well said.....Lizzy sidhani kama umemuelewa vizuri Bishanga huyo Cindy hajalaumu kuhusu watoto wala divorce kilichotokea ni yeye kuongea na huyo mwanaume na baada ya hapo mwanaume akachanja mbuga! Hata ingekua mimi ningejiuliza kulikoni ina maana baada ya kujua kuwa ni mtaliki na ana watoto ndio kasoro mojawapo au?
Sikatai huyo Cindy ni binadamu na anaweza kuwa na mapungufu yake kama binadamu mwingine yoyote.
Cindy ana akili sana ila huyo mwanamume ni very smart na genius wa karne!!
Babu DC!!
The Boss na BabuDC,ina maana mtalaka mwenye watoto hadi deserve kuwa na mwenza?
Nimepokea ombi maalum toka kwa mama chanja wangu mtarajiwa ,anasema kuna mtu kamwomba ushauri,katika hili naye anaomba mchango wenu.
Ni hivi:
Kuna mdada mmoja (tumwite Cindy), Cindy aliolewa na akaachika.Alipata watoto wawili kwenye ndoa yake na anaishi mwenyewe na wanae.Majuzi kuna baba mmoja aliingia kwenye ofisi ya dada yake Cindy (tumwite Brenda) na hapo ofisini huyo baba aliona picha ya Cindy na akamtunuku. Alijitahidi kuomba contact za Cindy lakini Brenda akawa anakataa.Jamaa king'ang'anizi pamoja na Cindy kumwambia dada yake asitoe contact zake lakini tokana na presha yajamaa mwisho Brenda alimpa jama namba ya Cindy.Zikanza simu na sms zisizoisha mpaka Cindy akakubali akutane na jamaa.Wakakutana,wakala,wakanywa,in the process Cindy akamweleza jama ukweli kuwa yeye ni divorcee with two kids.Kuanzia siku hiyo hajamsikia wala kumwona jamaa tena.
Cindy anajiuliza hivi jamaa kakimbia kisa ana watoto? Au kisa ni u divorcee?apparently dada yake kumbe hakumweleza jamaa kuwa cindy aliwahi kuolewa na ana watoto.
Hivi wanaume mnakerwa kuwa na mwanamke mwenye watoto/divorcee,kwa nini?
mimi sikumaanisha hivyo
na wala nilivyomuelewa DC sivyo hivyo
mimi na DC tunaona hapa kitendo cha mdada kusema ukweli mapema ni cha kijasiri
na cha akili na cha kupongezwa
na vile vile kwa mwanaume kuwa mkweli hawezi na hataki pia ni kitendo cha ujasiri na cha kupongezwa
kuliko 'wangedanganyana' na kuwatesa watoto wasio na hatia....
asante DC
umeonesha busara mno hapa..
mwanaume anapokimbia bila kufanya 'uchafuzi'
anapaswa kupongezwa
The Boss na BabuDC,ina maana mtalaka mwenye watoto hadi deserve kuwa na mwenza?
Ahsante sana mkuu,
Tafsiri yangu ni kuwa these guys are real....no faking!!
Babu DC!!
Dark City naomba nikuulize swali ila mtu yoyote anakaribishwa kulijibu. Hivi wewe kama mwanaume ukiwa unamtaka mwanamke(na huna uhakika kama hana bwana) ukawa kila ukimpigia simu yuko home hata iwe late(yani mida yoyote,after working hrs)hana cha weekend wala nini. Huyo mwanamke utamfikiriaje???anafaa au anaogopesha kupelekea ww uchanje mbuga lol......nataka kujua wanaume in general(ama wengi wenu)huwa mnamuonaje mtu kama huyo.
Bishanga,
Hatuongelei suala na kudeserve au la, tunaongelea suala la kuwa na mwenza amabaye yuko tayari kumbema mtalaka na mizigo yake yote...Mara nyingi watu wanakuja na ajenda zao na mtu kama huyo dada anatumiwa kwama daraja tu!!
Babu DC!!
Naomba ueleze zaidi ili ueleweke,
Kwa kili hii ya uzee, bado sijakuelewa!!
Babu DC!!
. swali langu ni kuwa mwanaume anapokutana na mwanamke wa namna hii,anafurahia au anamshangaa kuwa kwanini hajichanganyi?.