Mtwara kupandisha bendera yetu

Mtwara kupandisha bendera yetu

Hao wananchi hawajui hata gesi inafananaje na wala hawajui utaratibu wake ulivyo. Wanadanganywa tu na wanasiasa. Waambie gesi sio kama maji ya bomba ni lazima isafirishwe ipelekwe kwenye mitambo. Sana sana wanatakiwa wadai manufaa yatokanayo na hiyo gesi yaani mapato. Watoe mapendekezo yao yatasikilizwa tu sio hato ys bendera wanataka kuwa kama Pwani huko Kenya?
 
Kwann hawakuukataa umeme wa mtera na kidatu wakati unavutwa na kupelekwa kwao.?au ndo ubinafsi huo???Kilimanjaro nao wakisema hela ya mlima Kilimanjaro isiende serikali kuu,dodoma na singida si watakufa njaa?

Siku zote wamekuwa wakitumia wa majenereta,haukuwa wa grid ya Taifa mkuu..
 
Mfumo wa majimbo unahusika

We acha tu dada.. Mi mwenyewe wa mikoa ya kaskazini,ila nimeishi sana Mtwara.
Fikiria kuna wilaya inaitwa Tandahimba.Unaambiwa imekuwa ikishindana manispaa za Dar kwa kuiingizia serikali mapato...! Inakuwa kwenye 3 bora karibu kila mwaka..
Ni kwa ajili ya kilimo cha Korosho. Imagine misimu miwili iliyopita iliingiza 54 bn.. Lakini maisha wanayoishi wenyeji sasa.. Au miundombinu yake sasa.. Acheni tu,ila hii nchi inatakiwa kuwa reformed au sijui nitumie neno gani labda..
 
kwann hawakuukataa umeme wa mtera na kidatu wakati unavutwa na kupelekwa kwao.?au ndo ubinafsi huo???kilimanjaro nao wakisema hela ya mlima kilimanjaro isiende serikali kuu,dodoma na singida si watakufa njaa?



utumie akili,,
hakuna aliekuambia ya kwamba watu hawataki kushare hiyo gase,hoja ni kwamba shughuli zote za processing zifanyike mahala husika kunapopatikana hiyo gase,,lione kwanza
 
hao wananchi hawajui hata gesi inafananaje na wala hawajui utaratibu wake ulivyo. Wanadanganywa tu na wanasiasa. Waambie gesi sio kama maji ya bomba ni lazima isafirishwe ipelekwe kwenye mitambo. Sana sana wanatakiwa wadai manufaa yatokanayo na hiyo gesi yaani mapato. Watoe mapendekezo yao yatasikilizwa tu sio hato ys bendera wanataka kuwa kama pwani huko kenya?

wewe nawe utambe una nini??

Ushawaona wenzako wajinga sio??watu wanaelewa kila kitu,labda wewe ndie mjinga wa mambo,,

kinachotakiwa gase ghafi isisafirishwe,,uandaliwe utaratibu wa processing sehemu husika inapopatikana gase yenyewe,ili manufaa kwa wakazi yaonekane kwa kiasi kikubwa,unakuja na hoja zako mfu unajiabisha tuh hapa
 
Sina Uhakika na usalama wa kufanya utafiti, kisha uvunaji katika mkoa mmoja halafu uzalishaji na ushafirishaji katika mkoa huo huo. La msingi hapa ni kujua Mtwara itanufaika vipi?

Kwa habari ya Lindi, nachojua kutajengwa kiwanda cha kuzalisha gesi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
Kilwa inauwezekano mkubwa sana ya kujenga bandari kama mbadala wa watafiti badala ya wote kutumia mtwara

Kengine Gesi inayopelekwa dar ni kwa ajili ya uzalishaji umeme wa taifa sielewi kama wananchi wanaambiwa ukweli au mimi nina taarifa zisizo sahihi....ila taarifa zangu ni kutoka kwa watafiti wakubwa
 
utumie akili,,
hakuna aliekuambia ya kwamba watu hawataki kushare hiyo gase,hoja ni kwamba shughuli zote za processing zifanyike mahala husika kunapopatikana hiyo gase,,lione kwanza
wewe ndo zuzu tena hutumii akili kabsa.,narudia tena,kilimanjaro si wangegoma na wao kuwa mahotel yote ya kitalii yanayotangaza na kupokea wageni wa mlima Kilimanjaro yawe moshi tu,na sio dar,Tumia hicho kichwa ulichopewa na Mungu kufikiri,usitumie vichwa vya wengine kufikiri.SHAME ON U.
 
Siku zote wamekuwa wakitumia wa majenereta,haukuwa wa grid ya Taifa mkuu..
Tatizo hapa ni kuwa mtwara hawaelewi wanachokitaka,shida yao ni mgawo wa mapato ya gesi kwenye halmashauri yao au gesi kusafirishwa,,,inakuwa shida sana kuona kuwa hata hujui unachokitaka.
 
bendera siafiki.... labda itafutwe njia mbadala maana bendera tayari ni kesi ya uhaini hiyo.... yani ni sawa na kusema hawana Imani na rais naona watafute njia mbadala tu isije ikala kwao kupandisha bendera ni sawa na unadeclare taifa lako labda kama mimi ndo nicwe mwelewa
 
wewe ndo zuzu tena hutumii akili kabsa.,narudia tena,kilimanjaro si wangegoma na wao kuwa mahotel yote ya kitalii yanayotangaza na kupokea wageni wa mlima Kilimanjaro yawe moshi tu,na sio dar,Tumia hicho kichwa ulichopewa na Mungu kufikiri,usitumie vichwa vya wengine kufikiri.SHAME ON U.



akili yako ndogo
huwezi kuelewa,anyway leave it to us
au wewe ni ccm mwenyewe??

pili pili hizi zinakuwashia nini,,kitu usichokielewa ni bora kukaa kimya kuliko kuandika uozo kama huu
nenda shule kwanza
 
akili yako ndogo
huwezi kuelewa,anyway leave it to us
au wewe ni ccm mwenyewe??

pili pili hizi zinakuwashia nini,,kitu usichokielewa ni bora kukaa kimya kuliko kuandika uozo kama huu
nenda shule kwanza
Big show anapumuliwa kisogoni na wnaume wenzie,hope you are not.
 
‘KWANINI HAWATAKI GESI ITOKE MTWARA’ DESEMBA 13, 2012 Mtandao wenu wa KUSINI
ulichapisha bahari zinazohusu vyama vya siasa vya
upinzani vya wilaya ya Mtwara kuungana kupinga
gesi wenda Dar es Salaam kwa kaulimbiu “Gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu”. Kutokana na maoni na michango ya wasomaji
wangu, KUSINI imeona bora ichapishe hoja
zinazojengwa na Wana Kusini katika kutia nguvu
hoja yao ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam
kwa njia ya bomba. Kimsingi wakazi wa kusini hawapingi gesi kwenda
nje ya Mtwara na Lindi, wanasema gesi inaweza
kupelekwa kokote Duniani ili mradi iwe iliyosafishwa
tayari kutoka Mtwara na sio mbichi (raw). Wanasema ni vema kiwanda cha kusafisha gesi
kikajengwa Mtwara ili wakazi wa Mtwara wapate
ajira na hivyo kupunguza hali duni ya maisha
inayowakabili kwa sasa, wanahoji ni mwekezaji gani
aliye tayari kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 500
kwenda Mtwara kuwekeza wakati gesi ambayo ingekuwa kigezo cha yeye kwenda huko inapatikana
Dar es Salaam? Wakazi wa mikoa ya kusini wameona kwa macho
yao kule Songosongo Kilwa mkoani Lindi, ambako
gesi imesafirishwa kwenda Dar es Salaam, hakuna
kiwada wala mwekezaji aliyewekeza eneo lile, zaidi
ya ufukara kuzidi kuwaandama wakazi wale. Waungwana husema, kosa si kutenda kosa bali
kurudia kosa. Hoja nyingine ni ile ya mitambo ya kufua umeme
kujengwa Kinyerezi, wanahoji kwanini Dar es
Salaam na sio Mtwara, ipi ni gharama kubwa
kujenga bomba au kutandaza nyaya za umeme?
Jibu hapo ni kutandaza nyaya za umeme ni nafuu,
kwanini basi mtambo huo usijengwe Mtwara halafu umeme ukapelekwa hata Rwanda? Hoja ya KUSINI ni kwamba kwanini tutumie akili
nyingi kuongeza uhamiaji wa watu kutoka vijijini
kwenda mijini badala ya kutatua tatizo? Leo hivi mitambo, viwanda vingejengwa Mtwara
watu wangetoka Dar es Salaam na kwingineko kuja
kufanya kazi Mtwara, watu wangehama mjini na
kukimbilia kijijini, lakini hebu jiulize leo jiji la Dar es
Salaam ndilo tegemeo la pato la Taifa kwa asilimia
zaidi ya 80, iwapo jiji hili litapatwa na janga lolote (siombei) hivi Tanzania itakuwa katika hali gani? Hapa nadhani ni ufinyu wa kufikiri, ndio maana hata
kuhamia Dodoma hawataki wamekaririshwa kuwa
‘Dar ndiyo mpango mzima’ na kwamba kitu kingine
kizuri hakipaswi kuonekana zaidi ya Dar na maeneo
mengine na sio kusini. Wananchi wa mikoa hiyo pia wanaumizwa na
historia ambayo mikoa ya kusini mara baada ya
uhuru ilitangazwa kuwa ni maeneo ya kupigania vita
ya ukombozi kusini mwa Afrika, kwa msingi huo
hakuna maendeleo yeyeto kwa miaka 10, ndiyo
maana barabara za kuingia Lindi na Mtwara hazikutengenezwa. Ndiyo maana Reli ya Kutoka Nachingwea kwenda
bandari ya Mtwara iling’olewa, ndiyo maana mikoa
ya Lindi na Mtwara haikuunganishwa na umeme wa
grid ya Taifa. Watu wa kusini wanahisi kuonewa kwani hata
walipotaka kulima zao la pamba ambalo wataalam
wa kilimo wanathibitisha kuwa linastawi vizuri katika
mikoa hiyo serikali ilipiga marufuku kwa madai wapo
wadudu nchi ya Msumbiji ambao wanaweza kuingia
Tanzania nakuathiri pamba ya kule mikoa za kanda ya ziwa. Wazee wa mikoa hii wanasema kulikuwapo na
makubaliano yasiyo rasmi kuwa baada ya vita vya
ukombozi kwisha mikoa ya kusini ingefidia kwa
kuharakishiwa maendeleo jambo ambalo
halijafanyika hadi leo. Mungu kawaona kawapa gesi, nayo inaondolewa
kupelekwa Dar ndipo wanapohoji Kusini imeikosea
nini Tanzania? Kwani kuna ubaya gani mitambo na
gesi ikibaki Mtwara, sio Tanzania au wakazi wake
hawasitahili? KUSINI inashauri Serikali kutafakari upya jambo hili
vinginevyo linaweza kutupeleka pabaya, hebu
tujifunze kwa wenzetu Sudani Kusini. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Mkulu
Ungeunganisha uzi huu Kwenye main Topic ingeleta umbo la maada Kwa ukamilifu, ila main Topic ikibaki kama ilivyo fishy elements humu Jf ambao husoma heading leaf hupata harufu Kali sana ya kibaguzi, but wakisoma sababu za sure zina mantiki kubwa..
 
Back
Top Bottom