Mtwara kupandisha bendera yetu

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
MTWARA KUPANDISHA BENDERA YAO Mwenykiti wa UDP Mtwara mjini Seleman Chimpele akihutubia mkutano VYAMA Sita vya siasa vya upinzani vya wilaya ya Mtwara vimeungana kuendesha mikutano ya adhara ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kupinga gesi asilia kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Katika kutengeneza umoja huo vyamahivyo vimekubalina kutengeneza bendera ya Mtwara itakayopandishwa kuashiria umoja wa wananchi hao katika kutetea rasilimali yao. Tayari Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi wa ujenzi wa bomba hiyo huko Kinyelezi jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita, kitendo kinachopingwa na wakazi wa mikoa ya kusini hususani Lindi na Mtwara. Hoja za wananchi za kupinga gesi kwenda Dar es Salaam zilisababisha kuzomewa kwa mawaziri watatu mbele ya katibu mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana alipofanya mkutano wa adhara soko kuu mjini Mtwara hivi karibuni.

Jana viongozi wa vyama vya siasa Sita, NCCR Mageuzi, APPT aendeleo, TLP, ADC, Chadema na UDP walianza mikutano ya kupinga kuhamishwa kwa gesi katika viwanja vya Mkanaledi. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Uledi HassanAbdallah alisema wapo tayari kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya nguvu ya umma na mahakama. "Kwa hali ilivyo ni njia mbili tu zinaweza kuokoa gesi yetu isipelekwe Dar es Salaam, moja kwa njia ya maandamano, pili mahakama" alisema Uledi Alifafanua kuwa "Gesi ikihamishwa mikoa ya kusini itaendelea kuwa masikini hadi mwisho wa dunia… tuseme inatosha, tuwe tayari kutetea maslahi yetu kwa ajili ya vizazi vyetu" Alisema katika awamu hiyo ya kwanza mikutano minne itafanyika ikitanguliwa na kauli mbiu "Gesi kwanza, vyama baadae, hapa hakitoki kitu" Katibu wa TLP wilaya ya Mtwara, Hayadhi Walilanga alisema ili kufanikisha hilo bendera moja itatengenezwa ambayo itajulikana kama bendera ya Mtwara ambayo itakuwa kama ishara ya muungano wao katika kueteta gesi. "Wachoraji watuandalie bendera moja takayotambulisha Mtwara katika kutetea rasilimali yao ya gesi isiporwe na wachache….tutaipandisha kila kwenye mkutano wetu" alisema Walilanga.

My Take;
Mambo yatatokota vizuri muda si mrefu. Kila kwenye gesi na mafuta barani Africa ni lazima machafuko
 
‘KWANINI HAWATAKI GESI ITOKE MTWARA’ DESEMBA 13, 2012 Mtandao wenu wa KUSINI
ulichapisha bahari zinazohusu vyama vya siasa vya
upinzani vya wilaya ya Mtwara kuungana kupinga
gesi wenda Dar es Salaam kwa kaulimbiu “Gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu”. Kutokana na maoni na michango ya wasomaji
wangu, KUSINI imeona bora ichapishe hoja
zinazojengwa na Wana Kusini katika kutia nguvu
hoja yao ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam
kwa njia ya bomba. Kimsingi wakazi wa kusini hawapingi gesi kwenda
nje ya Mtwara na Lindi, wanasema gesi inaweza
kupelekwa kokote Duniani ili mradi iwe iliyosafishwa
tayari kutoka Mtwara na sio mbichi (raw). Wanasema ni vema kiwanda cha kusafisha gesi
kikajengwa Mtwara ili wakazi wa Mtwara wapate
ajira na hivyo kupunguza hali duni ya maisha
inayowakabili kwa sasa, wanahoji ni mwekezaji gani
aliye tayari kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 500
kwenda Mtwara kuwekeza wakati gesi ambayo ingekuwa kigezo cha yeye kwenda huko inapatikana
Dar es Salaam? Wakazi wa mikoa ya kusini wameona kwa macho
yao kule Songosongo Kilwa mkoani Lindi, ambako
gesi imesafirishwa kwenda Dar es Salaam, hakuna
kiwada wala mwekezaji aliyewekeza eneo lile, zaidi
ya ufukara kuzidi kuwaandama wakazi wale. Waungwana husema, kosa si kutenda kosa bali
kurudia kosa. Hoja nyingine ni ile ya mitambo ya kufua umeme
kujengwa Kinyerezi, wanahoji kwanini Dar es
Salaam na sio Mtwara, ipi ni gharama kubwa
kujenga bomba au kutandaza nyaya za umeme?
Jibu hapo ni kutandaza nyaya za umeme ni nafuu,
kwanini basi mtambo huo usijengwe Mtwara halafu umeme ukapelekwa hata Rwanda? Hoja ya KUSINI ni kwamba kwanini tutumie akili
nyingi kuongeza uhamiaji wa watu kutoka vijijini
kwenda mijini badala ya kutatua tatizo? Leo hivi mitambo, viwanda vingejengwa Mtwara
watu wangetoka Dar es Salaam na kwingineko kuja
kufanya kazi Mtwara, watu wangehama mjini na
kukimbilia kijijini, lakini hebu jiulize leo jiji la Dar es
Salaam ndilo tegemeo la pato la Taifa kwa asilimia
zaidi ya 80, iwapo jiji hili litapatwa na janga lolote (siombei) hivi Tanzania itakuwa katika hali gani? Hapa nadhani ni ufinyu wa kufikiri, ndio maana hata
kuhamia Dodoma hawataki wamekaririshwa kuwa
‘Dar ndiyo mpango mzima’ na kwamba kitu kingine
kizuri hakipaswi kuonekana zaidi ya Dar na maeneo
mengine na sio kusini. Wananchi wa mikoa hiyo pia wanaumizwa na
historia ambayo mikoa ya kusini mara baada ya
uhuru ilitangazwa kuwa ni maeneo ya kupigania vita
ya ukombozi kusini mwa Afrika, kwa msingi huo
hakuna maendeleo yeyeto kwa miaka 10, ndiyo
maana barabara za kuingia Lindi na Mtwara hazikutengenezwa. Ndiyo maana Reli ya Kutoka Nachingwea kwenda
bandari ya Mtwara iling’olewa, ndiyo maana mikoa
ya Lindi na Mtwara haikuunganishwa na umeme wa
grid ya Taifa. Watu wa kusini wanahisi kuonewa kwani hata
walipotaka kulima zao la pamba ambalo wataalam
wa kilimo wanathibitisha kuwa linastawi vizuri katika
mikoa hiyo serikali ilipiga marufuku kwa madai wapo
wadudu nchi ya Msumbiji ambao wanaweza kuingia
Tanzania nakuathiri pamba ya kule mikoa za kanda ya ziwa. Wazee wa mikoa hii wanasema kulikuwapo na
makubaliano yasiyo rasmi kuwa baada ya vita vya
ukombozi kwisha mikoa ya kusini ingefidia kwa
kuharakishiwa maendeleo jambo ambalo
halijafanyika hadi leo. Mungu kawaona kawapa gesi, nayo inaondolewa
kupelekwa Dar ndipo wanapohoji Kusini imeikosea
nini Tanzania? Kwani kuna ubaya gani mitambo na
gesi ikibaki Mtwara, sio Tanzania au wakazi wake
hawasitahili? KUSINI inashauri Serikali kutafakari upya jambo hili
vinginevyo linaweza kutupeleka pabaya, hebu
tujifunze kwa wenzetu Sudani Kusini. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mi nawaunga mkono! Why kila kitu Dar? Ni upuuzi. Watu mikoani wanafuata maji ya kunywa km 5, eti Dar wanaweka flyovers. Huu ni ushenzi
 
Tulisha sema hapa! Kwamba kabla ya Mkulu kumaliza awamu yake hii, kwa hali hii ya kuwa mnafiki, ataiacha nchi ikiwa vipande vipande.

There we go.
 
Hatukatai (MAFILILI) Hii ni mali ya Tanzania,Wana Mtwara tunataka kuuona Mkataba wa Gas kati ya Nchi na huyo Mwekezaji unasemaje?,tumesikia kuna watu wamewekewa Pesa Uswis na Makampuni ya Gas na Mafuta (haya yote yako Mtwara)
Hatujaiona sababu ya Msingi ya Kujengwa Pipe la Gas tu Dar na kinu cha kufulia Gas kuwa huko .
Tuliahidiwa kutakuja Viwanda Vingi Mtwara kwani kutakuwa na Umeme wa uhakika ,Je Viwanda vitakuja kama Umeme utakuwa unafuliwa Dar.

Sasa hivi hapa inapita Gari inatangaza leo saa 8 mchana kutakuwa na Mkutano wa watu kutoa maoni yao ya Sera ya Gas kuanzia saa nane,wakati wanafahamu leo hapa Mtwara kuna Mkutano MKUBWA pale BIMA wa muungano wa vyama vyote kuhusu kupinga Gas kusafiri kwenda Dar .

TUTAFIKA TU
 
CHADEMA wanasema tuu kwa maneno ,Serikali za Majimbo ,sasa Mtwara wanaonesha kwa Vitendo .Bendera hiyoooooo inakuja.
 
Bendera Hawathubutu .....
Lakini wana haki ya kupigania gesi Izalishwe Huko...Dar na Mikoa mengine wapelekewe Final Products....
Kuhusu umeme ...uzalishwe huko na kusambazwa sehemu nyengine nchini......
Hii si kwa Mtwara bali sehemu yoyote ile yenye Mali ASILI
 
Yeah,mwisho watapaleka bagamoyo,tukomae nao chacha gechi yetu ichiondoke baaa
 
Ni kweli Mungu akikunyima akili amekunyima kila kitu! Na mamiresource yoote hii mungu aliyotujaalia bado tunalialia tuu!
 
Kwann hawakuukataa umeme wa mtera na kidatu wakati unavutwa na kupelekwa kwao.?au ndo ubinafsi huo???Kilimanjaro nao wakisema hela ya mlima Kilimanjaro isiende serikali kuu,dodoma na singida si watakufa njaa?
 
Ngoja nichangamkie tenda ya kuchora bendera ya Mtwara, na kutunga wimbo wa mkoa wa Mtwara
 
MTWARA KUPANDISHA BENDERA YAO Mwenykiti wa UDP Mtwara mjini Seleman Chimpele akihutubia mkutano VYAMA Sita vya siasa vya upinzani vya wilaya ya Mtwara vimeungana kuendesha mikutano ya adhara ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kupinga gesi asilia kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Katika kutengeneza umoja huo vyamahivyo vimekubalina kutengeneza bendera ya Mtwara itakayopandishwa kuashiria umoja wa wananchi hao katika kutetea rasilimali yao. Tayari Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi wa ujenzi wa bomba hiyo huko Kinyelezi jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita, kitendo kinachopingwa na wakazi wa mikoa ya kusini hususani Lindi na Mtwara. Hoja za wananchi za kupinga gesi kwenda Dar es Salaam zilisababisha kuzomewa kwa mawaziri watatu mbele ya katibu mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana alipofanya mkutano wa adhara soko kuu mjini Mtwara hivi karibuni.

Jana viongozi wa vyama vya siasa Sita, NCCR Mageuzi, APPT aendeleo, TLP, ADC, Chadema na UDP walianza mikutano ya kupinga kuhamishwa kwa gesi katika viwanja vya Mkanaledi. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Uledi HassanAbdallah alisema wapo tayari kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya nguvu ya umma na mahakama. "Kwa hali ilivyo ni njia mbili tu zinaweza kuokoa gesi yetu isipelekwe Dar es Salaam, moja kwa njia ya maandamano, pili mahakama" alisema Uledi Alifafanua kuwa "Gesi ikihamishwa mikoa ya kusini itaendelea kuwa masikini hadi mwisho wa dunia… tuseme inatosha, tuwe tayari kutetea maslahi yetu kwa ajili ya vizazi vyetu" Alisema katika awamu hiyo ya kwanza mikutano minne itafanyika ikitanguliwa na kauli mbiu "Gesi kwanza, vyama baadae, hapa hakitoki kitu" Katibu wa TLP wilaya ya Mtwara, Hayadhi Walilanga alisema ili kufanikisha hilo bendera moja itatengenezwa ambayo itajulikana kama bendera ya Mtwara ambayo itakuwa kama ishara ya muungano wao katika kueteta gesi. "Wachoraji watuandalie bendera moja takayotambulisha Mtwara katika kutetea rasilimali yao ya gesi isiporwe na wachache….tutaipandisha kila kwenye mkutano wetu" alisema Walilanga.

My Take;
Mambo yatatokota vizuri muda si mrefu. Kila kwenye gesi na mafuta barani Africa ni lazima machafuko

Mkuu hivi hivyo vyama ulivyovitaja vipo kweli Mtwara na Lindi? Maana kule nijuavyo mie ni CUF na CCM baaas!!!
 
Back
Top Bottom