Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,187
Upo msemo wa Kiingereza ambao tafsiri yake inasema; “kurudia kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile, huku ukitarajia matokeo tofauti, ni uendawazimu.”
Sitaki kusema kuwa Zanzibar imefikia hatua hiyo linapokuja suala la muafaka. Lakini imefika wakati sasa tujiulize hii miafaka (sijui kama huo ndio wingi wa neno muafaka) ambayo imekuwa ikijirudia muda mfupi kila baada ya uchaguzi mkuu haiashirii huu msemo wa Kiingereza niliounukuu?
Inashangaza kuwa kila baada ya uchaguzi kunakuwa na mgogoro wa kisiasa Zanzibar unaotokana na malalamiko kuhusu uchaguzi. Siku zote malalamiko yanatolewa na vyama vya upinzani kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Hapa, vyama hivyo vya upinzani (kilianza CUF na sasa kuna ACT Wazalendo) vinatishia kususia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Kila mara, mgogoro huo unafuatiwa na vikao baina ya Chama Cha Mapinduzi (ambacho ndicho kinalalamikiwa) na chama cha upinzani. Kila mara mazungumzo haya huzaa makubaliano (yaite muafaka) na baada ya hapo chama cha upinzani hurudi kujiunga kwenye SUK.
Lakini mara tu baada ya kujiunga, malalamiko hutolewa tena na chama hicho cha upinzani kikieleza kasoro kadhaa katika uendeshaji wa SUK.
Unapokaribia uchaguzi, chama hicho cha upinzani kinaweza kuja na tishio la kususia uchaguzi lakini suluhu hutafutwa na hatimaye kinashiriki uchaguzi.
Wakati wa kampeni kunawezaa kuwa na malalamiko kutoka chama hicho cha upinzani kuhusiana na kutotendewa haki na na Tume ya Uchaguzi (ZEC). Lakini hatimaye chama hushiriki uchaguzi.
Mara tu baada ya uchaguzi, malalamiko ya chama cha upinzani kuhusu kutotendewa haki katika uchaguzi huibuka na mzunguko wa majadiliano, makubaliano, malalamiko mapya, majadiliano tena, makubaliano hujirudia mpaka unapofika uchaguzi mwingine.
Kila mara chama cha upinzani Zanzibar hutoa malalamiko na madai yale yale. Kila mara suluhu hutafutwa kwa njia ile ile. Kila mara Suluhu huwa ni ile ile.
Kila mara tunashuhudia mzunguko huu ukijirudia huku wahusika wakuu, walalamikaji na wanaolalamikiwa wakifanya yale yale lakini wakiueleza umma kuwa wanatarajia kuwa wakati huo kutakuwa na matokeo tofauti.
Nadhani sasa umefika wakati wanasiasa wa Zanzibar watupumzishe kidogo. Huu mtindo wao wa kufanya mambo yale yale, kwa namna ile ile na kutuahidi kuwa kutakuwa na matokeo tofauti, unapaswa kufika mwisho.
Inashangaza sana kuwa watu wazima, ambao wanaaminiwa na wananchi wengi, wanatufanyia mambo haya mchana kweupe.
Hapa majuzi tumesikia tena kuwa baada ya ACT Wazalendo kususia kujiunga kwenye SUK baada ya kulalamikia uchaguzi w mwaka jana, yamefanyika mazungumzo na sasa suluhu inakaribia kupatikana na kama inavyotarajiwa ACT kitajiunga kwenye SUK.
ACT Wazalendo kinasisitiza kuwa mufaka utakaopatikana utaweka mbele maslahi ya Zanzibar. Hii nayo si kauli mpya. Kila mara vyama vya upinzani vilipolalamika na muafaka kufikiwa tuliambiwa kuwa muafaka huo ni kwa maslahi ya Zanzibar.
Kama ni hivyo, inashangaza sana kuwa maslahi ya Zanzibar ni kuendeleza mzunguko wa malalamiko – majadiliano - makubaliano na kurudi tena kwenye malalamiko!