Huu wizi nao umeshapiga hodi Tanzania! Ulaya uko siku nyingi sana. Wanatumia njia nyingi na kuuza vitu vya aina nyingi! Muuzaji anakuwa kwenye gari anaendesha halafu anapolenga target yake anasimama na kukuuliza njia ya kwenda kwa mfano airport au sehemu nyingine. Baada ya kumwelekeza anakuambia pengine nilikuwa kwenye maonyesho ya mavazi na hapa kuna jacket la ngozi au suti zimebaki nitoe na kitu kidogo nikuachie... Sasa wewe kwa kusikia jacket la ngozi unalinunua chapchap kumbe si ngozi ya ukweli au suti si original ni za bei rahisi tu.Kuna mzungu (asili ya italiano) ana rav4, anatumia kigezo kuwa anasafiri kwenda airport kwa hiyo anasuit za armani original kwa dola 700 kwa 3.
Suit hizo ni fake na unaweza nunua kwa dola 50 tu.