Mtwara kuwa kama Niger Delta

Mtwara kuwa kama Niger Delta

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,638
Reaction score
1,219
Wana JF,

Kadiri upepo unavyovuma huko kusini mwa Tanzania kwenye mkoa wa Mtwara kuhusiana na Gasi Asilia hali inazidi kubadilika kila kukicha.
Kwa wale mnaofahamu historia na Siasa za Nigeria kuna sehemu yenye utajiri wa Mafuta inayoitwa NIGER DELTA. Hili eneo linazalisha karibu asilimia 80 ya mafuta ghafi yanayochimbwa nchini Nigeria. Lakini Wananchi wanaoishi maeneo hayo ni masikini wa kutupwa!
Kutokana na hali hiyo wananchi wanaokaa eneo hilo waliamua kupinga Makampuni yanayochimba mafuta katika eneo hilo kwa kulipua mabomba ya mafuta,kuwateka mateka wafanyakazi wa kigeni wanaofanya kazi kwenye makampuni hayo ya kuchimba mafuta na kuwaua pale waajiri wao wanapo kataa kutoa pesa ili wawaachie mateka hao.

Sasa inavoelekea hali hii inaenda kuikumba Tanzania katika mkoa wa Mtwara ambako kwa sasa kuna harakati kubwa za kuanza uchimbaji na usafirishaji wa Gasi asilia toka Mtwara na kwenda Bagamoyo na Dar. Mawazo na ushauri wa Wananchi wa Mtwara wa kutaka na wao wanufaike na hiyo Gasi asilia kwanza kabla haijasafirishwa kwenda Dar na Bagamoyo yamepuuzwa na Serikali ya CCM!

Sasa wana Mtwara wameamua kula sahani moja na Watawala wa CCM. Tumesikia nyumba za Viongozi wa CCM,Polisi na Wafuasi wa wao zikichomwa moto kuonyesha kupingwa kwa jambo hilo. Tumeanza kusikia pia kwamba Mkandarasi anayechimba na kuweka mabomba ya kupitisha hiyo Gasi anatishiwa na Wanannchi hao wenye hasira. Sasa tumeanza kusikia magari yanayopeleka vifaa vya ujenzi wa Bomba hilo yameanza kushambuliwa na Wananchi.

Hiyo ni dalili ya hatari kwamba tunaenda kuwa na Niger Delta huko Mtwara very soon. Serikali msipuuze jambo hilo kaeni na Wananchi mfikie mwafaka badala ya kutumia mabavu. Mungu ibariki Tanzania.
 
waache waendelee kuwapuuza maana kazi ya ukombozi itazidi kuwa rahisi kwetu 2015
 
Back
Top Bottom