Mtwara kuchele!

Mtwara kuchele!

Hivi karibuni nilibahatika kutembelea mji wa Mtwara. Kwa kweli nimeshuhudia mabadiliko makubwa. ..
Hivi sasa kuna ujenzi wa nyumba za makazi na majengo ya biashara kwa wingi. BoT wanajenga ghorofa kwa ajili ya ofisi zao. Nimeambiwa waheshimiwa wawili wanaotajwa kugombea urais wanajenga pia mahoteli (ya mmoja imekamilika na ndiyo jengo pekee lenye lift mjini Mtwara!).


Barabara za lami zimeongezeka kutoka nne zilizokuwepo mwaka juzi…Benki ya Dunia walifadhili ujenzi wa barabara kadhaa ambazo mojawapo imeanza kuwekwa taa za barabarani (taa za kwanza barabarani mjini Mtwara!). Hata barabara ya kwenda kwa Mkuu wa Wilaya sasa ina lami…
Nimeshuhudia ujenzi wa barabara kwenda feri (kivuko cha kwenda Msanga Mkuu, sawa na Kigamboni kwa Dar). Nikaambiwa pia uundwaji wa kivuko hicho unaendelea vizuri. Kivuko cha Kilambo kwenye Mto Ruvuma kwenda Msumbiji kimekwishamilika…


Ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote umeanza…nimeona Wachina wakiendelea na ujenzi. Upanuzi au uboreshaji wa majengo ya bandari unavutia na unaendelea. Nimeambiwa pia kuna mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege.
Usafiri wa Dar-Mtwara ni wa kutosha na mabasi ya kisasa-Yutong na Higer yanapishana barabarani. Hata barabarani/njiani kati ya Dar na Mtwara (kuanzia Rufiji mpaka Lindi) pameanza kubadilika.
Zuri zaidi, Mtwara hakuna mgao wa umeme kama miji mingi hapa nchini.

Kuna upimaji wa viwanja unaoendelea kwa kasi na hata UTT wamewekeza kwenye mradi wa viwanja. Viwanja mjini vimepanda bei sana…waweza pata kiwanja cha biashara mjini kwa bei ya 800m/-, amini usiamini!

Kuna vituo vitatu vya FM Radio vinavyochangamsha mji…bila kusahau Maisha Club!
Bajaji na Bodaboda ndo usiseme…teksi rasmi ndo hakuna.


Kwa kweli Mtwara ya sasa imeanza kupendeza…Mtwara kuchele! na kwa mwendo huu CCM watashinda tena kwa kishindo huko Mtwara!

acha kuwafanya watu mtwara limbukeni ww fa** Magamba hawana lao pale, unafikiri yale mateso waliyopata hata mwaka hujaisha wameyasahau? Ata km m2 ana kichwa panzi sio kihvyo ndg, jipangeni
 
PANYA ANAPOMLA MTU KISOGONI WAGA ANAMPULIZA! Kilichopo Mtwara Hauwezi Kukifananisha Kabisa Na Mnacho Kiona . CCM Mmetusaliti Nchi Mmewakabidhi Majangiri Wachina. Tunahangaika Hatujui Niwapi Tutaibukia CCM Metisaliti!
 
kwa kufikiria nje ya box!! uko sawa 100%
Ila kosa ni kwamba wapanga miji bado wanachora ramani za kizamani sana!! ila hii ndo ilikuwa nafasi ya kubaidilisha mtwara zaidi hata ya dar na si mwanza tu? maana muda upo, barabara pana, masoko, hospital makazi n.k, ila utajakuta makazi horera na upanuzi wa barabara tena baada ya miaka 5!!

SP

You are right...Lindi, Mtwara na Tanga ndiyo miji iliyopangwa vyema na mkoloni kabla ya uhuru wa Tanganyika. Wapanga mji kwa sasa inatakiwa wafikirie mji wa kisasa ambao hautakuja kutumbukia kwenye kero za Dar katika miaka michache ijayo.

Hatari nyingine kwa sasa ni kule maeneo ya "uzunguni" naona wanabadilisha matumizi ya ardhi...eneo la low density wanaanza kujenga vi-pub na vi-gesti!
 
'class struggle' leads development. sasa ninyi mlio mashambani endeleeni kushangaa!
 
Hivi bado hujapona ule ugonjwa wako? Eti miaka 10 ijayo mtwara itaizidi mwanza! Shame one you. Hiyo miaka kumi unayozungumzia inamaana Mwanza hakutakuwa na shughuli za kiuchumi na hivyo kusitisha maendeleo yake? Ungekuwa unaakiri wewe usingepost ujinga wako. Katafute ripoti ya UN Habitat ujue miji inayokua kwa kasi ukanda wa Afrika mashariki na ndio urudi jamvini...Ukumbuke hapa jamvini hakuna wajinga kama wale uliowalia fedha ya msiba (rambirambi)


Ayasemayo huyu jamaa ni ukweli mtupu kwani Mtwara kuna uwekezaji wa hali ya juu na hata hiyo miaka kumi ijayo naona ni mingi mno kuipita Mwanza. Mwenyewe nimetoka kuwekeza kwenye viwanja huko wiki iliyopita na yote yaliyosemwa nimeyaona.
 
Back
Top Bottom