Huyu kijana mdogo ametokea kwenye ubunge na kuwa waziri ndani ya miaka miwili tu ameshakua tajiri na utajiri unaokimbizana na wale mafisadi kina Lowasa na kina Chenge! hii haiwezekani lazima achukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria ikiambatana na viboko 12 siku anaingia jela na siku anatoka jela anapata viboko 12 akamwadisie mkewe!
you are 'marked for death'!
Pole sana kwa kupata likizo yenye malipo,vp ulikuwa kimya mpaka ripoti ya kamati ya bunge imnase maige?na vp? Dili za wanyama pori washkaji wanakushirikisha au likizo mpaka huko?
Ndugu Mwenyekiti wa jukwaa hili,
Mimi naitwa Toto M. Kassi, Afisa Misitu Wilaya ya Same. Tarehe 23.12.2010 Mheshimiwa Waziri Ezekiel Maige, tukiwa kwenye Msitu wa Hifadhi Asilia ( Nature Reserve) wa Serikali Kuu wa Chome Wilayani Same, bila kujali misingi ya utawala bora, Waziri Maige alinisimamisha kufanya kazi za misitu na Mkurugenzi wa Misitu akaniandikia barua tarehe 07.01.2011 kutekeleza amri ya Waziri Maige.
Hivyo basi, kuanzia tarehe 07.01.2011 hadi hii leo naendelea kulipwa mshahara bila kufanya kazi. Msituni. watu wanaofanya uharibifu ikiwamo uvunaji haramu wa misitu ya asili bado wanaendelea na vitendo vyao hivyo. Sababu ya kusimamishwa kazi kwangu ni kwamba
nimezuia wavunaji misitu na wachimbaji madini ambao wana maslahi na Mkuu wa Wilaya ya Same na Mheshimiwa Maige mwenyewe.
Mimi sio mtumishi wa Wizara yake. Nipo Tamisemi ingawa kitaaluma ni Afisa Misitu. Ukweli ajira yangu haiko kwake, Waziri
amekurupuka kwa nia mbaya. Labda kosa langu ni kutetea rasilimali za umma zisihujumiwe. Vinginevyo sina kosa lolote na ndio maana mpaka sasa kujua nini iwe hatma yangu kiajira mbali ya kunilipa mshahara kila mwezi bila kufanya kazi. Nimefika Wizarani mara mbili. Ukweli pale Wizarani wanamwogopa sana Maige. Kila mtu anaogopa kushughulikia malalamiko yangu. Waziri anawatisha na wengine
kuwasimamisha kazi hovyo kwa maslahi yake.
Ndugu Mwenyekiti, Malalamiko yangu yako Tamisemi na Idara Kuu ya Utumishi. Tume ya Utumishi wa Umma na wizarani kwenyewe. Sijui hatima yangu, lakini ukweli mpaka sasa nalipwa mshahara bure, bila ya kufanya kazi. Ni mimi, Toto Kassi Mjumbe aliyewekwa
kijiweni na Waziri Maige ( Niko tayari kutoa ushahidi wa niliyoyaeleza hapa;
0784 715977)
Serikali ya kihuni,kitapeli nk hii,eti waziri anamuhonga mhudumu wa ndege $3000 ili apate kukubaliwa kimapenzi tu!mkuu si kua watufafanulie tu walipataje hizo mali bali walitakiwa kufikishwa mahakamani kama kina mramba,kufungwa na kutaifishwa pia!ila kwa kua hawa ni washkaji wa mzee wa visasi basi tusitarajie ilo
namba ya simu hiyo hapo, nenda hewani kama unataka details zaidi.Kwenye barua ya kusimamishwa umeandikwa charge zipi ambazo ndo basis ya kusimamishwa? Lakini kama mwajiri wako umesema ni tamisemi inakuaje mkurugenzi wa misitu ambaye yupo wizara ya malialisi awe na mamlaka ya kukusimmisha? Je mwajiri wako alisemaje? Kama vipi tuwekee madocument hapa tuyaone.