Mtwara Vipi Jamani?

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,040
Salam Wakuu!
Ni juma la pili sasa nipo mjini Mtwara kikazi namshukuru Mungu.
Japo ni mara yangu ya mwanzo kuishi hapa nimebaini kuwepo kwa kasi ya mabadiliko hasa ktk fursa za kibiashara kutokana na kuwepo makampuni kadhaa makubwa ya kigeni yanayoendesha shughuli zao hapa mjini Mtwara ktk sekta ya nishati nk. Makampuni haya yameweza kuto ajira si haba kwa wazalendo wengi kwa ngazi ya kati na chini kutoka ukanda huu wa kusini na mikoa mingine pia.
Pia kuna vyuo na taasisi za elimu ya juu zimeanzisha vituo vyao hapa mjini Mtwara kama vile Chuo kikuu cha St. Agustino, Veta nk... Ambako huko kuna mkusanyiko mkubwa wa wageni kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo wanafunzi na wafanyakazi ktk taasisi hizo. Kwa hayo machache nidhahiri kuwa mji wa Mtwara unashuhudia mabadiliko na ongezeko la fursa ambazo hapo kabla hazikuwepo.
Kinachosikitisha ni kuwa wenyeji wa mji wa Mtwara wameshindwa kwenda sawia na mabadiliko hayo niliyoyataja. Hali ilivyo ktk upatikanaji wa huduma na namna ya utoaji wa huduma hizo pale inapopatikana japo kwa uchache inatia shaka.
1.Vituo vingi vya kuuzia mafuta havina nishati hiyo muhimu
2. Maduka (hata yale ya uswahilini)yanafunguliwa kuanzia saa 1 hadi 2 asb.
3. Wafanyabiashara wadogo Vocha, Vigenge, Vinywaji baridi na wale wa kati wanafanya kazi hiyo kwa mazoea zaidi hawana lugha ya kistaarabu. Unaweza ukasubiri hadi dk 10 mwenye duka hajakusemesha japo kukuangalia. Na unapoamua kuondoka kwa kuokoa muda wako utasindikizwa na maneno ya kifidhuli "Nenda we si mteja" mara nyingi kila utakapoenda hali ni hiyo.
4. Hata huduma ya chakula inapatikana kwa taabu ktk maeneo mengi ya mji na zilizopo haziendani na kasi ya mabadiliko ya kimji.
Kwa bahati nimebaini kuna jamaa kutoka mikoa ya kaskazini wanachangamkia fursa na nimeshuhudia mkusanyiko wa wateja wakifuata huduma na lugha murua sambamba na utayari wa mtoa huduma.
Kwa maoni yangu WanaMtwara wanapaswa kubadilika kungali mapema na kuchangamkia fursa zilizopo na zijazo. Kikubwa wabadilike ktk namna ya utoaji wa huduma zao hasa ktk kauli njema kwa wale wanaowapa huduma. Vinginevyo wataishia kushuhudia wageni wakijitwalia fursa mchana kweupeee!!
Nawasilisha...
 
Mweh!! Bwashee kwanza pole sana na adha unayopata ila tuna mpango wa kuwanyolosha wafanya biashara kiburi wote tushamwambia mr area kamshina mpya
 
Ni kweli kabisa, nilikuwa huko mwaka jana kikazi, wafanyabiashara ni jeuri hawana lugha nzuri kabisa!
 
Back
Top Bottom