watu bure lakini pia kuna walivynjiwa nyumba zao na wengine kulazimishwa kula picha ya maalim seif ambazo zilikuwa zimebandikwa katika ukuta wa nyumba.

  kwa ufupi ni mambo mengi sana sana ambayo hata mengine hayasemeki maana ni ya udhalilishaji na mimi ni mwanamke ninaumia sana nikiyasimulia lakini juu ya suala hili nakumbuka hata waandishi waliokuwepo walikuwepo waandishi wengine kutoka bara akiwemo john ngahyoma wa BBC alikwenda Pemba na kuwahoji watu waliokuwa wamepigwa na kudhalilishwa. kati ya walidhalilishwa hata wabunge akina khalifa walipigwa nao na waliwekwa alama mgongoni kwa kipigo.

  unguja kulikuw ana watu kadhaa waliokuwa wameathirika na matatizo kama hayo sasa mtu anaponambia kama zanzibar hakuna tatizo mimi nashangaa sana ukiondosha lile la kukoseshwa nafasi za kazi na takwimu zipo kama unazihitaji kuna listi ya wapemba wangapi amabo wamo serikalini na katika nafasi za kutoa maamuzi lakini kuna udhalilishaji mkubwa sana umefanyika zanzibar.
  naomab niishie hapa kwa hakika sijaandika kwa ufasaha kutokana na haraka ya kukimbilia kuangalia news.

  stone towner
   
 19. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Nakupa pole maana hujui unachokijengea hoja, mimi si mzanzibar lakini najua siasa za zanzibar za tangu enzi za "siasa za gozi" najua kuwa Mzee Karume hakuwa Rais wa Zanzibar ila alikuwa mtawala kwanini?Rais huchaguliwa na mtawala hutawala aidha kwa mabavu au kwa kupindua! najua kuwa tangu mapinduzi ni mtu mmoja tu kutoka pemba amewahi kushika nafasi ya waziri kiongozi kwenye serikali ya mapinduzi. Najua kuwa mawaziri wote wa serikali ya zanzibar hakuna hata mmoja anaetoka visiwa vya pemba. Sasa kama wewe huoni tatizo hapo basi utakuwa kipofu au una lako jambo.

  Serikali inayotakiwa ishirikishe wazanzibari wote, leo hii ikifika wakati Rais wa Tanzania awe anatokea BAgamoyo tuu unadhani watu hawatapaza sauti? walipokuwa Sokoine, Msuya, Sumaye na Lowasa waliposhika uwaziri mkuu watu walisha anza kusema kuwa nafasi hiyo sasa inataka kujengeka kama desturi watu wa kaskazini ni yao! Kenye bunge la juzi kuna mbuge alilalamika sana kwanini kaskazini wanapendelewa miradi ya maendeleo yote inapelekwa huko kwanini?akasema inakuwa kama "sisi waislamu kila tukisali lazma tuelekee kaskazini"

  Mgororo uliopo Zanzibar sio wa uzushi au wa kupangwa kama wewe unavyodai.

  Mgogoro wa Kenya kuna viombo huru vilieleza kuwa yale machafuko yalipangwa na moja ya makabila makubwa na ukiangalia kwa undani utaona makabila makubwa mawili ndio waadhirika wakuu (Luo la Raila na KIkiyu la Kibaki) Maeneo ya coast hayakuwa na athari ila katika zile sehemu wanazokaa hayo makabila mawili kama nje ya mji wa mombasa maeneo ya bombolulu, shanzu na Bamburi. lakini city centre hakukua na machafuko na wala hakuna nyumba zilizochomwa moto!

  Zimbambwe ni zaidi ya mnavyo ona nimebahatika kuwa na rafiki anaeishi Zimbabwe na juzi juzi nilikuwa nae Dar es Salam akielekea China ameniambia kuwa machafuko ya Zimbabwe ni zaidi ya mambo ya siasa kuna na ukabila pia! Kuna washona na wantebele washona wanamsapoto Mugabe na Wantebele wanamsapoti Tchangarai.


  Kwa mifanoi hiyo hapo inaonyesha ubaguzi ndio unaochochea fujo kuanzia uunguja na upemba, Uluo na Ukikuyu na Ushona na Untebele sasa iweje wao waweze wa unguja na wapemba washindwe? Hivi ndivyo ilivyo?[/FONT]
   
 20. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  rafiki yangu Kibunango kumbe unaota, kam huoti basi kimbilia Muhimbili haraka kwani Malaria inakuja, Leo kama Tanzania watasema cuf wameshinda uchaguzi Zenj ndio imetoka na anaebisha ndie atakuwa mhaini, kumbuka Abod Jumbe alikwishia wapi? na yeye alikuwa raisi mzima kama unavyotaka tuseme kwahiyo zenj tulieni
   
Loading...