Mtuhumiwa wa kutorosha wanyamapori alikuwa na vibali vyote halali kutoka Serikalini

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
RAIA wa Pakistan, Kamran Ahmed, aliyetuhumiwa na kisha kutiwa hatiani katika kashfa ya kutorosha wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti, alikuwa na vibali vyote halali kutoka serikalini, Raia Mwema linaweza kuthibitisha.

Mpakistan huyo alitoweka akiwa chini ya dhamana, akahukumiwa bila kuwapo mahakani na sasa imedhihirika kwamba kutoweka kwake kulikuwa ni kuficha ushiriki wa vigogo katika mpango wa kuuziana wanyama hao.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema, umebaini kwamba Kamran Ahmed alikuwa na vibali vyote muhimu vya kusafirisha wanyama hao pamoja na hati ya makubaliano (MoU), kati yake na Idara ya Wanyamapori ya Tanzania.

Wanyama hao hai wenye thamani ya shilingi milioni 170 za Tanzania walisafirishwa Novemba 26, 2011, kwa Ndege ya Jeshi la Qatar (Emir Air force) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Hati ya makubaliano (MoU) ambayo Raia Mwema inayo nakala yake, inaonyesha kuwa kulikuwa na makubaliano kimaandishi baina ya Kamran, kama Wakala wa Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) na Erasmus Tarimo, kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.

Tarimo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori kati ya mwaka 2007 na 2011, kabla ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Alitia saini hati hiyo Mei 28, 2009 kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, imebainika kuwa kabla kutiwa saini makubaliano hayo, ofisa wa Serikali ya Tanzania aliyetambulika kwa jina moja la Midele alikwenda Karachi-Pakistan kukagua bustani ya kutunzia wanyama (zoo) ambako wangepelekwa wanyama hao kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa picha zilizopatikana kutoka vyanzo vya uhakika vya habari vya gazeti hili, Midele anaonekana akiwa mbele ya lango la kuingilia katika bustani wakati nyingine zinamwonyesha akiwa na maofisa kadhaa wa Serikali ya Pakistan katika “miondoko” tofauti.

Taarifa zinadai kuwa Midele alikwenda Pakistan kwa kulipwa gharama zote na Kamran, ikiwa ni pamoja na posho za kujikimu, nauli ya ndege na gharama ya malazi. Baada ziara hiyo, hati hiyo ya makubaliano ndipo ilipotiwa saini.

Hati hiyo yenye kurasa nne ina vipengele 16 na imeainisha kuwa wanyama watakaokamatwa na kusafirishwa hawatatumika kwa shughuli za kibiashara.

“Malengo ya Hati (MoU) hii ni kujulisha ridhaa ya Wizara ya Malialisili na Utalii kuipatia Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) tembo watoto wanne (4), kwa ajili ya Zoo (bustani ya kuhifadhia wanyama) ya Karachi na hifadhi, kwa madhumuni ya kutoa elimu na uhifadhi,” inasema sehemu ya kwanza ya hati hiyo.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja iwapo bustani ya wanyama ya Karachi ni ya kibiashara au kwa ajili ya huduma za kijamii.

Nyaraka zaidi zinabainisha kuwa katika kashfa hiyo, maofisa wa Idara ya Wanyamapori Tanzania ndiyo waliohusika kuwakamata twiga hao na wanyama hai wengine, wakilipwa posho na Kamran.

Aidha, pia vitendo hivyo vimefanyika kinyume cha Sheria ya Tanzania ya Wanyamapori (Wildlife Conservation Act) ya mwaka 2009, ambayo inazuia biashara ya wanyamapori hai.

Sura ya 5 kifungu cha (2) kipengele (a) (b) na (c) kinafafanua kuwa mtu au taasisi itaruhusiwa kukamata mnyama wa aina yoyote kwa sababu tu za utafiti, elimu, kiutamaduni na si kwa sababu za kibiashara.

Uchunguzi unaonyesha kuwa katika kipindi chote wakati biashara hiyo ikifanyika nyaraka za serikali zilitumika tu kwa malengo ya kujikinga na mkono wa sheria pale mambo yatakapoharibika.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kamran alikuwa anawalipa maofisa wote wa serikali waliofanikisha mipango hiyo kwa fedha za kigeni kati ya dola za Marekani 20,000 na 50,000 kama “huduma ya kuwanunua” wanyama hao.

“Katika kipindi cha miaka miwili kabla ya kufichuliwa kwa kashfa hiyo maafisa wa Idara ya Wanyapori walipokea fedha kutoka kwa Kamran kama rushwa na wao walimtengenezea nyaraka za kiserikali ili wanyama wafike salama huko sokoni,” anadai mmoja wa watu wa karibu wa Kamran.

Kwa mujibu msiri huyo, Kamran alikuwa na mtandao mpana wa usafirishaji wanyama hai duniani kiasi cha kuwekwa katika orodha maharamia 139 waliokuwa wanatafutwa na Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika nchi 36 dunia kote.

Operesheni ya kuwatafuta watu hao ilipewa jina la “infra terra” na ilizinduliwa Oktoba mwaka 2014 na Kamran alikuwa mtu wa 17 katika orodha hiyo.

Mtandao wa Kimataifa wa Interpol unamtaja Kamran kuwa ni raia wa Pakistani, aliyezaliwa mwaka 1985, anatafutwa na Serikali ya Tanzania kwa kosa la kusafirisha wanyama hai kutoka Tanzania kwenda Qatar. Interpol wanaeleza kuwa Kamran alilipa gharama za usafiri wa ndege ya kijeshi iliyopakia twiga na swala kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Qatar.

Kwa mujibu wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (World Wildlife Fund - WWF), utoroshaji wa wanyama hai ni biashara kubwa inayoendeshwa na mtandao hatari wa kimataifa.

Mtandao huo husafirisha wanyama hai na viungo vya wanyama kama ilivyo kwa dawa za kulevya na silaha.
Kutokana na jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa, mfuko huo unakiri kuwa ni vigumu kujua kwa uhakika gharama halisi ya biashara hiyo haramu.

Lakini wataalamu mbalimbali wanakadiria thamani ya biashara hiyo kuwa Dola za Kimarekani bilioni 20, na kuifanya kuwa ni biashara haramu ya nne inayoingiza pesa nyingi duniani, ikitanguliwa na dawa za kulevya, noti bandia na usafirishaji wa binadamu.

- Source: Raia Mwema - Aibu,aibu
 
Just thinking here huyu mkwele angepewa miaka mingine mitano mbele, cjui ingekuaje wallah
 
Ccm walishauza hii nchi mika mingi iliyopita. Kilichobakia ilikuwa ni kutuuza tu raia.
 
Hivi haya majipu aliyodai atayatumbua na tumuombee anaanza kuyatumbua lini?

Mpaka sasa mimi naona wanatumbua vipere na vichunusi tu ............ kama hawajui majipu, basi haya ndiyo majipu!!

Kwa kazi aliyoifanya mpaka sasa wala hahitaji maombi maana sioni kama kuna hatari yeyote kwa utumbuaji wa vipere na vichunusi!! Siku tukisikia wameanza na issue za Richmiond, EPA, Escrow, Meremeta, Wanyama, Dawans, IPTL then itabidi nchi ianze maombi kumuombea Rais kama alivyotuomba.

Pamoja na zihaka zinazofavywa, Kikwete alikuwa jasiri mpaka akina Mramba na Yona wanasota jela mpaka leo!!
 
..sasa kama kuna signed MoU yenye kuonyesha bustani za wanyama zilipo(karachi) kwanini uchunguzi usifanyike na wenye bustani hizo kukamatwa kwa uchunguzi??...ama huyo Tarimo kama alisaini kwa niaba ya TZ kwanini asitafutwe huko kijijini kwake rombo anakokula pension ili asadie uchunguzi??....nchi hii imebakwa vya kutoshwa na hawa wezi....
 
kamran alikua anashushia wanyama nyumbani kwake alikua anafanya bila kificho inamaana alikua n vibali vyote.....na ofisi yke ilikua hapo stand ndogo y hiace jengo la mollel
 
Kamran kipindi hicho atakuwa alikuwa kwenye late twenties na kawaingiza mjini mafala kalala mbele na wanyama 140 na ushehe...
 
RAIA wa Pakistan, Kamran Ahmed, aliyetuhumiwa na kisha kutiwa hatiani katika kashfa ya kutorosha wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti, alikuwa na vibali vyote halali kutoka serikalini, Raia Mwema linaweza kuthibitisha.
Mpakistan huyo alitoweka akiwa chini ya dhamana, akahukumiwa bila kuwapo mahakani na sasa imedhihirika kwamba kutoweka kwake kulikuwa ni kuficha ushiriki wa vigogo katika mpango wa kuuziana wanyama hao.
Uchunguzi wa muda mrefu wa Raia Mwema, umebaini kwamba Kamran Ahmed alikuwa na vibali vyote muhimu vya kusafirisha wanyama hao pamoja na hati ya makubaliano (MoU), kati yake na Idara ya Wanyamapori ya Tanzania.

Wanyama hao hai wenye thamani ya shilingi milioni 170 za Tanzania walisafirishwa Novemba 26, 2011, kwa Ndege ya Jeshi la Qatar (Emir Air force) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Hati ya makubaliano (MoU) ambayo Raia Mwema inayo nakala yake, inaonyesha kuwa kulikuwa na makubaliano kimaandishi baina ya Kamran, kama Wakala wa Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) na Erasmus Tarimo, kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.
Tarimo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori kati ya mwaka 2007 na 2011, kabla ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Alitia saini hati hiyo Mei 28, 2009 kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, imebainika kuwa kabla kutiwa saini makubaliano hayo, ofisa wa Serikali ya Tanzania aliyetambulika kwa jina moja la Midele alikwenda Karachi-Pakistan kukagua bustani ya kutunzia wanyama (zoo) ambako wangepelekwa wanyama hao kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa picha zilizopatikana kutoka vyanzo vya uhakika vya habari vya gazeti hili, Midele anaonekana akiwa mbele ya lango la kuingilia katika bustani wakati nyingine zinamwonyesha akiwa na maofisa kadhaa wa Serikali ya Pakistan katika “miondoko” tofauti.
Taarifa zinadai kuwa Midele alikwenda Pakistan kwa kulipwa gharama zote na Kamran, ikiwa ni pamoja na posho za kujikimu, nauli ya ndege na gharama ya malazi. Baada ziara hiyo, hati hiyo ya makubaliano ndipo ilipotiwa saini.

Hati hiyo yenye kurasa nne ina vipengele 16 na imeainisha kuwa wanyama watakaokamatwa na kusafirishwa hawatatumika kwa shughuli za kibiashara.
“Malengo ya Hati (MoU) hii ni kujulisha ridhaa ya Wizara ya Malialisili na Utalii kuipatia Halmashauri ya Jiji la Karachi nchini Pakistan (CDGK) tembo watoto wanne (4), kwa ajili ya Zoo (bustani ya kuhifadhia wanyama) ya Karachi na hifadhi, kwa madhumuni ya kutoa elimu na uhifadhi,” inasema sehemu ya kwanza ya hati hiyo.
Hata hivyo, haikufahamika mara moja iwapo bustani ya wanyama ya Karachi ni ya kibiashara au kwa ajili ya huduma za kijamii.

Nyaraka zaidi zinabainisha kuwa katika kashfa hiyo, maofisa wa Idara ya Wanyamapori Tanzania ndiyo waliohusika kuwakamata twiga hao na wanyama hai wengine, wakilipwa posho na Kamran.
Aidha, pia vitendo hivyo vimefanyika kinyume cha Sheria ya Tanzania ya Wanyamapori (Wildlife Conservation Act) ya mwaka 2009, ambayo inazuia biashara ya wanyamapori hai.
Sura ya 5 kifungu cha (2) kipengele (a) (b) na (c) kinafafanua kuwa mtu au taasisi itaruhusiwa kukamata mnyama wa aina yoyote kwa sababu tu za utafiti, elimu, kiutamaduni na si kwa sababu za kibiashara.

Uchunguzi unaonyesha kuwa katika kipindi chote wakati biashara hiyo ikifanyika nyaraka za serikali zilitumika tu kwa malengo ya kujikinga na mkono wa sheria pale mambo yatakapoharibika.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kamran alikuwa anawalipa maofisa wote wa serikali waliofanikisha mipango hiyo kwa fedha za kigeni kati ya dola za Marekani 20,000 na 50,000 kama “huduma ya kuwanunua” wanyama hao.

“Katika kipindi cha miaka miwili kabla ya kufichuliwa kwa kashfa hiyo maafisa wa Idara ya Wanyapori walipokea fedha kutoka kwa Kamran kama rushwa na wao walimtengenezea nyaraka za kiserikali ili wanyama wafike salama huko sokoni,” anadai mmoja wa watu wa karibu wa Kamran.
Kwa mujibu msiri huyo, Kamran alikuwa na mtandao mpana wa usafirishaji wanyama hai duniani kiasi cha kuwekwa katika orodha maharamia 139 waliokuwa wanatafutwa na Polisi wa Kimataifa (Interpol) katika nchi 36 dunia kote.

Operesheni ya kuwatafuta watu hao ilipewa jina la “infra terra” na ilizinduliwa Oktoba mwaka 2014 na Kamran alikuwa mtu wa 17 katika orodha hiyo.
Mtandao wa Kimataifa wa Interpol unamtaja Kamran kuwa ni raia wa Pakistani, aliyezaliwa mwaka 1985, anatafutwa na Serikali ya Tanzania kwa kosa la kusafirisha wanyama hai kutoka Tanzania kwenda Qatar. Interpol wanaeleza kuwa Kamran alilipa gharama za usafiri wa ndege ya kijeshi iliyopakia twiga na swala kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Qatar.
Kwa mujibu wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (World Wildlife Fund - WWF), utoroshaji wa wanyama hai ni biashara kubwa inayoendeshwa na mtandao hatari wa kimataifa.

Mtandao huo husafirisha wanyama hai na viungo vya wanyama kama ilivyo kwa dawa za kulevya na silaha.
Kutokana na jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa, mfuko huo unakiri kuwa ni vigumu kujua kwa uhakika gharama halisi ya biashara hiyo haramu. Lakini wataalamu mbalimbali wanakadiria thamani ya biashara hiyo kuwa Dola za Kimarekani bilioni 20, na kuifanya kuwa ni biashara haramu ya nne inayoingiza pesa nyingi duniani, ikitanguliwa na dawa za kulevya, noti bandia na usafirishaji wa binadamu.

- Source: Raia Mwema - Aibu,aibu
atakuwa mbowe ndo alimpa:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Wanyama 130 kwa shilingi milioni 170, Ina maana kila mmoja ni kama 1.3 milioni. Mbona ni ndogo sana karibu sawa na wale mbwa wa polisi. Hivyo hawawezi kurudishwa?
 
Daaaah ERASMUS TARIMO tenaaaa :cool: :eek: ....Haki ya Mola sasa ninaanza kuamini,japo mwanzo ilikuwa ngumu sana.
 
..sasa kama kuna signed MoU yenye kuonyesha bustani za wanyama zilipo(karachi) kwanini uchunguzi usifanyike na wenye bustani hizo kukamatwa kwa uchunguzi??...ama huyo Tarimo kama alisaini kwa niaba ya TZ kwanini asitafutwe huko kijijini kwake rombo anakokula pension ili asadie uchunguzi??....nchi hii imebakwa vya kutoshwa na hawa wezi....
Mkuu huyo Tarimo hawezi Fanya jambo kubwa Na LA hatari hivyo peke yake,
 
alikuwa na 26 years kudadeki. wazee na maupara yao akawalamba chenga kama gaucho.
 
Back
Top Bottom