Mtumishi anadai: "Nalipwa mshahara bila kufanya kazi kwasababu ya Maige"

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
( Madai haya yamefikishwa na mtumishi wa umma kwenye http://mjengwablog.com)

Ndugu Mwenyekiti wa jukwaa hili,

Mimi naitwa Toto M. Kassi, Afisa Misitu Wilaya ya Same.


Tarehe 23.12.2010 Mheshimiwa Waziri Ezekiel Maige, tukiwa kwenye Msitu wa Hifadhi Asilia ( Nature Reserve) wa Serikali Kuu wa Chome Wilayani Same, bila kujali misingi ya utawala bora, Waziri Maige alinisimamisha kufanya kazi za misitu na Mkurugenzi wa Misitu akaniandikia barua tarehe 07.01.2011 kutekeleza amri ya Waziri Maige.

Hivyo basi, kuanzia tarehe 07.01.2011 hadi hii leo naendelea kulipwa mshahara bila kufanya kazi. Msituni. watu wanaofanya uharibifu ikiwamo uvunaji haramu wa misitu ya asili bado wanaendelea na vitendo vyao hivyo.

Sababu ya kusimamishwa kazi kwangu ni kwamba nimezuia wavunaji misitu na wachimbaji madini ambao wana maslahi na Mkuu wa Wilaya ya Same na Mheshimiwa Maige mwenyewe.

Mimi sio mtumishi wa Wizara yake. Nipo Tamisemi ingawa kitaaluma ni Afisa Misitu. Ukweli ajira yangu haiko kwake, Waziri amekurupuka kwa nia mbaya. Labda kosa langu ni kutetea rasilimali za umma zisihujumiwe. Vinginevyo sina kosa lolote na ndio maana mpaka sasa kujua nini iwe hatma yangu kiajira mbali ya kunilipa mshahara kila mwezi bila kufanya kazi.

Nimefika Wizarani mara mbili. Ukweli pale Wizarani wanamwogopa sana Maige. Kila mtu anaogopa kushughulikia malalamiko yangu. Waziri anawatisha na wengine kuwasimamisha kazi hovyo kwa maslahi yake.

Ndugu Mwenyekiti,
Malalamiko yangu yako Tamisemi Idara Kuu ya Utumishi. Tume ya Utumishi wa Umma na wizarani kwenyewe. Sijui hatima yangu, lakini ukweli mpaka sasa nalipwa mshahara bure, bila ya kufanya kazi.

Ni mimi, Toto Kassi
Mjumbe aliyewekwa kijiweni na Waziri Maige

( Niko tayari kutoa ushahidi wa niliyoyaeleza hapa; 0784 715977)
 
Duh! tuhuma, uzembe, ubadhirifu kila kukicha.
Ni vizuri Toto umefika hapa kuweka na kubainisha wazi namna Maige alivyo mzembe na mbabe kwa hasara ya Taifa. Tuhuma hizi na viambatanisho vitumike wakati Maige anasimama mahakamani.
 
Kila kukicha ubadhirifu, ubabe na ufisadi wa mawaziri wa kikwete unazidi kujidhihirisha, wanaumbuka kwa matendo yao maovu wanayoyafanya. Maige bila shaka atakuwa ndiye waziri mbadhirifu kuliko wote katika cabinet ya kikwete.

Nadhani sasa umefika wakati wa wananchi tuchukue hatua dhidi ya hawa mawaziri wanaofanya kazi za kuhujumu rasilimali zetu badala ya kuzilinda kama walivyoapa. Huu ni ushahidi mwengine kwamba maige amejinufaisha kifisadi na kuwepo kwake wizara ya maliasili na utalii. Hii ninaiongezea juu ya utoroshwaji wa wanyamahai kwenda uarabuni uliofanyika mwaka jana.

Waziri maige ni muhimu akafilisiwa kwani dalili zote zinaonyesha kwamba yeye ndiye kiongozi wa genge la wahujumu wa rasilimali zetu nchini.
 
Uharibifu wa mazingira Same unatisha. Maeneo ya Chome kuna udongo wa boxte unachimbwa na kupelekwa Kenya na pia licha ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kufukuzwa wapo wakubwa wanaoendeleza uchimbaji. Tunasikitika sana Mbunge wetu anatambua hilo ila amekaa kimya
 
Hivi hata wakipigwa chini hawa mawaziri, haitakuwa busara na ucha Mungu endapo tukiwataka watufafanulie wamepataje mali walizo nazo, na wakishindwa tuzitaifishe?

Mkuu kawaida ukitaka kuadhibu ni kutoa adhabu iyakayouma zaidi-kwa kuwa mawaziri wetu hawa mali wanazipenda sana, nadhani adhabu itakatowaumiza zaidi ni kufilisi mali zao zote walizonazo-hiyo pekee ndio itakayowaumiza zaidi ya kuvua tu uwaziri!!
 
Hakika mimi ndie mzalendo pekee niliyebaki katika nchi hii. Huyu Maige afilisiwe, ni nyang'au mkubwa sana!
 
Katika historia ya nchi hii hakuna waziri wa mali asili na utalii aliyeweza kuweka hadharini ufisadi kama huu wa Maige! Anayemfuatia alikua ni Zakia Hamdani Mehggi lakini huyu mama alikua anakula na kupuliza! 100% Maige anahusika na wale Twiga waliosafirishwa pale Kilimanjaro International Airport na wanyama wengine sheria ichukue mkondo wake.
 
mwanaichi iliripoti MAIGE kumpa mhudumu wa ndege dola 3000 huku maige akiomba namba ya simu ya yule mdada

dada mwanzoni aligoma kuzipokea ila baada ya dakika kadhaa akachukua huu mshiko
 
Sababu ya kusimamishwa kazi kwangu ni kwamba nimezuia wavunaji misitu na wachimbaji madini ambao wana maslahi na Mkuu wa Wilaya ya Same na mhe. maige


nimeipenda hiyo kweli baba mwanaasha kazi anayo
 
Hivi hata wakipigwa chini hawa mawaziri, haitakuwa busara na ucha Mungu endapo tukiwataka watufafanulie wamepataje mali walizo nazo, na wakishindwa tuzitaifishe?

Serikali ya kihuni,kitapeli nk hii,eti waziri anamuhonga mhudumu wa ndege $3000 ili apate kukubaliwa kimapenzi tu!mkuu si kua watufafanulie tu walipataje hizo mali bali walitakiwa kufikishwa mahakamani kama kina mramba,kufungwa na kutaifishwa pia!ila kwa kua hawa ni washkaji wa mzee wa visasi basi tusitarajie ilo
 
mwanaichi iliripoti MAIGE kumpa mhudumu wa ndege dola 3000 huku maige akiomba namba ya simu ya yule mdada

dada mwanzoni aligoma kuzipokea ila baada ya dakika kadhaa akachukua huu mshiko
Ya kweli haya??
 
mwanaichi iliripoti MAIGE kumpa mhudumu wa ndege dola 3000 huku maige akiomba namba ya simu ya yule mdada

dada mwanzoni aligoma kuzipokea ila baada ya dakika kadhaa akachukua huu mshiko
haka kastori kameni imprec ebu dadavua
 
you are 'marked for death'!

embu kuwa mkweli. Ni kwani nini uliomba kazi? Nadhani unaweza kuja na majibu marefu mengi na marefu sana lakini hitimisho litakuwa uliomba kazi ili upate kulipwa mshahara. Sasa kama unalipwa mshahara hata bila ya kufanya kazi unaangaika nini?

Au unataka kutuambia kuwa unapata maslahia zaidi ya mshahara unapokuwa kazi? Dili za kuchuma mazao kwenye hizo mbunga sasa upati tena kwa sababu huuendi kazini.

 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom