Mtwara: Dk. Kigoda, Tizeba watimuliwa Mtwara

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
MAWAZIRI wawili wa Rais Jakaya Kikwete, jana walionja ‘joto la jiwe’ baada ya wananchi wa Mtwara kuwazomea mkutanoni na hivyo kulazimika kukatiza mkutano wao.

Mawaziri hao ni Dk. Abdallah Kigoda wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, waliokuwa wameongozana na Balozi wa Nigeria hapa nchini, Nshaya Manjabu, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dangote ya Nigeria, Deva Kumar.

Tukio hilo limekuja zikiwa ni wiki chache tangu kutokea kwa vurugu kubwa mkoani humo katika wilaya za Mtwara Mjini na Masasi ambapo wananchi waliharibu mali za baadhi ya viongozi wa kisiasa na serikali na kumuua askari mmoja huku watu wengine wanne nao wakiuawa kwa kupigwa risasi.

Wananchi hao wa Mtwana na Lindi wamekuwa na msimamo mkali wakipinga serikali kujenga bomba la kusafirisha gesi asili kutoka kwao kwenda jijini Dar es Salaam bila kuwekewa mazingira mazuri ya kiuchumi.

Katika kuonyesha kuwa wananchi hao walikuwa wamepania kuwasulubu mawaziri hao, walifika mkutanoni huku baadhi yao wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kuhoji mkutano huo umeruhusiwa na nani wakati serikali imepiga marufuku mikutano na maandano mkoani humo kwa muda.

Mara baada ya viongozi hao kufika uwanjani, Waziri Kigoda aliwasalimia wananchi akisema: “Mtwara oyeee!!!”

Waziri huyo aliitikiwa na wananchi: “Haitoki hata kama umekuja wewe hatutaki wala hatukuelewi! Mlikuwa wapi kuja huku mapema kutuelewesha habari za viwanda?”

Wanachi hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe uliosomeka: “Kauli mbiu: gesi haitoki, tunashukuru baada ya kimya kirefu sasa leo mmefungua rasmi mikutano tukianzia huu mkutano wenu na gesi ndio roho yetu.”

Wakati ‘zomeazomea’ hiyo ikiendelea, baadhi yao walianza kurusha mawe katika hali iliyowalazimu viongozi kuufunga mkutano huku Jeshi la Polisi likiamuru wananchi kutawanyika katika viwanja vya mkutano.

Mara baada ya hali hiyo ya vurugu, Naibu Waziri wa Uchukuzi alilazimika kuwatuliza wananchi ili wasikilize akisema: “Nisikilizeni mtaelewa tu, mwekezaji amepatikana na amemaliza hatua ya kwanza ya kufanya makadilio ya gharama za ujenzi.”

Aliongoza kuwa mamlaka ya viwanja vya ndege inafanya mazungumzo naye ili masharti ya uwekezaji yaweze kufahamika na upanuzi wa uwanja kuanza mapema.

Hata hivyo, wananchi hao hawakutulia huku wakiendelea kupiga kelele na kuwazomea: “Hilo ni changa la macho, hatutaki propaganda zenu, tumechoka na siasa zenu.”

Mkuu wa Mkoa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, hakupata nafasi ya kuzungumza kutokana na wananchi hao kuzomea huku wakimtaka aondoke.

Awali, Kigoda akizungumza katika viwanja vya bandari ya Mtwara na watumishi mbalimbali, alisema kuwa lengo la ujio wake mkoani humo ni makabidhiano ya makontena 38 ya vifaa vya ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dagonte kinachotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Msijute, wilaya ya Mtwara vijijini.

Makabidhiano hayo yalikuwa kati yake na Naibu Waziri wa Uchukuzi. Pamoja na mambo mengine, Kigoda alisema kuwa serikali itaendelea kupokea wawekezaji mbalimbali watakaoomba kuwekeza katika mkoa huo.

Alisema wanaangalia zaidi uwekezaji katika ujenzi wa viwanda kwa kuwa Mtwara ni kitovu cha uchumi wa taifa huku akisisitiza kuwa utafiti wa kitaalamu na kisayansi unaonyesha gesi hapa Mtwara ni nyingi sana.

Alisema viwanda vingi vitajengwa hapa na gesi itakayobaki lazima itapelekwa katika maeneo mengine

Chanzo: Tanzania Daima, Ijumaa 29 Machi 2013.
 
• WAZIRI: MTWARA OYEEE….WANANCHI: HAITOKI

na Mwandishi wetu

Alisema viwanda vingi vitajengwa hapa na gesi itakayobaki lazima itapelekwa katika maeneo mengine.

Rais dhaifu huunda baraza dhaifu la mawaziri.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mtwara hali bado no tete na jamaa wameonyesha msimamo wa ajabu sana kama Alqaida!!
 
GOOD! wamezidi kutudanganya hawa watu.......WANAAMINI WATU/ WANANCHI NI MAAMUMA!
Nawapongeza sana ndugu zangu wa huko kwa kusimama kidete kutetea utajiri uliopo huko kwao, na huu unapaswa kuwa mfano kwa wananchi wote popote pale walipo kupinga kwa vitendo aina zozote za dhuluma zinazofanywa na serikali katika maeneo yao.

Huko nyuma waziri wa nishati na madini alidai gesi iliyogunduliwa huko ni kidogo sana, lakini leo wanasahau na kudai eti Mtwara kuna gesi nyingi......HII NI DALILI YA UTAPELI.
Wao waendelee tu na mipango yao ya kuiendeleza BAGAMOYO kwa kutumia rasilimali zipatikanazo maeneo mengine ya nchi..... HUKUMU YAO YAJA!

Leo wanarejea zile ngonjera zao za eti Mtwara itakuwa kitovu cha uchumi wakati hawataki kuindeleza bandari ya huko.
 
Hizi habari ni nzuri sana na sasa elimu ya uraia imeanza kueleweka vizuri
Bravo ndugu zangu wa Mtwara,uvunaji wa gesi uende sambamba na maendeleo ya Mtwara
 
Ccm hawajui kuwa mabadiliko yapo ndani ya mioyo ya wananchi, ninyi endeleeni na kuwatafutia kesi chadema lakini ipo siku ccm mtalia na kusaga meno.
 
nimeipenda hiyo. yaani viongozi walioongoza kipindi cha JK hawatamsahau. ukilikoroga hamna wa kukutetea bali ujitetee mwenyewe. kama ulaya vile.
sikutarajia kama simbakalia bado yupo mtwara. nilifikiri alishahamishwa. bila shaka hatakuwa na amani ya kuongea na kuongoza kama zamani akiwa mtwara maana wananchi wapo negative toward him.
tena natamani hata mmoja angepatwa na jiwe ili na wengine wajue. kweli JK mtoto wa mujini.
 
Habari kama hii ihuwezi kuikuta sehemu nyingine zaidi ya gazeti la Tanzania Daima.

Ukiisoma na kuipembua, imajaa mashimo mengi ili mradi tu desperate kuleta negative news kuhusu serikali.

Hii wala huwezi kusema ni habari bali ni maoni ya mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima.
 
Si wameziba msikio!!!!, Maadamu si vipofu haka kibubu tutaongea tu.
 
Safi sans wana mtwara,hivi niwaulize kwani muoe hiyo bandari yenu mtaendelea kupaki mitumbwi mpaka Lini?hamstahili lions mameli makubwa yanakuja kupakia korosho na budhaa nyinginezo kutoka kwenye viwanda vyenu na kwenda kuuza nje?Amkeni wamakonde na wana kusini wote tuikomboe tanganyika yetu dhidi ya huyu kaburu mweusi masisiem ambayo yanajitapa eti nyie ndio mtaji wao!!!!!!!
 
Habari inapochanganywa na maoni ya mwandishi, matokeo yake hata mantiki na flow inapotea hewani.

Kwa mtaji huu, siyo ajabu hata wananchi wanajikuta wana weweseka kimtazamo na kifkra.
 
Mbona Waziri kigoda anasema"gesi iliyogunduliwa Mtwara ni nyingi sana"lkn Waziri Mhongo alisema"Mtwara wana gesi chache mno na gesi nyingi ipo kwenye deep sea ambayo sio mali ya Mtwara kama mkoa"!Kauli gongana hizi tumuamini nani!
 
Habari kama hii ihuwezi kuikuta sehemu nyingine zaidi ya gazeti la Tanzania Daima.Ukiisoma na kuipembua, imajaa mashimo mengi ili mradi tu desperate kuleta negative news kuhusu serikali.Hii wala huwezi kusema ni habari bali ni maoni ya mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima.
Mng'oeni kucha
 
Habari inapochanganywa na maoni ya mwandishi, matokeo yake hata mantiki na flow inapotea hewani.Kwa mtaji huu, siyo ajabu hata wananchi wanajikuta wana weweseka kimtazamo na kifkra.
Nnalo Hilo na dhuluma zenu kawaambie masisiem wenzako wananchi wameamka na ule Wizi wenu wameushtukia keyjei kawatosa mnapiga kelele Kama mazuzu!!!
 
Back
Top Bottom