Mtwara: Mwanafunzi kidato cha pili ajinyonga kisa mapenzi

Mtwara: Mwanafunzi kidato cha pili ajinyonga kisa mapenzi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,716
kitanzi.jpg

​
Binti Salma Abdalah ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mkoani Mtwara aliyekuwa akiishi Mbawala Chini, amefariki dunia kwa kujinyonga, baada ya kukutwa na simu ambayo alipewa na mpenzi wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya, amesema tukio hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii baada ya wazazi wa binti huyo kuamua kumfukuza nyumbani na kumtaka kwenda kusihi kwa bibi yake kutokana na utovu wa nidhamu, na ndipo akaamua kujitoa uhai wake.

Kamanda Mkondya ameendelea kwa kueleza kwamba wazazi wake waligundua kuwa binti yao alikuwa akimiliki simu ambayo hawajamnunulia, na walipomuuliza hakuwa na jibu sahihi, ndipo baba mtu ambaye ni baba wa kufikia aliamua kumfukuza nyumbani kutokana na kuchoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu, na kuelekea sokoni kwenye biashara zake kumtafutia nauli, huku mama yakle kuelekea shambani kwenye shughuli zake za kilimo,

“Ni binti ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili, sasa asubuhi baba yake wa kufikia akasikia simu ikiita kutoka chumbani kwake, akamuambia mama yake na kumuuliza alikoipata, lakini hakuwa na jibu, baada ya hapo wazazi wake wakatoka kuelekea shambani na kumwambia kuwa wamechoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu hivyo wakirudi wasimkute aondoke, huku nyuma akaamua kujinyonga kwa kutumia khanga”, amesema kamanda Mkondya.

Taarifa zaidi kutoka kwa mashuhuda wa tukio wamesema binti huyo alipojinyonga aliacha ujumbe uliosema kwamba "Nampenda sana Daudi, siwezi kukaa naye mbali najua hili ni kosa kwangu lakini nawaomba wazazi wangu mumpende sana Daudi maana akiwa kwenye matatizo, mimi sitajisikia vizuri".
 
sasa alikoenda huko mbona ndo ameenda mbali zaidi na daudi. any way R.I.P
 
Ndio nakubali kwa kidato cha pili alikua bado haja jitambua ye ni nani na thamani yake katika jamii alikua bado hajaitambua,hivyo tunasema that is the problem ,R I P
 
Ni muhimu kuwa karibu na watoto wetu na kuwaongoza hasa katika kile kipindi cha biological changes za mwili

Sky Eclat umeongea kitu cha muhimu sana, bt wengi wanadhani kuwa karibu na watoto wakati wa hizo biological changes, basi ni kuwa mkali na kutembeza mkong'oto pale wanapoona watoto hawasikii.. Ni kosa kubwa sana.. Biological changes haziwezi kuzuiwa kwa ngumi, fimbo, kipigo wala anything else.. Ni vema wazazi/walezi wakalielewa hili, ili kuepusha tragedy kama hii ya huyu binti masikini.. Ni vema wazazi wakawaelewa watoto, hata kama wanayoyasikia hawayapendi, kuwasikiliza kwa makini, na kuwaongoza kwa kuwaelewesha na pia kuwapa mbadala.. Hii tabia ya kumkazania mtoto asifanye mapenzi, wakati kwingine kote anakokwenda huko anakuta mazingira rafiki ya kufanya mapenzi, imepitwa na wakati..

Sasa hawa wazazi, wamemkuta mtoto na simu, wamemfukuza.. Tena mtoto wa kike mwenye umri mdogo bado.. Wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kifo cha huyu binti.. Hawawezi kukwepa..
 
Daudi dah,

Hapo mtoto alikuwa kafika,

First love mbaya sana,

Mimi kuna demu nilimkuta hajatibolewa nikaanza mimi,

Baadaye nikazingua weeee alitaka kujiua chumbani kwangu

Nikasema kazi ipo hapa
 
Back
Top Bottom