Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 741
- 281
Hivi karibuni nilibahatika kutembelea mji wa Mtwara. Kwa kweli nimeshuhudia mabadiliko makubwa. ..
Hivi sasa kuna ujenzi wa nyumba za makazi na majengo ya biashara kwa wingi. BoT wanajenga ghorofa kwa ajili ya ofisi zao. Nimeambiwa waheshimiwa wawili wanaotajwa kugombea urais wanajenga pia mahoteli (ya mmoja imekamilika na ndiyo jengo pekee lenye lift mjini Mtwara!).
Barabara za lami zimeongezeka kutoka nne zilizokuwepo mwaka juzi Benki ya Dunia walifadhili ujenzi wa barabara kadhaa ambazo mojawapo imeanza kuwekwa taa za barabarani (taa za kwanza barabarani mjini Mtwara!). Hata barabara ya kwenda kwa Mkuu wa Wilaya sasa ina lami
Nimeshuhudia ujenzi wa barabara kwenda feri (kivuko cha kwenda Msanga Mkuu, sawa na Kigamboni kwa Dar). Nikaambiwa pia uundwaji wa kivuko hicho unaendelea vizuri. Kivuko cha Kilambo kwenye Mto Ruvuma kwenda Msumbiji kimekwishamilika
Ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote umeanza nimeona Wachina wakiendelea na ujenzi. Upanuzi au uboreshaji wa majengo ya bandari unavutia na unaendelea. Nimeambiwa pia kuna mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege.
Usafiri wa Dar-Mtwara ni wa kutosha na mabasi ya kisasa-Yutong na Higer yanapishana barabarani. Hata barabarani/njiani kati ya Dar na Mtwara (kuanzia Rufiji mpaka Lindi) pameanza kubadilika.
Zuri zaidi, Mtwara hakuna mgao wa umeme kama miji mingi hapa nchini.
Kuna upimaji wa viwanja unaoendelea kwa kasi na hata UTT wamewekeza kwenye mradi wa viwanja. Viwanja mjini vimepanda bei sana waweza pata kiwanja cha biashara mjini kwa bei ya 800m/-, amini usiamini!
Kuna vituo vitatu vya FM Radio vinavyochangamsha mji bila kusahau Maisha Club!
Bajaji na Bodaboda ndo usiseme teksi rasmi ndo hakuna.
Kwa kweli Mtwara ya sasa imeanza kupendeza Mtwara kuchele! na kwa mwendo huu CCM watashinda tena kwa kishindo huko Mtwara!