Mtumishi wa mungu na traffic

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Mtumishi wa MUNGU mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police.
Police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi, mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? Mbona gari lako matairi yameisha, Wakati wote huo Mtumishi wa Mungu hakuelewa cha kufanya, hatimaye polisi akamuamuru Mchungaji waende nae kituoni.
Njiani polisi alimuuliza, umesema wewe ni Mtumishi wa MUNGU? Je, una biblia ndani ya gari?, akajibu ndio ninayo.
Polisi: Pack gari pembeni na nionyeshe biblia.
Mtumishi akapaki gari na kutoa biblia, Polisi akamuamuru Mtumishi 'fungua na usome Mathayo 5:25-26." Mtu wa Mungu akasoma, Imeandikwa hivi:- "Patana na Mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani: yule mshtaki asijekukupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.Amin nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho".
Mtumishi wa Mungu akampa polisi yaliyo ya kaisari.
Polisi akatabasamu na kumuwekea mkono kichwani mtumishi huku akisema "Msifanye migumu mioyo yenu". Enenda kwa amani.
 
Nimeipenda
 
Back
Top Bottom