Mtwara: Serikali imesema bandari ndiyo njia pekee ya usafirishaji itakayotumika kusafirisha Korosho na si barabara


Kunguru Mjanja

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Messages
1,972
Likes
3,214
Points
280
Kunguru Mjanja

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2012
1,972 3,214 280
korosho-jpg.625941


Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo amesema bandari hiyo ilitumika mwaka jana kusafirisha korosho na kufanya vizuri hivyo maamuzi hayo hayajabadilika.

Amesema mkoa wa Mtwara umepata manufaa makubwa kutokana na bandari hiyo kukusanya ushuru wa korosho ambapo kwa mwaka jana pekee bandari hiyo iliweza kukusanya shilingi Bilioni miamoja na ishirini na nne kama ushuru wa forodha.

Hata hivyo amesema serikali pia imekukusanya shilingi Bilioni 21 ikiwa ni fedha ya ushuru wa korosho,na katika fedha hizo imetoa shilingi Bilioni miamoja na thelathini na saba kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea.

Hivyo amesema kwa manufaa hayo serikali ya mkoa itaendelea kusimamia hilo ili kuhakikisha bandari ya mtwara inatumika vema katika usafirishaji wa korosho na kuwataka wafanyakbiashara kutumia bandari hiyo ambayo kwa sasa imeboreshwa.

Hata hivyo amekemea baadhi ya wafanyabiashara wanaoendelea kusafirisha korosho kwa kutumia barabara na kusisitiza kuwa mkoa umejipanga kukabiliana na wale wote wasiotii maagizo ya serikali na yeyote atakayekamatwa sheria itachukua mkondo wake.

CHANZO: ITV
 
Pundugu

Pundugu

Member
Joined
Sep 22, 2017
Messages
53
Likes
54
Points
25
Pundugu

Pundugu

Member
Joined Sep 22, 2017
53 54 25
Mkuu wa mkoa aliyetoka aliongea hivihivi, kwani hiyo CD haijaanza kuscrach.
 

Forum statistics

Threads 1,235,471
Members 474,585
Posts 29,223,237